Lowassa kachezeshewa "chekundu cheusi"?

Lowassa kachezeshewa "chekundu cheusi"?

This time hatarudi!, he won't play anymore, "the games people play"!.
"The winner takes it all, the looser standing small!".
P.
Bora wewe umeelewa sasa maana tulisema mashabiki wa EL hawaitakii mema CCM na jibu ni mkutano Mkuu jua wengi wapo upinzani walijua CCM 2015 watatupa Garasa wao watoe King
Salama ya EL kwa karata ya mwisho ni CC leo mchana km hakuingia ndio byebye na kundi lake kwani nafasi finyu ktk 18 maana kuna wenyeviti wa Jumuia zote Maspika wawili
Nape na Mangula.hivyo bora aendeleze biashara zake alphatel, wasomali wa Intergrated, Tanzanite, vyombo vya habari nk
Urais atulie Mkiti wake kamwambia wasikichafue Chama wangoje May 2015
 
mkuu nakupinga sana, ila yawezekana uko sahihi, lakini kama utakuwa ulifuatilia hotuba ya jk siku ya jumamosi vizuri utajifunza alimpiga sana madongo uyo el unayedai kuwa ni rafiki yake wa siku nyingi, alitaja wagombea uraisi kuwa ndo wankigawa chama chao, alikemea rushwa ilotolewa hasa katika uchaguzi wa umoja wa wanawake na hata kushauriwa ayafute matokeo na iko bayana aloshinda kuwa mwenyekiti wa jumuiya iyo ni mtu wa kaka el na aliwezeshwa na el.
Makamba kwa niaba ya kikwete alifunguka jana akimponda mtu mmoja asokuwa na kazi anajitaidi kumuangusha jk ktk uenyekiti natumai alokuwa akitajwa kutokuwa na kazi ni el.
Jamani kwa ayo machache sikubalian nawewe hawa jamaa hawako vizuri kiurafiki, na jk anaogopa el akiukwaa upresidaa aweza ata kumgeuka uko mbeleni, km moja ya kulipa kisasi
Mkuu wewe ni mfuatiliaji mzuri lakini unashindwa kabisa kuona kabisa nini kinachoendelea nyuma ya pazia!!

kama unadhani Lowassa na Kikwete ni maadui embu jiulize maswali haya:

1/Wiki moja kabla ya huu mkutano wa CCM, Jakaya Kikwete alikuwa Monduli na kutamka kuwa ''Lowassa ni JEMBE'' Why?

2/Wengi walioshinda ndani ya chaguzi za CCM ni watu wa Lowassa tena kwa rushwa kubwa, kwanini Kikwete ameshindwa kutengua matokeo?

3/Kwanini Kikwete ameshindwa kusimamia mpango wa kuwavua magamba Lowassa na wenzake?

4/Lowassa amewahi kutamka mara kadhaa kuwa Yeye na Kikwete hawakukutana barabarani!! How? Why Kikwete hajawahi kukanusha hilo?
 
Inapokuja suala la kuongelea masuala ya CCM na hasa kumhusu lowassa huwa simuamini mwanakijiji hata kwa sekunde moja kwa sababu zifutazo,
1. kwanza mwanakijiji kwa kila dalili ya maandiko yake humu ni mfuasi wa Bernard Membe , hilo halina ubishi na hawezi muandika vibaya mfuasi wake.

2. kuhusu kutenganisha uenyekiti wa ccm na urais imebainika dhahiri kuwa walioandaa vipeperushi hivyo walifadhiliwa na membe na vyombo vya usalama vimethibitisha , zaidi walitaka aonekane ni lowassa wapate la kumsema, fuatilia tweets za serukamba utajua nini kiliendelea.


3. Nguvu ya lowassa nec ipime kwa wagombea wafuasi wake katika viti kumi vya NEC bara na Visiwani, hapo utaelewa bila kura za itifiki , kipenzi chako membe asingefurukuta.


mwisho niwaase wana JF kuwa linapokuja suala la Lowassa kupitia kwa MMKJJ litizameni mara mbili mbili kwa kuwa mara nyingi anaandika with a pre concluded assumptions . Kwa membe huwa hawezi kuficha hisia zake.
Wewe umeyapata wapi mamlaka ya kutuburuza kuamini mitazamo yako juu ya Mzee Mwanakijiji?kwanini ustuachie uhuru wetu wa kuchambua hoja ya mmkj kwa mitizamo yetu? Mijitu mingine kwa kujifanye yenyewe inaakili !!!!
 
Mliongea meeengi,mnaongea meeengi lakini unasahau kuongelea nguvu za mwenyekiti wa ccm,toka enzi za nyerere,mwenyekiti wa ccm ana nguvu nyingi sana kwenye vikao vya maamuzi,kuna wakati huko nyuma kulikua na hoja za kumpunguzia nguvu hizo,kina lowassa wangeanzia hapo miaka miwili iliyopita leo kazi ingekua rahisi sana bali hata vipeperushi vya bashe
 
Kupiga kura kwa staili ya mikoa ndo sababu kubwa ya waliotaka kumpinga JK kuingia mitini. Na siamini kuwa ktk hali ya kawaida kabisa kupata 100% ni kukubalika kwa kiwango hicho. hizi ni kura tuu lakini kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake baada ya kura hizo.

Angalia wapiga debe wote maelezo yao hii ni staili ya CCM toka huko nyuma si sheria bali ni mazoea yao. Amini usiamini hakuna uongo usiokuwa na ukweli uongo chanzo chake ni ukweli furani ili udanganywe ni lazima upewe ukweli ambao utauamini kisha ukaja gundua kuwa ulikua anadanganywa.

Ebu tusubiri kama 99.9% ni kumkubali Mwenyekiti wao basi hakutakua tena na mitafaruku ndani ya CCM, vinginevyo, basi kura hizi ni unafiki wa funika kombe.

mitafaruku lazima iwepo kwenye demokrasia kwa kuwa katika hali ya kawaida haiwezekani watu wooote mkawaza na kufikiri sawasawa,hizi sio enzi ya zidumu fikra za mwenyekiti kaka,hiyo aliweza nyerere tu wakati ule sio sasa,muhimu mwisho wa siku ni kura,kama kapata za kutosha huyo ndio mwenyekiti hata kama watampinga lazima hawawezi kumuondoa tena na vikao vyote vya kumpata rais ajaye kupitia ccm ataviongoza yeye,hicho ndio watu wanaomuona kikwazo kwa ndoto zao kilichokua kinawafanya wahangaike na vipeperushi na mapesa
 
Mkuu MJJ,
Ingawa wengi wangependa huyu nyoka aondolewe kwenye siasa za TZ, lakini ni vema tukawa waangalifu sana kwenye kumfikiria kuwa anakufa hivi karibuni. EL inaelekea anazaidi ya roho saba. Marehemu Mwalimu JK alimkung'uta na labda kumzika tena waziwazi tofauti na hii ya mafumbo anayofanya Kikwete, lakini bado EL akaibuka na kuwa PM na akajikusanyia nguvu nyingi zaidi mikononi mwake. Mchezo wa karata tatu unachezwa, lakini tusubiri matokeo ili tusije-tukashangaa ikawa anayechezewa ni Kikwete badala ya EL. Let's wait and see.
Hamna kitu,kikwete kamzidi tu maarifa huyu mmasai feki,hawezi kuwa rais bil mbeleko ya mwenyekiti huo ndio ukweli,jk alibebwa pia na mbeleko hiyo,ni mkapa tu ndio aliingia kwa mbeleko ya mzee wa butiama
 
With CCM so much is speculation
hujui nini ni nini
nani ni nani
Mara Mangula adui wa Kikwete
mara sasa washkaji
mara Nape adui wa Mkama mara sasa washkaji
mara huyu ataondolewa .mara kapandishwa cheo...
Aliekuwa anaweza kuielewa CCM alikuwa Sheikh Yahya peke yake.....
sisi wengine mpaka tujifunze elimu ya utabiri na majini hatuwezi

teh teh teh...The Boss bora umesema.
 
Kama mngejua tangu awali kwamba huu mchezo wote centers around Richmond Scandal. Isingekuwa hiyo hakika JK angembeba Lowassa kulipa fadhila.

JK hana ubavu wa kumbeba Lowassa waziwazi na huku anajua Membe au Dr. Mwakyembe watakuja kuirudisha scandal ya Richmond

Mbaya zaidi uchunguzi wa Richmond scandal ulifadhiliwa na taasisi inaitwa MCA (millenium challenge account) ambayo ipo affiliated to US

From day one nilisema Membe ndiye chaguo la Wamarekani thus automatically hand picked successor to JK
 
Zuma alikuwa na support ya COSATU(chama cha Wafanyakazi)

Pia alikuwa na support ya SACP(South Africa Communist Party)

Na pia hako ka-Malema

Katika safu ya Mbeki ni yule mama Nkosazana Dlamini peke yake ndo alikuwa "ana ndimi mbili" walobaki wote walikuwa wanamsupport Zuma

Naona kama Lowassa hakujipanga vizuri.

Ila mimi siku zote nimekuwa nikisema mtafutue JK kashfa ya kumpunguzia support kwa wananchi. Kashfa itakayomfanya aone aibu hata kusimama mbele ya NEC let alone kumnadi mtu wake

Red bold mkuu!! Kulikuwa na sababu gani yeye kukubali kubeba lawama za Richmond? Si angemwaga vyote tu?

Ila EL huwa namfananisha na ManU, ni mzee wa come back!!!! Nawahi kubeba box, maana na kikazi cha usiku bana!!!
 
Red bold mkuu!! Kulikuwa na sababu gani yeye kukubali kubeba lawama za Richmond? Si angemwaga vyote tu?

Ila EL huwa namfananisha na ManU, ni mzee wa come back!!!! Nawahi kubeba box, maana na kikazi cha usiku bana!!!

Culprit wa Richmond ni Lowassa. JK hawezi kumuanika. Nilichokuwa nasema pale ni kwamba, Lowassa na uchafu wake kwakuwa yuko karibu na JK anajua siri nyingi za JK angeweza kuwatumia CHADEMA waziweke hadharani kumkata makali JK
 
hawa jamaa ni marafiki kihistoria lakini currently ni maadui kwani wamesalitiana kwa mengi sana kwanza richmond ishu ya gamba lowasa alishawahi kusema hivi mwenyekiti nikweli hufahaamu lolote kuhusiana na richmond pili mwanae lowasa yaani fred lowasa anahusishwa na kusambaza vipeperushi vyakutokuwa na imani na mwenyekiti wa ccn
 
Mwanakijiji wewe ni mchambuzi mzuri mfano wa chekundu - cheusi unafurahisha lakini katika muktadha huu ni mfano mfu. Nani alikwambia kuwa Mh. Lowassa na Rais Kikwete ni maadui? Watu wanawekewa maneno nao wanayabeba kama majuha.
Lowassa na Rais Kikwete ni Marafiki wa siku nyingi na hakuna wa kuwatenganisha wala wao hawana sababu za kuwa maadui, wawe maadui kwa lipi???

Anayesema kuwa hawa ni maadui ama atakuwa ana matatizo kwenye ubongo na mfumo wote wa ufahamu wake au atakuwa ni wakala wa kuendelea kupumbaza watu kwa makusudi yao na hapo ndipo wanaokubali na kufikiri kuwa ni maadui ndio wanachezeshwa chekundu- cheusi!!

Hii ni JF watu tuna vichwa vizuri!!

Bwana Hon. MP, Mbona unaandika kwa jazba? au dio ule msemo, "jiwe likimpata mmbwa lazima abweke"?
 
With CCM so much is speculation
hujui nini ni nini
nani ni nani
Mara Mangula adui wa Kikwete
mara sasa washkaji
mara Nape adui wa Mkama mara sasa washkaji
mara huyu ataondolewa .mara kapandishwa cheo...
Aliekuwa anaweza kuielewa CCM alikuwa Sheikh Yahya peke yake.....
sisi wengine mpaka tujifunze elimu ya utabiri na majini hatuwezi

Kweli kaka ni mauza uza kila kukicha tusishangae siku ya siku yeye Jk akampitisha tena kwe mbwembwe EL
 
lowasa alishawahi kusema hivi mwenyekiti nikweli hufahaamu lolote kuhusiana na richmond
In fact alikuwa anamaanisha kwamba je yale maamuzi yote ya Richmond yalikuwa ni yake binafsi bila kupata consent ya JK
?

Nionavyo mimi kauli hiyo hamsafishi Lowassa. Tume ya Dr. Mwakyembe ilimtaka Lowassa awajibishwe unaliongeleaje hilo?

Halafu inasemekana kuwa Frederick Lowassa ni mmoja wa wamiliki wa Richmond
 
Mkuu Mwita
Mbona unataka kuwa muhuni uzeeni somo umelielewa naona umeanza kuingiwa na hofu kubwa na 2015

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama,
Naona huyu mshashi anaogopa sana kariakoo.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mwanakijiji, Jaribuni kuondoa hisia za JK na EL maana hao siyo CCM. Itazameni TANZANIA tuitakayo utaona kuwa CCM wanaanza kubadili upepo wa siasa za nchi kuelekea 2014 & 2015. Kama chama kikongwe na kinachokubali kujisahihisha kimeonyesha njia. Tuvitume vyama vyote vya siasa vijipange barabara kuelekea katika mafanikio dhabiti kwa nchi yetu. Mtu mmoja mmoja ama ka-kikundi fulani wasigeuke ajenda.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom