Lowassa could've done better...

Lowassa could've done better...

JK inawezekana alikuwa ana wivu kuona besti yake naye akiingia kwenye listi ya mapresdaa. Ili kwenye group lao EL asimfunike. Maana kiukweli walikuwa marafiki. Lakini urafiki wa JK ulikuwa wa kinafiki zaidi.

JK akaleta siasa za "kuvua gamba", akiwa target walio kuwa wakipigiwa kelele za ufisadi. JK alijuwa EL si fisadi lakini alinyamaza na kuendeleza politics za kiswalihina. Ufisadi wote wa kuuza nchi EL hajatokea.

JK yuko responsible kwasababu hata mimi nilimpigia kura Maghufuli badala ya Lowassa kwa kuamini ni fisadi ambaye JK anaogopa kumtimua waziwazi ili chama kisimegeke. But I was wrong.

JK pia alitaka wananchi wamkumbuke uongozi wake ndo maana akaona JPM anafaa zaidi kwasababu anamfahamu vyema(alishawahi kupindua maamuzi yake mengi tu JPM alipokuwa waziri na JK rais), JK alijuwa kuna namna mambo yatakuwa ndivyo sivyo na wananchi kulalamika zaidi, hence kumkumbuka.

However nimekaa nikafikiria, sababu kubwa ya kumpigia kura JPM badala ya Lowassa ni ufisadi. Nikasubiri ccm wamshitaki EL, wapi. Subiri wataje kashfa ambaye kiukweli amehusika yeye, hakuna.

Yani ina maana kashfa ya kuuza nyumba za serikali kwa ndugu zake, inaonyesha wazi uncle Magu ni fisadi na wala siyo EL.

Kwahiyo hapa kusema JPM ni msafi kuliko EL ni upotoshaji mkubwa kabisa.

Hivyo basi hapo ndo tofauti kubwa ya kwanza kabisa kati ya hao viongozi wawili. Pia kingine ni busara. Mzee EL ana busara sana, na pia huchaguwa maneno ya kuzungumza nk.

Watu hao lakini pia wana similarities. Yani kuna mambo wanafanana. Na hilo ni ufuatiliaji, utekelezaji na uwajibikaji.

Hizo ndo nguzo kuu za sifa za Lowassa. Sasa wale ambao hatukuwa na uhakika kuhusu EL, tukaona kuwa Maghufuli pia anaweza kufanya tu kama yeye.

Lakini tofauti ni ukosefu wa busara kwenye maamuzi hayo. Busara ikikosekana kwenye jambo lolote la msingi, basi matokeo yake ni sawa "kujipiga risasi ya mguuni" ukiwa kwenye safari inayoitegemea miguu hiyo.

EL pia ni msikilizaji. Hiyo sifa rais wetu wa sasa hana. Nina imani kuna anaowasikiliza wachache, ambao hao kwake hawana makosa.

Pamoja na sifa ya ujasiri na uchukuaji wa maamuzi magumu alizonazo EL, bado ni mtu mwenye UPENDO na HURUMA.

Rais anaonekana ana ujasiri. Wengi wanapiga wanasema ni uoga. Mimi ninaamini ana ujasiri, lakini hana upendo wala huruma hata chembe.

Binafsi ninaamini rais lazima awe na empathy, yani uwezo wa kujiweka kwenye nafasi ya mtu mwingine na kuona anayopitia. Mtu wa namna hawezi kukosa huruma na upendo, ingredients ambazo ni muhimu sana kwenye jamii ya kitanzania. Aliposhindwa kujiweka kwenye nafasi ya wafiwa, aliamuru rambi rambi zisikabidhiwe kwa wafiwa/waathirika. Hapo ndipo utaona umuhimu wa empathy kwa kiongozi mkuu wa nchi.

Pia EL siyo mtu wa visasi wala vinyongo. Kwa kuwa nilikuwa nimeshamchukia sana kwasababu za uongo kuwa ni fisadi namba moja nchini, nilishindwa kuamini kama hana hizo characteristics.

Nikawa nadhani anajifanyisha tu pale ambapo akitukanwa wala hajibu. Na wanaomuita fisadi hawamyimi usingizi. Yani wala hakutumia nguvu kubwa kupingana na hao wanaomuita fisadi na matusi mengine.

Binafsi ninaamini kuwa JPM amepiga marufuku siasa kwasababu ya Lowassa. Kiukweli, wengi wangeona makosa makubwa tuliyofanya.

Hapo mwanzoni nilikubaliana na JPM kuwa serikali inatakiwa ipewe muda wa kufanya kazi na kutekeleza ahadi zake badala ya kuendeleza siasa. However sasa nimegunduwa kuwa sababu kubwa ni yeye binafsi. Wasiwasi kuwa wananchi watagunduwa mapema makosa waliyoyafanya.

Kama Mungu akimpa uzima, na afya ikawa inaruhusu, nina imani kuwa Lowassa bado ana nafasi ya kuongoza Taifa letu. Pengine akayafanya yale mazuri yaliyoko kwenye uongozi huu wa sasa, na kuachana na negativity zote za utawala huu.

La mwisho kabisa, ni uzalendo wa kweli.
kila mtu ana uzuri na ubaya wake ilakwa hili la ufisadi lowasa asingeweza kabisa na hata kwa hili suala la madini mzee asingeweza kwa mambo ya demokrasia huru nalo bado nina shaka ila labda angekuwa nafuu
 
Ukweli ni KUWA LOWASA ni fisadi kama walivyo wana CCM wengine..and so magu...Common denominator kwao wote ni Ufisadi.so usitegemee wakachukuliana hatua.

Mimi nawalaumu CHADEMA kujichanganyana sana na hatimaye kusababisha wananchi waende katika uchaguzi kushindanisha wana CCM wawili.

Kosa ambalo kila siku chadema wanafanya ni kutokuwa na Malengo ya Muda mrefu ,ya kati na muda mfupi.Succession Plan ikiwa ni jambo la msingi sana.

chadema walipaswa kumweka mtu aliyeshiba filosofia na itikadi ya chama chake.mtu ambaye amejitambulisha na kubeba taswira ya Chadema.Kimsingi ilikuwa ni kosa sana kumsimamisha lowasa kama mgombea wa urais wa Chadema.Ila wangempokea na kusuport mtu mwingine Let say Slaa.Leo tungeonea mambo mengine hapa.

Na kosa lingine wanalofanya ni kutojipanga kwa chaguzi zijazo.Hata huyo lowasa amekuwa na faida kwao kwa short run.in long run anawagharimu.Calliber yake haiwapi uhai wananchi na kuona future ya taifa ndni yake.

Chadema wasitegemee kupata mteremko.waache kulalamika.haiwasaidiii.wakomae

cc Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji
 
Hii nchi imefika hapa tulipo si kwasababu ya viongozi tu bali wananchi wengi ambao ni mazuzu kama mleta mada.
Mleta unawakilisha aina ya mazuzu wasiojua nchi ilifika wapi na ilihitaji kiongozi wa aina gani kutuchongea njia tuliyopotea.

Mtu anazunguka misikitini, makanisani vyama mbalimbali vya kijamii kote anamwaga hela,,, akiulizwa anasema eti pesa za marafiki zangu,,,hujiulizi hizo ela angezirudisha vipi!???

Pia yote kwa yote, walioasisi vita ya ufisadi na kupelekea Lowassa kujiuzulu ni CHADEMA. Labda mleta mada ungeuliza je Chadema waliudanganya na kuulaghai umma!????

Sent from my HTC Desire EYE using JamiiForums mobile app
Unaweza ukaongea sna mkuu hawata kuelewa sababu watz wengi ni static not dynamic.
sipendi.kuongea mengi nna sbabu zangu .....mpe mda.JPM
 
Dogo mradi wa maji ziwa Victoria Lowasa kaukuta uko mezani kwa utekelezaji.

City water Lowasa alikuwa akivuta 200m kwa mwezi kama commission alipoingia mwandozya wizarani akmjulisha mkapa akampiga marufuku Lowasa kupokea commission ndo chuki yake Lowasa ikaanza kwa city water alipoupata Waziri mkuu ikaanza nao.akawatimua.

forget about this highly corrupt man Lowasa.
Mkuuu JF kuna depended mind ......too static and rigidilly...idea.Ukisema hayo utapngwa tu.
 
Jaribu kuwa makini unapojibu hoja ya mtu. Jina tu linakushinda. Hayo mengine inakuwaje?
You asked a question (Is it plagiarized work? and I answered your question.

Hoja gani ya mtu unayoongelea? Huko kulikosea spelling jina lako la kizungu linahusianaje na swali lako? Au hata maana ya plagiarism huijui, unanakiri kama kasuku? Jibu nililotoa is 100% correct for your plagiarized question, Mr Invincible.
 
You asked a question (Is it plagiarized work?) and I answered your question.

Hoja gani ya mtu unayoongelea? Huko kulikosea spelling jina lako la kizungu linahusianaje na swali lako? Au hata maana ya plagiarism huijui, unanakiri kama kasuku? Jibu nililotoa is 100% correct for your plagiarized question, Mr Invincible.

Unatoa jibu halafu unajisahihisha mwenyewe.
 
Ukweli ni KUWA LOWASA ni fisadi kama walivyo wana CCM wengine..and so magu...Common denominator kwao wote ni Ufisadi.so usitegemee wakachukuliana hatua.

Mimi nawalaumu CHADEMA kujichanganyana sana na hatimaye kusababisha wananchi waende katika uchaguzi kushindanisha wana CCM wawili.

Kosa ambalo kila siku chadema wanafanya ni kutokuwa na Malengo ya Muda mrefu ,ya kati na muda mfupi.Succession Plan ikiwa ni jambo la msingi sana.

chadema walipaswa kumweka mtu aliyeshiba filosofia na itikadi ya chama chake.mtu ambaye amejitambulisha na kubeba taswira ya Chadema.Kimsingi ilikuwa ni kosa sana kumsimamisha lowasa kama mgombea wa urais wa Chadema.Ila wangempokea na kusuport mtu mwingine Let say Slaa.Leo tungeonea mambo mengine hapa.

Na kosa lingine wanalofanya ni kutojipanga kwa chaguzi zijazo.Hata huyo lowasa amekuwa na faida kwao kwa short run.in long run anawagharimu.Calliber yake haiwapi uhai wananchi na kuona future ya taifa ndni yake.

Chadema wasitegemee kupata mteremko.waache kulalamika.haiwasaidiii.wakomae

cc Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji
Mkuu nadhani kuna namna inatakiwa tuangalie issue hii kwa jicho la tatu.

Kwanza utambuwe kuwa hizo kashfa zilitoka ndani ya serikali kwa wana ccm wenyewe.

Kwa mantiki hiyo, kuna mawili

1) waliowapa siri chadema wana malengo yao binafsi na ya kisiasa. Nina imani kwamba vita ndani ya ccm ndo inapelekea hizo siri kuvuja. Na wanaozivujisha, pengine wakiwa na malengo ya binafsi ya kisiasa nk.

2) Kwamba walivujisha siri kwasababu ya uzalendo. Hii pointi nina mashaka nayo sana. Kwasababu kama bado wamo humo humo, hawataki kutoka, zaidi zaidi wanazidi kuji position kwa madaraka zaidi, ulaji nk, basi nasita kusema ni uzalendo. Naona kama ni malengo binafsi zaidi na ya kisiasa.

Hilo nimegunduwa kwasababu hadi sasa yule aliyekuwa akipigiwa makelele kama fisadi mkuu, hayuko kwenye kashfa kuu za kifisadi. Hapo unaweza kuona pengine wapiga kelele wale walikuwa wanataka wawachafue baadhi ya wanasiasa wanaowaona ni kizingiti kwa malengo yao binafsi ya kifisadi pamoja na yale ya kisiasa.

Inawezekana kabisa hao watu waliwaingiza chaka chadema. Hilo sikatai.
 
Ndo maana sa hivi tuache mambo ya siasa tuangalie Taifa letu humo kwenye siasa hao watu wanajua wao wanachokitaka hivi vyama vilificha watu wengi ambao wapo kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na si taifa wamekua wanatumia nguvu ya vyama na support ya wananchi kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na ndio maana tulihitaji rais kwanza asie na mambo ya siasa na uhuni wa humo ili kufikia tunapopataka huyo mzee mimi naona tungepigwa tu changa la macho baadae tena tuje na hadithi nyingine
 
Lowassa angekuwa mbinafsi, angebaki ccm kama hao wengine? Unadhani hajui madhara ya kuwa upinzani? Siasa ni kazi yake lakini kazuiwa.

Mhalifu anapelekwa mahakamani au anazuiwa siasa?
 
1) waliowapa siri chadema wana malengo yao binafsi na ya kisiasa. Nina imani kwamba vita ndani ya ccm ndo inapelekea hizo siri kuvuja. Na wanaozivujisha, pengine wakiwa na malengo ya binafsi ya kisiasa nk.
Mkuu.huhitaji kupewa siri kujua kuwa lowasa alihudumu kama waziri kwa miaka mingi sana.akiwa kwenye baraza ameshiriki kuidhinisha mambo mengi ambayo yameitia nchi hasara.Vile vile magufuli.

Tena lowasa yuko kwenye Cabinet toka miaka ya tisini mwanzoni .magufuli mwaka 1995.wote kwa pamoja wameshiriki kuleta madudu mengu tu.kwa hio huhitaji kupewa siri yoyote
Hilo nimegunduwa kwasababu hadi sasa yule aliyekuwa akipigiwa makelele kama fisadi mkuu, hayuko kwenye kashfa kuu za kifisadi. Hapo unaweza kuona pengine wapiga kelele wale walikuwa wanataka wawachafue baadhi ya wanasiasa wanaowaona ni kizingiti kwa malengo yao binafsi ya kifisadi pamoja na yale ya kisiasa.
Lowasa ni fisadi mkuu.bado tu hutaki kuamini.Pona yake ni kwa sababu yeye ni CCM kama CCM wenzake.Ufisadi kwao ni jadi.kamwe hawawezi kuchukuliana hatua
 
JPM japo ana dosari ila amejitahidi kupita kiasi kwa yale mazuri
 
Mkuu.huhitaji kupewa siri kujua kuwa lowasa alihudumu kama waziri kwa miaka mingi sana.akiwa kwenye baraza ameshiriki kuidhinisha mambo mengi ambayo yameitia nchi hasara.Vile vile magufuli.

Tena lowasa yuko kwenye Cabinet toka miaka ya tisini mwanzoni .magufuli mwaka 1995.wote kwa pamoja wameshiriki kuleta madudu mengu tu.kwa hio huhitaji kupewa siri yoyote

Lowasa ni fisadi mkuu.bado tu hutaki kuamini.Pona yake ni kwa sababu yeye ni CCM kama CCM wenzake.Ufisadi kwao ni jadi.kamwe hawawezi kuchukuliana hatua
Mkuu, since we have to work with what we have, lazima ujuwe kuchambuwa kati ya mchele na chuya.

Hadi usawa huu, ninaamini chadema waliingizwa mkenge na ccm kwakuwapatia "taarifa za ufisadi" zenye malengo yao binafsi. Tatizo ni kwamba chadema hawajakubali ku admit hiyo kitu.

Unaposema pona yake ni kwasababu yeye ni ccm hata sikuelewi.

Nasema we gotta work with what we have kwasababu karibia wote wanaotaka urais washakuwa kwenye cabinets.

Na kwa jinsi ambavyo wanajali kuhusu "collective responsibility ", wote wanakuwa responsible. Na anayekwenda kinyume ni msaliti wa serikali na atafukuzwa. Haijalishi kwamba issue yenyewe ni mbaya kwa maslahi ya Taifa. Na kwahivyo ccm hapo wako responsible.

Mimi nimepima na kuangalia siasa ambazo zimetuletea rais aliyeko madarakani, nikatizama nyuma. Nikaona where and what went wrong, ndo maana hata sasa wananchi wengi wako confused kuhusu chadema, na wao hawajachukuwa hatua yoyote kutoa maelezo na kuwataka radhi wananchi. Kwa namna nyingine nashindwa kuwalaumu moja kwa moja kwasababu wamezuiwa kufanya siasa.
 
kila mtu ana uzuri na ubaya wake ilakwa hili la ufisadi lowasa asingeweza kabisa na hata kwa hili suala la madini mzee asingeweza kwa mambo ya demokrasia huru nalo bado nina shaka ila labda angekuwa nafuu
Kwani la ufisadi nani ameweza hadi usawa huu?

Na hata hiyo ya madini si ni hao hao walioko madarakani walisaini hiyo mikataba?

Afadhali Lowassa yuko kwenye timu ya Tundu Lissu ambaye alipingana na hiyo mikataba toka enzi na enzi. Afadhali ni nani kati ya hao wawili hao wawili kama si aliyeko kwenye timu inayopinga mikataba mibovu kusainiwa? Upande ambao hautaki tupate hasara kwa maamuzi mabovu?

Huyu wa sasa bado anakumbatia chama kilekile chenye watu walewale.

Usidanganywe na siasa za kuitana wasaliti. Kuwa makini usijekuta unaicheza ngoma yao kama walivyofanya chadema.
 
Magufuli ni rais bora kabisa kuwai kutokea. Acheni akili fupi za kiafrika, huyo lowassa kwa mfano angefanya nini ambacho magu hafanyi zaidi ya wizi yeye na genge lake la kina rostam karamagi

Hilo genge limefikishwa Mahakama ya mafisadi au bado linarandaranda mtaani?
 
Mimi ni muhanga wa ajira lakini bado nampenda
Me ni muhanga wa bomoa bomoa lakn bado nampenda. Najua anafanya haya kwa manufaa ya wengi
Naona kuna huruma huruma kama vile Raisi anaonewa. Ukweli ni kwamba ni Magufuli mwenyewe kajitakia haya matatizo pasipo ulazma.

Kuzuia wapinzania kufanya mikutano, kuzuia bunge kuenda live, watu kufa kufa kiajabu, wanasiasa kuwekwa ndani bila sababu ya maana, wanasiasa kupigwa risasi, visasi mpaka kwa mawakili kuvunjiwa maofisi an Manji anavyofanyiwa.., kubomolea watu nyumba kinyume na sheria... .

Kusema unapenda nchi halafu ukiletewa wala rushwa husemi lolote mpaka wawe maaduni wako.

Kusema hupendi vyeti feki wakati huohuo unaajiri watu wenye vyeti feki.

Kusema hapa kazi tu wakati unafanya mikutano ya CCM ikulu....

Wivu wa kikanda kuzuia Moshi kuwa jiji bila sababu ya kimsingi...

Hizi ndiyo sababu watu wanamatatizo na Magufuli. Hakuna Mtanzania asiyependa maendeleo lakini watu hawatampa raisi maisha yao kwa kisingizio cha uzalendo wakati hafuati hata anayosema mwenyewe
Source: Kamundu
 
Mbegu kabla ya kuota inabidi kuoza kwanza, halafu ndio inaanza kuota, ndio kanuni ya Kimungu, Magufuli ni Rais Mzuri sana, sio mnafiki kama hao wengine, Ni sifa ya shujaa, Magufuli anachosema ndio anachokifanya, hapindishi, lakini pia ameweza kufanya vizuri katika nyanja zote muhimu katika muda mfupi,Mafanikio yaliyopatikana katika miaka miwili ya Urais wake ni makubwa sana, muelekeo wa nchi miaka kumi ijayo unaleta matumaini, isipokuwa HAPA KAZI inataka ufanye kazi ili upate mkate, na uko mbele hakutakuwa na kukaa kwa shemeji tena.
Labda tuseme "Maghufuli ni mtu mzuri", lakini sisi watanzania ndo tumefanya makosa kumpa kazi asiyoiweza?

Au makosa ni yake kujaribisha kuomba kazi iliyomzidi uwezo?
 
Hata JK hakutaka huyu jamaa apite aisee kilichofanyika ni kua JK alikua na team ambayo jamaa yake Mem...alikua, pia Migiro, Makamba jamaa wa EL walikua wengi kumkomoa wakampitisha jamaa,na kibaya jamaa mwenyewe anajua hastahili kitu chochote kile aiseee ndo mana uongozi wake full kujistukia...
I second this...

Uncle Magu anaweza akawa ni mtu mzuri tu.

Lakini pia nakubali wenye makosa ni partially sisi wananchi na partially yeye Magu mwenyewe.

Sisi tuliompigia kura kwa kumpa majukumu ambayo hayawezi, tulifanya kosa kubwa....

On the other side, na yeye yuko responsible kwa makosa kwa kujaribisha kazi ambayo haiwezi na haitakiwi kujaribishwa, Bali inatakiwa uwe na maono kwa Taifa.

Hayo aliyaweka wazi yeye mwenyewe. Kwamba alijaribu tu, hakuwa anafikiri kuwa atashinda, na siyo kazi aliyokuwa ana uhakika anaweza kuifanya.

Haitakiwi uwe genius kujuwa kuwa sumu haionjwi.
 
Unadhani nick name ya "mtu mwenye maamuzi magumu" ilianzia wapi?

Na uwajibikaji haukuwepo alipojiuzulu?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Mpaka leo sijaelewa kwanini kama ni fisadi kweli ile mahakama ya Yohana haijamshughulikia?? As a matter of fact hakuna ktk wote waliowahi kutuhumiwa tuliosikia mf Chenge wakipelekwa mahakamani sasa tutaamini vipi kuwa ni kweli alcohol anapambana na ufisadi? Tumetumia gharama kubwa na mbwembwe nyingi kuianzisha ila ipo kama pambo kama hiyo tu sio ufisadi ni nini??

TUJIKUMBUSHE: Vita ya Lowassa Urais na Rais Kikwete
 
Back
Top Bottom