Simsemei Mwanakijiji katika hili. Lakini inamaana mtu akitoa hoja usiyokubaliana nayo au inamlenga unayempenda wewe, tayari unamhusisha na mtu mwingine ambaye haivi na unayempenda? acheni kuwa na vichwa vya panzi. Tuwe tunajadiri hoja siyo kumshambulia mtoa hoja eti anatoa hoja fulani kwakuwa hana mapenzi au ana mapenzi na mtu fulani. Maoni yangu ni kwamba; mabadiriko yanayofanyika ndani ya CCM kwa sasa; yawe ya kinafiki au ya dhati, yanamweka mamvi katika kona mbaya. Ni mchapa kazi mzuri, ni mkali dhidi ya wazembe. Hapo namkubali. Lakini kasoro kubwa aliyo nayo; anamajeraha mwili mzima ya kukosa uzalendo na uadirifu. Nikifika hapo tu, akili inagota. Mwalimu Nyerere hakuwa mjinga kumshitukia 1995. " wewe ni kijana mdogo, huwezi kueleza jinsi ulivyopata mali ulizonazo". Mamvi nyweeeee! mpaka leo. Bado Richmwendi, mhhh! hapana. Lakini acha aendeleee kugawa hela, watu wale, wanywe, wastarehe. Ili waendelee kuzila, watazidi kumdanganya, " mzee, upepo ni mzuri, utapeta tuuu!". Wakati wa vita kati ya Tanzania na Uganda; Idd Amin alikuwa hapendi kupewa taarifa za kwamba majeshi yake yanazidiwa nguvu. Washauri wake wakamjulia, walichokuwa wanakifanya ni kumwambia mambo safi, majeshi yetu yanafanya kazi nzuri na adui anarudi nyuma. Mwisho kidogo angekamatwa akiwa hai ndani ya Uganda kutokana na kutopata taarifa sahihi. Mtu wa karibu na mzee wa kufanya maamuzi magumu hata kama ni ya hovyo ameniambia; mzee hapendi negative information. Hivyo, si ajabu akajikuta anamwaga mapesa yanaliwa akijidanganya mambo yako poa kumbe yalishapinda zamaniiiiiiii! Mlioko karibu naye please mshaurini. Kama atatumia mahela kibao kisha nafasi asiipate, ukijumlisha na matatizo ya kiafya aliyo nayo mnadhani nini kitatokea. Kuweni na huruma, acheni kujali mshiko na ulabu pekee!