Mimi ni muumini na mfuasi mzuri wa Mwalimu, Hayari Baba wa Taifa (Rais wenu hataki kumwita hivyo, anamwita mzee, kamwambukiza hata Membe). I believe Mwalimu was a great foreseer, karibu mambo mengi ambayo aliyasemea way back during his regime hata baada ya kustaafu, hasa miaka ya 90, yametokea.
Nani hajui kuwa mwalimu alishangaa kuona kuna jina la Lowassa katika miongoni mwa wagombea mwaka 1995, nani hajui kuwa mwalimu hakutaka mgombea urais mwenye asili ya kijeshi, mwenye makundi, anayependa kuwa na kundi kusaka uongozi, nani hajui kuwa mwalimu alitishwa na utajiri wa Lowassa namna ulivyopatikana kwa njia zisizo halali?
Mwalimu hakuwahi kumchukia mtu kwa utajiri wake, alichukia namna iliyotumika kupata utajiri, hasa njia za haramu, watu kujitajirisha kwa jasho la wengine au kwa kuhujumu, rushwa (ufisadi). Nimewahi kusikia namna Mwalimu alivyomshangaa Lowassa mbele ya watu kuwa kaupataje ukwasi, nasikia ilikuwa mbele za watu ubalozi fulani hivi. Nani asiyejua kuwa Lowassa kachafuka kwa tuhuma za ufisadi mkubwa nchi hii. I normally argue kuwa Mwalimu hakumpatia baraka Lowassa (unaweza kusema alimlaani).
Angalia wote ambao Mwalimu hakuwasema vizuri au hakuwataka kwa sababu ya matendo yao, wako wapi leo hii. Angalia wote ambao mwalimu aliwataka kwa sababu ya uadilifu wao, wako wapi leo hii.
Aliwasema vibaya au hakuwataka akina Malecela, Kikwete mwenyewe, kina Lowassa na wengine wengi mnaweza kunisaidia. Angalia tulivyopuuza ushauri wake mwingi nini kinachotokea? What is happening now with a lote of practicals on the ground is what Mwalimu Exactly cautioned several times.
Mwalimu aliwasema vizuri au kuwataka akina Salim Ahmed Salim, akina Kawawa, akina Sokoine, Mkapa, na wengine wengi, ndiyo leo ni watu wa kuheshimiwa na kukumbukwa kwa uadilifu na uzalendo kwa maendeleo ya watu na taifa.
Lowassa hajawahi kuwa msafi pamoja na side B yake katika utendaji na usimamizi wa mambo. Moja ya ishara nzuri kuwa si msafi ni jitihada zilizopo sasa za kumsafisha, kama ni msafi kwa nini asafishwe. Kitu kimoja hakijui, pamoja na uwezo wake wa kiakili, ni kuwa Watanzania hawataki kumsikia, amechafuka kwa tuhuma mno, kadri anavyozidi kujisafisha ndivyo anavyozidi kuibua maswali zaidi na kuchafuka zaidi. Akubali kuwa urais kwake ni ' a thing of the past...history' basi.