Lowassa kachezeshewa "chekundu cheusi"?

Lowassa kachezeshewa "chekundu cheusi"?

Mzee Mwanakijiji nakushukuru kwa changamoto ya kimawazo, ila tu niwakumbushe mambo mawili makubwa nayo ni kuwa chama kinaendeshwa na sekretariat lakini maamuzi yake yapo kwa kamati kuu na NEC na kama katika mtizamo wa watu waliowengi kuwa katika kuutaka Uraisi kimtizamo Rais Kikwete anatofautiana na Edward Lowasa basi tofauti hizi haziwezi kutuambia nani ni nani katika mbio hizo kwa kuangalia wajumbe 20 wa NEC waliochaguliwa kwenye kapu au uzuri wa secretariat iliyoundwa bali tunalazimishwa kuangalia mchakato wa wajumbe wa NEC katika mikoa na wilaya lakini pia tuangalie wajumbe wa mkutano mkuu na profile zao. Wengi nimewaangalia Kizota na niseme wazi wajumbe walikuwa zaidi ya elfu mbili lakini asilimia 75 yao ni wafu wamepeleka kura dodoma hawakwenda kupiga kura. Kupeleka kura ni kuelekezwa kampigie nani, wakati kwenda kupiga kura ni kutafakari athari na umuhimu wa kura yako katika kuchangia kutoa maamuzi ya hatima ya uongozi bora katika chama na nchi.

Hatuangalii nani kashinda leo na kufanya hivyo ni kusaliti siasa wamekusanyika Dodoma ili CCM ishinde na sii wana CCM mmoja mmoja kushinda. Na kama takwimu za uchaguzi Dodoma zinaonyesha wanachama mmoja mmoja wameshinda basi CCM inatoka kizota ikiwa imeshindwa. Nimefanya uchambuzi naona hakuna hata mtu mmoja ambaye anabeba ushindi wa Chama. Msikilize karume halafu uniambie kama leo CCM imetoka kizota ikiwa ni chama kimoja kwani ni nini haja yake kusoma kanuni za ASP.
 
With CCM so much is speculation
hujui nini ni nini
nani ni nani
Mara Mangula adui wa Kikwete
mara sasa washkaji
mara Nape adui wa Mkama mara sasa washkaji
mara huyu ataondolewa .mara kapandishwa cheo...
Aliekuwa anaweza kuielewa CCM alikuwa Sheikh Yahya peke yake.....
sisi wengine mpaka tujifunze elimu ya utabiri na majini hatuwezi

JF kuna vichwa vya kila aina...JF kuna mtaji mkubwa wa fikra.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji
Tangu juzi jumamosi kulikuwa na makundi mawili yenye mvutano mkali pale dodoma,kundi la Mh.Lowasa na wengine watiifu kwa JK walibakia uande huo,lakini JK alipoarifiwa kuwa kuna mpango wa kumpigia kura za HAPANA nae akaamua kuhakikisha kila sehemu anapata za chini ya kapeti na misimamo yao,watu wakagawanyika ndipo akapata jeuri ya kuwapiga mkwara kwenye ufunguzi na kubadilisha ratiba ya kupiga kura za Wajumbe wa Nec-CCM Taifa hapo akawa kisha wachanganya kwa kuwa aliarifiwa kuwa Mh.Lowasa anataka kuandalia watu wake chakula cha jioni.
Nadhani kama ni mtu wa kukoma Mh.Lowasa atakuwa amekoma maana watu alioamini ni wake si wake bali ni wa wenzao na kwa kweli mpango wake hauwezi kutimia na kwenye hili natumai atarejea Ujerumani kwenye matibabu...!!

Hivi kweli Lowassa ni dumb kiasi hicho cha kuandaa mkutano Dodoma kipindi hiki na watu wake?

Hujalewa wakati unaandika haya?
 
Inapokuja suala la kuongelea masuala ya CCM na hasa kumhusu lowassa huwa simuamini mwanakijiji hata kwa sekunde moja kwa sababu zifutazo,
1. kwanza mwanakijiji kwa kila dalili ya maandiko yake humu ni mfuasi wa Bernard Membe , hilo halina ubishi na hawezi muandika vibaya mfuasi wake.

2. kuhusu kutenganisha uenyekiti wa ccm na urais imebainika dhahiri kuwa walioandaa vipeperushi hivyo walifadhiliwa na membe na vyombo vya usalama vimethibitisha , zaidi walitaka aonekane ni lowassa wapate la kumsema, fuatilia tweets za serukamba utajua nini kiliendelea.


3. Nguvu ya lowassa nec ipime kwa wagombea wafuasi wake katika viti kumi vya NEC bara na Visiwani, hapo utaelewa bila kura za itifiki , kipenzi chako membe asingefurukuta.


mwisho niwaase wana JF kuwa linapokuja suala la Lowassa kupitia kwa MMKJJ litizameni mara mbili mbili kwa kuwa mara nyingi anaandika with a pre concluded assumptions . Kwa membe huwa hawezi kuficha hisia zake.
bado unawaamini usalama wa taifa tanzania?
 
True, True Quite -- Hata Nape na Lowassa ni mabest kinoma sembuse JK na EL--hao damu damu.

Mwanakijiji wewe ni mchambuzi mzuri mfano wa chekundu - cheusi unafurahisha lakini katika muktadha huu ni mfano mfu. Nani alikwambia kuwa Mh. Lowassa na Rais Kikwete ni maadui? Watu wanawekewa maneno nao wanayabeba kama majuha.
Lowassa na Rais Kikwete ni Marafiki wa siku nyingi na hakuna wa kuwatenganisha wala wao hawana sababu za kuwa maadui, wawe maadui kwa lipi???

Anayesema kuwa hawa ni maadui ama atakuwa ana matatizo kwenye ubongo na mfumo wote wa ufahamu wake au atakuwa ni wakala wa kuendelea kupumbaza watu kwa makusudi yao na hapo ndipo wanaokubali na kufikiri kuwa ni maadui ndio wanachezeshwa chekundu- cheusi!!

Hii ni JF watu tuna vichwa vizuri!!
 
Mzee Mwanakijiji umenena hasa hawa watu wanazidi kutengana zaidi na kwa mbali
Lowassa iko siku ataamini hela sio utu na huwatenga watu
Namwombea Afya njema
 
Last edited by a moderator:
pple are highly obsessed with their ccm, seems like hearts and minds ar ccm while body are opp side! tutaendelea kupelekwa mchakamchaka na hawa jamaa had lini bhana? tym wl cum.. no one wl talk abt them too much lyk nw.. woga, njaa ndo zime2fikisha hapa.
 
Naamu mambo huko dodoma yako mwishoni na taarifa zikiwa wazi kabisa kuwa,

1. Swala la kupingwa vikali kwa Membe na JK, kutoka ubande unaosadikiwa kuwa ni wa Lowasa kupitia kwa vijana wake na kundi lake linalojitapa kuwa na fedha. Lowasa na kambi yake wameshindwa kabisa kutimiza adhima yao, membe amechomoza na ushindi wa kutosha tu hata kama hayuko nafsi 3 za juu, lakini pia Jk amechomoza na ushindi wa kishindo wa kukataliwa na watu wawili tu kati ya wajumbe 2397. Mbali ya vipeperushi vyoote vile,press conferencde za bashe za kumponda wazi Membe, vitisho, kampeni chafu za mtu kwa mtu,kuhonga nakadhalika, hata bidii ya kuhonga watu hadi milioni moja moja ili kufanikisha lengo lao lakini wapi mambo yamekwenda alijojo kwa lowasa na timu yake. Hizi ni gori mbili ndani ya dakika moja langoni mwa Lowasa na Bashe mbali ya bidii zoote za kuteketeza zaidi ya milioni 200 kuhakikisha hilo jambo halitokei. Pia kunaushahidi wa mazingira unaoonyesha kuwa wakati woote wa kikao hiki dodoma mama salma na familia yake mara nyingi wameonekana wakiwa karibu sana kinafasi na kimazungumzo na membe, na hiyo ni kuashiria kwamba hiyo familia ya membe na Jk ni kitu kimoja. Polesana Lowasa

LOWASA UNAPASWA KUJUA KUWA HATA KAMA UKIWA NA WATU NDANI YA CC NA MAFEDHA YAKO, LAKINI BAADHI YAO WAPO KATIKA SAFU YA UONGOZI WA SERIKALI ILIYOPO CHINI YA JK, SO KWA MANENO YA MDOMO NI KWAMBA WATAKUPAKA MAFUTA KWA MGONGO WA CHUPA, LINAPOKUJA KWENYE SWALA LA KURA YA SIRI WANAMPENDA JK, NA MATOKEO HAYO HAPO JUU NI USHAHIDI TOSHA KUWA WANAKURA PESA ZAKO, LAKINI BADO WAMEKUTOSA VIBAYA. JIPANGE MZEE

2. Kupendekezwa kwa mzee mangula, kurudi kuwa makamu mwenyekiti wa ccm, ni pigo lingine takatifu kwa Lowasa, kwani licha ya kwamba mwanzoni mwa mwaka 2004 kuelekea 2005 jk na Lowasa walikuwahawaivi na mangula, lakini kwa sasa jk hana cha kupoteza, thats why kaamua kumrudisha now baada ya kuona rushwa ndio msingi wa nafasi za uongozi wa ccm. Hili linakuja sambamba na kuwepo kwa tetesi kuwa wasira au makamba(senior) kumrithi Mkama, hapo litakuwa ni pigo lingine goli mbili (2) kwa kambi ya Lowasa, kwani hata kwa waliofuatilia leo madongo toka kwa makamba (senior) leo wakati akimnadi jk... laivu alikuwa akimchana lowasa
baadi ya kauli hizo ni hizi
a. JK ni changuo la Mungu na leo wanachagua Kocha tu kwani kikosi cha ushindi (team) ndio hiyo cc, ambapo Lowasa hana turufu ya kutosha ya kuweza kuiteka kama ambavyo goli mbili za kwanza zilivyoingia ndani ya dakika moja rejea pointi no 1 hapo juu
b. Kauli ya kwamba mtu anayesema tupige kura za maruhani na tumpunguzie raisi majukumu, hana maana huyo, huyo mtu anakazi moja nayo imemshinda leo anasema tumpunguzie mteule wa Mungu (akimfananisha jk na Isaya) huyo mtu hatufai
kwafupi sana leo Makamba (senior) ameongea asa if yeye bado ni katibu wa chama kamaliza kila kitu, na bila shaka kauli zake zinaimpact katika ushindi wa jk leo. mapaka hapo ni goli mbili zingine
c. Makamba anatambua kuwa jk alifanya makosa kama binaadamu labda kukutosa (Lowasa) na kukuingiza mkenge ujiuzuru, lakini Makamba anasema hiyo si sababu ya yeye kuchukiwa na watu bali achukiwe kwa kushindwa kutimiza ilani ya ccm, so kilichotokea hakina impact kwa chama wala kwake. Pole Lowassa

3. Goli la tano limefungwa kutokanana, na ukweli kwamba cc hiyo hiyo ndiyo iliyoamua kuwe na mgombea mmoja katika nafasi za unyekiti na makamu mbali ya kwamba katika cc hiyo kuna wanamtandao wa Lowassa hiyo kudhihirisha kuwa bado watu wake Lowasa hawana nguvu, kuzidi group lililoko karibu na Jk na automatically karibu na membe kwani inasemekana jk na membe wanaundugu kiukoo.


4. Goli la kufutia machozi kwa kambi ya lowasa ni lile lililotokea kwa maeneo mbalimbali kama hanangi kwa kushinda watu wake, lakini ukirejea maneno ya Makamba kuwa jk ni kocha na timu tayari imeshaundwa yaani cc ambayo ndiyo hiyohiyo iliyoridhia kurudi kwa mangula, na jka kuwa mgombea pekee tayari hapo lowasa utakufa kwa pressure tu mzee wangu hata kabla ya siku zako, mbali ya kuhonga mijihela makanisani, msikitini na hata kuwahonga wajumbe


USHAURI WANGU
1. Lowasa baki na biashara zako tu, usubiri kufa siku Mungu aliyokupangia lakini kucheza na siasa za bongo za unafiki zimeshakushinda na zitakuua mapema, kama unaweza kufanya transaction mpaka za milioni 500 kwa siku, kama mwanao fred anavyoeleza unatatizo gani zaidi, baki tu kama wakina bakheresa na mohamedi interprise wanaokula kuku kwa mrija tu katika biashara zao... huku wakiwaiti 10% toka serikalini katika dilimbalimbali za serikali, kwani wakati wa kampeni ndio wafadhili wakubwa wa kampeni za chama (ccm)

2. Lowasa kama bado unania na uogozi wa nchi hii, basi jua kuwa muda si rafiki yako kabisa, na jk ameshakucheza shere mbaya, ni dakika ya 89 sasa gori 5 kwa moja, unachoweaza kufanya ni kuweka mambo yoote hadharani.. ili wananchi wachambue kipi ni pumba na mchele, Licha ya kwamba utakuwa na kazi kubwa sana ya kujisafisha kwani watakuuliza ulikuwa wapi siku zooote hzio usieleze kama jk ndiye mwizi, na hata ukakubali kujiuzuru.. Pole sana. Jk ni mnafiki na anakutoa katika mstari taratibuu.....hii njia ya kudhani kuwa jk atakuachia madaraka sahau.. jk hanaga rafiki wa kudumu.. Pole sana

Endelea kutoa sadaka msikitini na Kanisani, labda Mungu ATAKUSAMEHE MAKOSA YAKO, Lakini kuendelea kufikiria Uraisi ni ndoto za mchana, kwani jk bado ananguvu ya zaidi ya 70% kwa vyombo vyoote vya usalama, lakini pia hata kaulili zake za kuwa 2015 hawataki kisimamisha mtu ambaye atakuwa kazi sana kumnadi kwa wananchi hasa kwa kuwa atakigharamu chama na atakuwa amechafuka hilo ni kudhihirisha kuwa huyo si mwenzio.

nakala, kwa chama, ritz1, pasco, zomba, Cafu ngangari na kwa mafisadi woote....
 
Sote tuko karibu na rais Kikwete maana ni rais wetu wote Tanzania nzima!

Kukacha wapi? kwa hiyo mtu asipokuwepo mahala alipo mwingine ndio uadui? Mbona Rais kaenda na kugawa ng'ombe kwa Lowassa na Lowassa alikuwepo na akimtambulisha kwa furaha ya kutimiza aliloahidi! Je tukio hilo tu moja unaweza kuweka conclusion ya mahusiano ya watu!

Ni nani kati yao aliwahi kumsema mwenzake kwa ubaya, wapi? Zaidi ya wapambe tu wanaozusha hayo. Pili uadui wao ni wa nini sasa. Hawa watu hawagombei urais pamoja, Rais Kikwete anamaliza kipindi chake na ni marafiki wa siku nyingi. Wewe unaweza kuwa mmoja wa mawakala wa kusambaza uongo, danganyeni wasiofikiri!

Mkuu usiwe mbishi katika hili. Uadui wa watu hawa ambao "hawakukutana barabarani" upo japo hauonekani wazi na ulianza kabla ya Lowasa kujiuzuru kwa kashfa ya Richmond. Na habari za ndani zinasema kuwa ilifika kipindi Kikwete alikuwa anamkacha Lowasa pale alipokuwa anataka kukutana naye. Chanzo cha uadui huo wa chinichini ni uroho wa mapema mno wa Lowasa kuutaka urais wakati Kikwete ndo tu ameanza ungwe yake ya kwanza. Kuna taarifa kuwa ilikuwa ifanyike kampeni kabambe ili Kikwete asiende hata kwenye awamu ya pili. Ukubali usikubali watu hawa wanachekeana tu kwa nje lakini kauadui kapo.
 
Duh kazi ipo!
Kweli CCM ina wenyewe!
Kila la kheri!
 
JF kuna vichwa vya kila aina...JF kuna mtaji mkubwa wa fikra.

kwahio Ritz unakubaliana na huyo jamaa kuwa hadi tuwe na elimu ya majini kama masheikh uoni huko ni kuudhalilisha uislamu itakuwa sheikh awe na elimu ya majini?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu usiwe mbishi katika hili. Uadui wa watu hawa ambao "hawakukutana barabarani" upo japo hauonekani wazi na ulianza kabla ya Lowasa kujiuzuru kwa kashfa ya Richmond. Na habari za ndani zinasema kuwa ilifika kipindi Kikwete alikuwa anamkacha Lowasa pale alipokuwa anataka kukutana naye. Chanzo cha uadui huo wa chinichini ni uroho wa mapema mno wa Lowasa kuutaka urais wakati Kikwete ndo tu ameanza ungwe yake ya kwanza. Kuna taarifa kuwa ilikuwa ifanyike kampeni kabambe ili Kikwete asiende hata kwenye awamu ya pili. Ukubali usikubali watu hawa wanachekeana tu kwa nje lakini kauadui kapo.

View attachment 71142 kama wewe inaonekana huijui siasa endelea na UMBULULA wako wa KICHADEMA yakwetu CCM hayakuhusu
 
ni aibu sana kwa mtu mzima kama membe hawezi kusimama mwenyewe inabidi asaidiwe tena na watoto wadogo kama ridhiwani...shame on him...huyu akiwekwa ikulu si atakua hapo kulinda maslahi ya JK na familia yake? ccm amkeni...hamuwezi kua na kiongozi kama membe hamtafika popote
 
Kama kawaida Pro-Chadema JF wanamjadili rais atakayekuja ambaye hatatoka CCM wamemsahau kabisa Dr Slaa na Chadema yao.

Ritz ndg. yangu, una tatizo kubwa. Nenda hospitalini ukapimwe akili, kwa maana nadhani unaugongwa unaoitwa CHADEMA. Chadema wanaingiaje kwenye minyukano yetu? Kwani hakuna makundi kwenye chama chetu ?

Khaaaa ! Unatia kinyaa. you are not helping CCM. you are exposing how CCM people have small brains. Sorry but that is the truth
 
Siupendi sana huu mchezo; kwani unaweza kukuaminisha kabisa kuwa utashinda. Unaona kabisa kwa macho yako kuwa karata nyekundu imefunikwa upande wa kushoto na unaona mtu mwingine anaapa kabisa iko pale na anaweka hela zake pale na wewe kwa kuamini "ulichokiona" na "ushawishi" wa mtu mwingine unaamua kuweka fedha zako pale. Unaulizwa una uhakika na wewe unaapa kabisa. Kweli ikifunuliwa unakiona kipo pale na wewe na yule mwingine wote mnalipwa! Unafurahia moyoni, unachekelea kwa sababu macho yako hayajakudanganya.

Raundi nyingine inafuatia; safari hii wewe peke yako una uhakika umeona karata iile na yule mwingine yeye anaweka pale ambapo una uhakika siko. Lakini kwa vile unaona kuwa una uhakika unaongeza na dau lake kusubiria mavuno. Karata zikifunuliwa unakuta umeliwa jumla!! Unataharuki na kuapa kuwa uliona kabisa. Unaamua kuondoka kwa kujikunyata. Umeweka fedha za ada ya watoto na pango la nyumba!

Baadaye unaambiwa kuwa wote wale walikuwa timu moja- yule mchezeshaji na yule shabiki aliyekuwa anakushawishi wewe - unaamua kurudi kwa hasira ili uwafungie kazi. Unakuta wameanua jamvi na wameondoka mahali. Unafikiria utamwambia nini mama wawili ukirudi nyumbani.

Ndivyo ambavyo tunaweza kuelezea jitihada kubwa ya kutikisa NEC na kumtikisa Kikwete. Kwa miaka karibu miwili kulikuwa na tishio la kutaka kutenganisha nafasi za Uenyekiti na ile ya Urais na hata siku chache zilizopita kulikuwa na madai ya kura za vijana ambao wanataka mabadiliko. Mwisho wa siku ni watu 2 tu walithubutu kumpigia kura za "Hapana" Mwenyekiti. Watu 2!

Kwa sababu hawakutegemea CCM kuwapiku kwa kubadilisha mtindo wa kupiga kura ambapo ingekuwa rahisi sana kuweza kujua kura za hapana zimetoka wapi. Hata uhesabuji kura - vyanzo vya ndani vinadokeza na hili litafumuka baadaye - ulifanywa ili kuhakikisha kujua ni kundi gani lilimpigia Rais kura za hapana.

Ni wazi mwisho wa kundi la Lowassa utaanzia leo; hasa tukisubiri uundwaji wa sekretariati mpya ya CCM ambayo itakipeleka chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Mtu kaliwa. Lakini atarudi tena na fedha nyingine kujaribu kucheza mchezo ambao uko dhidi yake?


by way of deception
 
Tuwaachie matajiri na ccm yao si wakulima na wafanyakazi tuhamie CHADEMA chama cha ukombozi zidi ya mkoloni mweusi tajiri aliye jimilikisha ccm.
 
Back
Top Bottom