Lowassa could've done better...

Lowassa could've done better...

acha kutudanganya ndugu, ulivoandika apo juu umekosea sana, Lowassa is not good katika maamuzi na uwajibikaji pia, na hana sifa za kua kiongozi bora
Unadhani nick name ya "mtu mwenye maamuzi magumu" ilianzia wapi?

Na uwajibikaji haukuwepo alipojiuzulu?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Uchambuzi mzuri. Ila kumbuka Lowassa hana maono kabisa ya uongozi. Rejea vision yake wakati wa uchaguzi: "education, education, education". Aliiga kwa Tony Blair (Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza) hii vision; na pia hakuwa na record nzuri ya kuendeleza elimu nchini. Legacy yake ilikuwa ni shule za kata. Ambazo karibu zote ni majanga. Kimaamuzi pia Lowassa ni bomu. Rejea memo alizokuwa akiandika kuharakisha suala la Richmond wakati wa uongozi wake ambazo zilikuja kuibuliwa na kamati ya Mwakyembe.

Sema yote lakini usiniambie Lowassa ni Kiongozi mzuri aisee. In fact, ukilinganisha na Magufuli, Magufuli is better, japokuwa mimi mwenyewe simkubali Magufuli sana.

So in your opinion huoni kama tatizo kubwa Tz ni elimu? No wonder!!
 
Lowassa zilipendwa hana nafasi tena katika siasa za bongo, atulie kama wenzake akina, Malecela , Dr. Salim, Msuya na wenginevo vinginevyo atakuja pata aibu tu
Kama ni zilipendwa, usitumie nguvu kubwa kumpinga na kumpakazia uongo.

Ni mtu wa tofauti siyo kama hao kina Msuya. Hao hawawezi kujitolea chochote kwa ajili ya Taifa hili. Wenyewe ni wastaafu wabinafsi na wengine wameshaambiwa wanawashwawashwa.
 
Muanzisha hii thread leo kaja na maada eti 'Lowassa angekuwa rais bora kabisa kuliko Magufuli'

muwe mnasimamia maamuzi na mitazamo yenu, mnakuwa na thamani zaidi--ulikuwa mpingaji sana wa ufisadi nchi hii

Fisadi anabaki kuwa fisadi haijalishi kaenda chama gani, yuko nje au jela, kama kaokoka na kujifanya malaika au la!!!

Fisadi ni identity hatakasikiki, wala kuosheka...wakiishafanya ufisadi kuna watu wanakufa kwa namna mbalimbali directly au indirectly! you can not reverse the damage done

Hata fisadi akaongea maneno matamu namna gani, au akaenda kukaa na watakatifu wa chadema! hata hawa watakatifu waliomuita kuja kunajisi ukuu wao bado haitamfanya fisadi kutakata!!

Vyama au mahali anapoenda na anapohamia havina mechanism ya kubadilisha moyo, damu na akili yake asiwe fisadi!

Lowassa ni fisadi sawa na walioko ccm, ambao for years wamejiwekea misingi ya unyonyaji, kuwa na biashara nzito na hawakutumika

Infact kisiasa Lowasa ni chadema, mirija, moyo na base zake zote za kupata hela ziko CCM inajulikana,

Lowasa na hao akina kikwete, mkapa, mwinyi , karamagi n.k wana biashara mbalimbali ambazo wako share

Leo anapokuja mwanachadema anatoa povu kana kwamba Lowasa alikufa akafufuka na akasahau na kuacha mambo yake ya kale unamwonea huruma!!

anapokuja ny.umb.u mmoja na kusema mbona hauyuko gerezani unacheka, kwani nani aliyesema ccm wasafi? hawa wote lao moja!!!!

endeleeni kusaga lami na ndala zenu zilizoisha

Lowasa kuwa Fisadi ni SI Unit, ni kama kuku KFC, au football barcelona, ni sawa na dhahabu barrick au ubongo wa lissu na sheria, Lowasa na ufisadi ni inseparable!!

Mengine yote semeni ila mtu huyu anapendeza sana kwa ID yake ya fisadi, imemvaa
Mimi nashangaa unapolazimisha kuwa Lowassa fisadi lkn mbona huyu aliyepo ndiye fisadi aliyekubuhu? Tena sisi tunataja ufisadi wake wazi lkn wewe unataka ufisadi wa kuambiwa. Haya ona ufisadi wa huyu MTU
1: kauza nyumba za serikali hata kwa wapenzi wake
2; kanunua kivuko kibovu
3: kavunja mikataba bila kufwata sheria hali iliyolitia hasara kubwa taifa letu
4: kakamata meli ya wachina kwa sifa tu na ameshindwa kesi tunalipa mabilioni
Amejenga barabara Nyingi zilizo chini ya viwango
Sasa mtu kama huyu unapata wapi nguvu ya kumtetea?
 
Mpaka leo sijaelewa kwanini kama ni fisadi kweli ile mahakama ya Yohana haijamshughulikia?? As a matter of fact hakuna ktk wote waliowahi kutuhumiwa tuliosikia mf Chenge wakipelekwa mahakamani sasa tutaamini vipi kuwa ni kweli alcohol anapambana na ufisadi? Tumetumia gharama kubwa na mbwembwe nyingi kuianzisha ila ipo kama pambo kama hiyo tu sio ufisadi ni nini??
 
Plagiarized work?
Theatre arts is plagiarism work. Mr Tony Blair's campaign words of "Education, education, education ... " were plagiarized by our theatre art expert. The decking of tarmac roads and so forth were all plgiarized work. I think this is what you meant Mr Invisible.
 
Jaribu kuwa makini unapojibu hoja ya mtu. Jina tu linakushinda. Hayo mengine inakuwaje?
 
Wengi hamjui kilichomponza Lowasa kwa JK.
Tatizo lilikuwa Lowasa kumdharau JK akiwa waziri mkuu kiasi cha kuwa akisafiri nje ya nchi bila kumjulisha JK wakati huo naye akiwa nje. Sasa jamaa alitaka kumuonyesha tu kuwa yeye yupo juu hata kama wao (Lowasa na marafiki zake) ndiyo waliomfikisha hapo juu.
Siungi mkono hoja
 
Magufuli ni rais bora kabisa kuwai kutokea. Acheni akili fupi za kiafrika, huyo lowassa kwa mfano angefanya nini ambacho magu hafanyi zaidi ya wizi yeye na genge lake la kina rostam karamagi
Kauli nyingine sidhni kama zinamantiki wewe ulijua MAGU kama atakua na akili za ajabu ajabu mara a waponde wenye vyet fake wakati huo huo anawakingia kifua wengine mcwe na ugonjwa wa kupendo chongo mkaita kengeza
 
Kama Mungu akimpa uzima, na afya ikawa inaruhusu, nina imani kuwa Lowassa bado ana nafasi ya kuongoza Taifa letu. Pengine akayafanya yale mazuri yaliyoko kwenye uongozi huu wa sasa, na kuachana na negativity zote za utawala huu.
Hapana ,..kwa lowasa zama zake zimeshapita.Yeye kama magufuli wana madhambi yao mengi sana kwa sababu kimsingi wote ni zao la CCM
 
Huyo Lowasa wakwenda kushirikiana na hao wakora wa Jubilee huko Kenya hapana asee bora tu Magufuli...kwa hizi move zake sidhan kama yule mzee alikua na nia njema na sisi kabisa mimi naona Mungu katuokoa tu kutupa Magufuli kule tungepotea kabisa yanayoendelea kwa sasa tuwe wavumilivu tu na tupige kazi tushaona hali yenyewe ipo kama hivi hio pesa kama kweli una uchungu nayo utapigana tu nchi bado ina fursa nyingi sio lazima kukaa huko maofisini au kuish kijanja janja hangaika unachopata rizika nacho tuache kua na tamaa za kuishi maisha ya wengine wakati kipato chetu halali tunakijua hata kama kitakua ni kidogo komaa tu hivyo hivyo hakuna mafanikio bila kupigika tulichokitaka tunatafutiwa ila hapo lazima tukubali wote tu kuteseka kama Taifa......kwani huko wafanyakazi mishahara imepunguzwa si ni ile ile au kwa wafanyabiashara kodi zimepanda sana kias cha kwamba hampati chochote? Kodi zile zile sheria zile zile tukubali tu wote tulifanya makosa tulipie tuliyoyatenda ndo tufike huko tulipotaka angalieni historia za mataifa yote huko ambayo tunatamani kua kama wao hawakufikia pale walipo kwa kutegemea mtelezo tu watu walijitoa kweli kuanzia viongozi hadi wananchi
 
kuhusu nyumba za serikali msikilize mwenyekiti wa chadema kanda ya pwani Mr Sumaye hapo juu anatoa ufafanuzi mzuri tu.

Richmond ni ya Lowassa ilo awezi chomoka, ukitaka ushaidi waulize lissu, mnyika na lema walishasema.ushahidi wanao.

Yani huyo Lowassa ni afadhari mtafute mwingine huyo ni mwizi ata nafsi yako inajua kutopandishwa kizimbani hakumfanyi kutokuwa mwizi wapo wezi wengi tu wa nchi hii awajafikishwa kortini sababu walituibia kwa akili nyingi lakini haiwafanyi kutokuwa wezi.

Magufuli ni kiongozi ni jasiri atatufikisha sehemu nzuri, amethubutu mpaka kugusa eneo la madini pamoja na kumbeza wengi tunaamini kuna matunda tutayaona huko.

Pengine sio mzuri kwenye siasa ndio maana vilio vyenu wengi haswa ni kwenye demokrasia.

Mkuu nimeiptia hii video kama nilivyoahidi. Lakini naona tunapishana hapa...

Kwanza tuachilie mbali issue kwamba uamuzi wote wa kuuza nyumba za serikali ulifanywa collectively na kwa kufuata taratibu, i.e. rais Mkapa kushauriwa kwake, tume kadhaa kuundwa. Hilo tuache.

Pointi yangu inakuja kwenye utekelezaji wa uncle Magu.

Kwasababu ilikuwa ni lazima mnunuaji awe mtumishi wa umma, ndugu yake alipewa hiyo status ili aweze kupewa nyumba hiyo. Nasema alipewa kwasababu ni kama tu waligawana hizo nyumba za umma ukiangalia hizo bei.

Suala la yeye kutake advantage ya uzembe wa serikali ambayo na yeye yumo kwa kuhakikisha ndugu wananufaika na ufisadi huo, ni ukosefu mkubwa sana wa uzalendo.
 
  • Thanks
Reactions: bne
Huyo Lowasa wakwenda kushirikiana na hao wakora wa Jubilee huko Kenya hapana asee bora tu Magufuli...kwa hizi move zake sidhan kama yule mzee alikua na nia njema na sisi kabisa mimi naona Mungu katuokoa tu kutupa Magufuli kule tungepotea kabisa yanayoendelea kwa sasa tuwe wavumilivu tu na tupige kazi tushaona hali yenyewe ipo kama hivi hio pesa kama kweli una uchungu nayo utapigana tu nchi bado ina fursa nyingi sio lazima kukaa huko maofisini au kuish kijanja janja hangaika unachopata rizika nacho tuache kua na tamaa za kuishi maisha ya wengine wakati kipato chetu halali tunakijua hata kama kitakua ni kidogo komaa tu hivyo hivyo hakuna mafanikio bila kupigika tulichokitaka tunatafutiwa ila hapo lazima tukubali wote tu kuteseka kama Taifa......kwani huko wafanyakazi mishahara imepunguzwa si ni ile ile au kwa wafanyabiashara kodi zimepanda sana kias cha kwamba hampati chochote? Kodi zile zile sheria zile zile tukubali tu wote tulifanya makosa tulipie tuliyoyatenda ndo tufike huko tulipotaka angalieni historia za mataifa yote huko ambayo tunatamani kua kama wao hawakufikia pale walipo kwa kutegemea mtelezo tu watu walijitoa kweli kuanzia viongozi hadi wananchi
Lowassa angekuwa rais halafu akapiga marufuku siasa za upinzani ndo ungeweza kuongea haya.
 
Magufuli anaumiza watu haohao anaojaribu kuwaponya. That's my problem with him. Huwezi kuniambia serikali inapiga vita ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi. Halafu serikali hiyohiyo ina pesa ya kukamata watu wake na kuwatisha kwa silaha za kivita pale hao watu wanapotaka kukusanyika kutoa maoni yao peacefully kuhusu mwelekeo wa nchi. Acha ujinga.
We are still a work in progress mda mwingine inabidi tu ufanye mambo ambayo watu hawatakuelewa ili malengo yatimie .....na lengo letu sote ni kuinua Taifa hili
 
Magufuli anaumiza watu haohao anaojaribu kuwaponya. That's my problem with him. Huwezi kuniambia serikali inapiga vita ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi. Halafu serikali hiyohiyo ina pesa ya kukamata watu wake na kuwatisha kwa silaha za kivita pale hao watu wanapotaka kukusanyika kutoa maoni yao peacefully kuhusu mwelekeo wa nchi. Acha ujinga.
Mbegu kabla ya kuota inabidi kuoza kwanza, halafu ndio inaanza kuota, ndio kanuni ya Kimungu, Magufuli ni Rais Mzuri sana, sio mnafiki kama hao wengine, Ni sifa ya shujaa, Magufuli anachosema ndio anachokifanya, hapindishi, lakini pia ameweza kufanya vizuri katika nyanja zote muhimu katika muda mfupi,Mafanikio yaliyopatikana katika miaka miwili ya Urais wake ni makubwa sana, muelekeo wa nchi miaka kumi ijayo unaleta matumaini, isipokuwa HAPA KAZI inataka ufanye kazi ili upate mkate, na uko mbele hakutakuwa na kukaa kwa shemeji tena.
 
EL siyo fisadi, angekuwa Fisadi basi serikali ya awamu ya Tano isiyovumilia ufisadi ingekuwa imeshamshitaki mahakamani!🙂
 
Lowassa angekuwa rais halafu akapiga marufuku siasa za upinzani ndo ungeweza kuongea haya.
Na ndio maana hajawa hio democracy kwetu huku kivuli tu cha hao wanyonyaji huko Kenya kwenyewe mnaposema ndo kuna demokrasia kubwa hao wanyonyaji wamekaa na hao viongozi wao wakiwakamua wananchi ila sababu matakwa ya watu fulani yako sawa na kuna watu wanafaidika na hao wanyonyaji mambo yanawekwa yaonekane sawa tu
 
Back
Top Bottom