Unajua kitu kimoja kipo very interesting - Lowassa anavuma na ana influence kubwa sana ndani na nje ya chama bila hata ya kuwa na nafasi yoyote ya ngazi za juu ndani ya serikali na chama zaidi ya kuwa mbunge kama wengine mia mbili na kitu ndani ya CCM, mjumbe wa NEC kama wengine mia mbili ndani ya CCM, na kuwa waziri mkuu mstaafu kama wenzake wengine watano waliopita na ambao bado wapo hai, lakini bado anavuma na ana influence kupita kiasi, kuliko hata marais waliopita (nje ya nyerere); Ni muhimu sana kwa viongozi wakuu wa taifa kulitafakari hili, hasa ukweli kwamba baada ya kustaafu siasa watapotea na kuwa irrelevant wakati influence ya Lowassa katika nchi hii na maisha yao kwa ujumla itakuwa bado ipo pale pale, bila ya kujalisha nani ndani ya CCM anakuwa rais wa tano wa nchi yetu; Ni muhimu wakaelewa kwamba influence ya lowassa inachangiwa sana na watu ambao wanamuunga mkono, mara nyingine bila hata ya yeye kuwajua moja kwa moja; Hawa ndio wanaompa Lowassa 'nguvu' katika nchi yetu kwani wamemkubali;
Hoja yangu ya msingi ni kwamba CCM waamue moja, aidha wavunje chama au wakubali kutokubaliana lakini waishi pamoja humo ndani, vinginevyo kila kiongozi akiamua kufunguka, tutapigwa na mshangao wa karne; Nani angeweza kuamini kwamba hata Sumaye ana hela uswiss? Hii ni kwa mujibu wa gazeti la Dira la wiki iliyopita;
Watu wanamzungumzia Lowassa kama mtumiaji mkubwa wa fedha wakati wa kampeni; Niwaambie ukweli tu kwamba - fedha nyingi za lowassa zinatoka kwa watanzania wanaojitolea kumpigania kwa hali na mali, vijana wenye fedha zao n.k, mara nyingine bila hata ya yeye kufahamu; wapo wengi mitaani na wanajulikana; Kama Lowassa ana kosa katika siasa za fedha, basi ni kutowatafuta wote wanaompigania na kuwakemea;
Vinginevyo nazungumzia hoja yangu hii katika muktadha wa CCM, sio uwanja wa siasa Tanzania kwa ujumla wake i.e. not inclusive of upinzani; Vinginevyo hoja yangu haitaeleweka;