Lowassa kachezeshewa "chekundu cheusi"?

HON. MP, acha ku cream. Hawa mabwana siyo marafiki tena take it from me. Inawezekana wewe hauko karibu na yeyote kati ya hao. Si uliona juzi EL alimkacha JK alivyokwenda Monduli

Teh teh.....kama vile zile kura 2 za 'HAPANA' ni za EL na EC....lol
 

Ndi hivi umeweza kujibu? Asante lakini
 
Sote tuko karibu na rais Kikwete maana ni rais wetu wote Tanzania nzima!

Mkuu isutuweke Maneno Mdomoni wengine hatukoa karibu kabisa na huyo Bwana, Kwanza aliingia Kimagumashi 2010
 
Unajua mkuu,ni kwamba Mh.Lowasa ni aina ya watu wenye kujiamini kupita kiasi na anaamini kupitia uwezo wake kifedha kila kitu kinawezekana kufanyika kwa jeuri ya pesa,japo huwezekana lakini haiwezi kuwa applied kila sehemu.

Hebu jiulize Bashe alitoa wapi uwezo wa kusema watafanya kila kinachowezekana kuhakikisha Mh.Membe hapiti?Nani alikuwa nyuma yake na ujue yeye sio mjumbe wa NEC,so mtu ambaye yupo nyuma yake ni mtu ambaye ni mwenye uwezo kifedha na hawezi Mh.Lowasa kujitenga na yule dogo.

Kazi ya kupiga kura za hapana kwa Mwenyekiti wao haikuwezekana kwa kuwa alishawatengenezea kila mazingira ya watu kujulikana endapo wanethubutu,JK alikuwa mjanja sana alihakikisha kila kitu anapata info zake na ndiyo maana kama ulikuwa makini pale ukumbini jamaa(maafisa Usalama-waliokuwa nyuma yake) walikuwa wengi na wanapokezana kutoka nje ili kumpa updates za nje,na alikuwa anamweleza hata akiwa anaongea ili kumpa hali halisi.So walichozidiwa ni trick na pia jambo jingine asilimia kubwa ya wajumbe mle ndani ni wageni so pia woga,unajua mtu mwenye Dola akitia ngumu unatokea wapi maana wengi mle ndani wameingia NEC ili wawe jirani na serikali na sio Mh.Lowasa so hawawezi kuwa watii kwa Mh.Lowasa badala yake ni kwa huyu Mwenye Dola maana wayatakayo yatapatikana kirahisi ila hizo milioni mojamoja za Lowasa zitawasaida nini...?!Hali imekuwa mbaya sana kwa Jamaa lazima arudi Ujerumani kuangalia tena afya yake...!!
 
Jay Kay mjuzi wa kujinyumbua kimwili na kifikra kama ajuavyo kucheza. He is smart on that.

Na uongozi uliotukuka, ukiitazama biography yake hakuna aliporudi nyuma, ni mbele kwa mbele tu. Anatisha.
 

Mimi sipendi kufuatilia siasa za maji taka lakini nataka nijue EL ana opportunity gani ya kupenya kwenye kinyanganyiro cha urais 2015
 
Na uongozi uliotukuka, ukiitazama biography yake hakuna aliporudi nyuma, ni mbele kwa mbele tu. Anatisha.
zomba nasikia 2015 kwenu ni Mulugo
 
Last edited by a moderator:
Binafsi naikumbuka sana hii kauli ya EL "Mimi na JK hatukutana barabarani". Na naamini mkataba wao wa kupokezana kijiti haujavunjwa na hautavunjwa kamwe
 
Yote tisa nilipenda kama kuna mtu anaweza kutusaidia kutuwekea ile hotuba ya Mzee Mangula. Maana ni fupi mno na pengine mnaojua kuzichambua msaidie kwa nini ilikuwa vile.
 
Kama kawaida Pro-Chadema JF wanamjadili rais atakayekuja ambaye hatatoka CCM wamemsahau kabisa Dr Slaa na Chadema yao.

Unajiita mtoto wa kariakoo wakati kiswahili chenyewe nehi nehi!! sasa hapo kwenye nyekundu ndio umemaanisha nini?
 
Unajiita mtoto wa kariakoo wakati kiswahili chenyewe nehi nehi!! sasa hapo kwenye nyekundu ndio umemaanisha nini?

Mkuu Mwita
Mbona unataka kuwa muhuni uzeeni somo umelielewa naona umeanza kuingiwa na hofu kubwa na 2015

Chama
Gongo la mboto DSM
 
kila siku nasikia lowassa ana hela nyingi,..hivi ni nyingi kiasi gani?
 
Mwanakijiji unafanya uchambuzi wa kizota kwa muono mfupi sana, Siasa ni mapambano ya Wanaume Lowassa hajashindwa na pia hana sababu ya kumtoa Kikwete ktk Uenyekiti, This is game, and is One man game and of the day, He must win, u know why? amejaribiwa vya kutosha na bado atajaribiwa ATAKAPO ANZA KAMPENI ZA WAZI WABAYA WAKE WOTE HAWATAKUWA NA JIPYA DHIDI YAKE TUOMBE UHAI TUSHUHUDIE THE BEST PREZ KTK MAISHA YETU
 
Nilitegemea Lowasa angejitokeza blodly kama Jacob Zuma kumpinga JK wazi wazi katika uchaguzi, na kama Lowassa angedhamiria na kujipanga mapema bila shaka angemuondoa JK katika kinyangányiro hiki.
Zuma alikuwa na support ya COSATU(chama cha Wafanyakazi)

Pia alikuwa na support ya SACP(South Africa Communist Party)

Na pia hako ka-Malema

Katika safu ya Mbeki ni yule mama Nkosazana Dlamini peke yake ndo alikuwa "ana ndimi mbili" walobaki wote walikuwa wanamsupport Zuma

Naona kama Lowassa hakujipanga vizuri.

Ila mimi siku zote nimekuwa nikisema mtafutue JK kashfa ya kumpunguzia support kwa wananchi. Kashfa itakayomfanya aone aibu hata kusimama mbele ya NEC let alone kumnadi mtu wake
 
Mimi sipendi kufuatilia siasa za maji taka lakini nataka nijue EL ana opportunity gani ya kupenya kwenye kinyanganyiro cha urais 2015
Fisadi Lowassa nafasi yake ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa CCM ni zaidi ya asilimia 70 kwa mujibu wa utafiti mdogo usio rasmi kutoka kwa mahasimu wake, kwa kuzingatia yafuatayo;

1/Idadi wa wajumbe kutoka kambi yake ndani ya vikao vya juu vya maamuzi CCM.

2/Uwezo wa pesa na namna ya kuzitumia katika harakati zake za kisiasa.

3/Ushawishi binafsi kwa wanaCCM.

4/Ubora wa timu yake katika kupambana.

5/Nguvu na kasi ya mafanikio ya mikakati yake.
 
Mengi yameshaongelewa, lakini yanayofanyika yanakanusha yanayoongelewa.
Ni muda sasa wa kujijenga kupitia political tactits badala ya kutegemea udhaifu wa wengine, ni muda wa kushinda na wale walio imara badala kutafuta udhaifa na hata kusingizia udhaifu wa watu ili kujifurahisha na kujipofusha.
Ni wakati wa kunadi sera na mikakati kwa jamii badala ya kutegemea sehemu kubwa ya biashara itokane na udhaifu.
Kuna jambo la kujifunza kupitia uchaguzi wa CCM, kwamba hata kama wao ni dhaifu basi wanafahamu namna ya kuishi na udhaifu wao.
Take it or not, kuna jambo kubwa la kujifunza hapo.
 
nionavyo mimi na ukifuatilia mwenendo mzima wa mkutano wao utagundua kuwa ccm wamefanya umafia wa demokrasia,kwa sababu kwa mgawanyiko uliopo hutegemei mtu apate kura zote,waliamua kuficha aibu,kwa mfano mangula hata kwao hawampendi iweje kwa siku mbili tu abadilishe upepo?ukweli unabaki kuwa mwaka 2005 mangula alikuwa kambi ya salim na hivyo kikwete alihakikisha hapati cheo chochote ndani ya ccm.iweje kwa siku mbili aonekane mtu sahihi?kwangu mimi mangula hawezi kumudu changamoto zilizopo ccm,kwani ataongoza ccm iliyogawika vipande viwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…