Lowassa apanda chati kuelekea uchaguzi mkuu 2015

Lowassa apanda chati kuelekea uchaguzi mkuu 2015

Ni pigo kwa Chadema sijui mtamsimamisha nani Zitto, Mbowe au Dr Slaa.

Ritz, acha maneno ya vijiweni bana, hiyo research yenu ya kati ya watanzania kumi saba wanamtaka EL umeitoa wapi? Au ndo research ambayo sample uliyotumia siyo true representative of the whole population? , mi naona ccm sasa mmeanza kukosa watu wenye mvuto!
 
Huyu so ndie yuleeee aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond so inakuwaje leo tena pia huyu huyu si ndo katajwa na kina Nepi kuwa ni Mafisadi pacha na wakapewa siku 90 so inakuwaje huyu Ritz na Pasco wanamkana tajiri wao Nepi na kuwapa chepuo Lol!!!Kweli ukitaka kushabikia Ccm na Lowasa lazima uwe na akili za maiti,big up mleta mada una sifa hizo.
 
Ritz ni vigumu kuamini km ni ww ambaye ulishuhudia jamaa akigalagazwa Arumeru na Mkwewe jua kuna sehemu gata ukimsimamisha na jiwe hapiti
Muda bado una haraka ya nini Vikao vitaamua km hela ww kula tu
 
Sio mie ni Watanzania ndio wanamkubali Lowassa rekodi yake ya utendaji ndio inambeba hata ukimchukia ni kazi bure mkuu katika Watanzania 10 wakihojiwa saba kati yao wanamkubali.

Watanzania gani hao? Embu toa ***** wako hapa man, fisadi fisadi tu, hasafishiki, watu qa kujipendekeza kama nyinyi ndo mnamfurahia!
 
Katika uteuzi wa mgombea urais kutoka Chadema italeta mtafaruku mkubwa, Dr Slaa ambaye ameishapata uzoefu wa kugombea nafasi hiyo hatarudishwa tena na chama chake, huo ndio ukweli. Kwa maana nyingine Chadema watalazimika kumtafuta mgombea mwingine ambaye kwa wakati huo hatokuwa na uzoefu wa mikiki katika nafasi ya urais.

Mbali na kumtafuta mgombea mbadala wa Dr Slaa, viongozi wa kanda zingine hawataafiki mgombea atoke eneo moja tu kila chaguzi unapofika. Mparaganyiko huu utasababisha Chadema kuvutana na ikifika hatua hiyo.

Jamii ya Watanzania wataogopa kumchagua mgombea kutoka upinzani hususani katika nafasi ya urais.

Ritz,
You are visionary. Ingekuwa zamani tungekuita nabii.
 
Ngome ya Chadema ipo Kaskazini na sehemu alizopata kura Dr Slaa zinafahamika ni sehemu chache sana, sehemu kubwa ya Kaskazini Lowassa akisimama anapita, Chadema watapata sehemu za Arusha Mjini na baadhi ya maeneo ya Karatu na Arumeru.
 
Ninaamini kama Lowassa angekuwa Waziri Mkuu bado hadi leo, ule mradi wa maji wa Ziwa Victoria usingekuwa umeishia Shinyanga pekee, bali ungekuwa umeishafika katika wilaya za Nzega, Igunga na mikoa ya Singida na Dodoma.


So Ritz Unachomaanisha ni kuwa PM wa sasa PINDA is the worst PM of all the time au??? Koz hata shule za Kata alizozianzisha zimewashinda hata kupeleka walimu......I too Admire that GUY... Hakuna Kiongozi asiekula hata sisi tunaopiga domo hapa tuna michongo yetu but at least ukila onyesha na kinachofanyika kuliko kula na hakuna kinachofanyika.
 
Wakisema mwakiembe, na prof mwandosya kidogo nitawaelewa. Mimi natokea kaskazini lowasa ni mwizi tu.
 
Ngome ya Chadema ipo Kaskazini na sehemu alizopata kura Dr Slaa zinafahamika ni sehemu chache sana, sehemu kubwa ya Kaskazini Lowassa akisimama anapita, Chadema watapata sehemu za Arusha Mjini na baadhi ya maeneo ya Karatu na Arumeru.

Ngoja Mbopo na Nnauye Jr wasikie hii Habari
 
Last edited by a moderator:
EL kama atapita katika msuguano uliopo katika chama chake then am like 80% sure kuwa Jamaa atachukua Nchi.... Hakuna asie na mapungufu katika hali ya uanadamu na EL ana mapungufu yake ila kwa kipindi alichokua PM alifanya mambo Yes kuna suala la RICHMOND aliharibu inawezekana Yes alipiga Pesa au watu walimtumia kupiga Pesa ile ndefu lakini nani katika viongozi wa nchi hizi za Africa ananishi maisha mabayo si ya Kifisadi???

Kiongozi gani ambae mtoto/watoto wake wanasoma St. Govt???? Kiongozi gani mwenye Acc moja tu NMB??? Hakuna msafi hata mmoja na ukweli ni kuwa Kosa moja hufuta mema yote BUT To me LOWASSA is the best candidate to lead us katika kipindi kijacho... Infact ningekuwa JK ningemrudishia U PM amalizie aliyoyaanzisha. Na akipata will prove u guys mnaompinga wrong...... Kwa sababu EL ni mtu wa maamuzi na mwenye AMRI.......and that is the kind of leader I want.....
 
Wanabodi,

Wakati mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM unaendelea kuanzia ngazi ya shina hadi taifa. Mbunge wa Monduli Edward Lowassa anaonekana kupanda chati kwa kasi ya ajabu na kuonekana ana nafasi kubwa katika mbio za urais 2015.

Uchambuzi wa kisiasa unaonesha karibu kila kona ya nchi hii, katika watanzania 10 utakaowahoji kuhusu ni nani hasa anayefaa kumrithi Rais wa sasa Kikwete, saba kati yao wanamtaja Lowassa wakidai ni "Jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila Mtanzania.

Makundi makubwa yanayotajwa katika mnyukanakano huo ni pamoja na kundi la Lowassa, Samwel Sitta, na Bernad Membe. Kila mmoja anapambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanaingiza watu wao muhimu katika vikao vya (NEC) na ndani ya Jumuiya za chama hicho, UVCCM, UWT, na Wazazi, katika makundi yote hayo Lowassa anaonekana kuwa ni mtu makini ana nafasi kubwa ya kupenya na kupererusha bendera ya chama hicho.

Kusimama kwa Lowassa kama mgombea Urais ni pigo kubwa kwa vyama vya siasa hasa Chadema, CUF na NCCR Mageuzi. Kutokana na rekodi ya Lowassa, ni mtu wa kufuatilia kila jambo analoamini katika dhamira yake kwamba linafaa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni mwenye hulka ya kusaidia na kuchangia shughuli za kijamii bila kujali itikadi za kisiasa wala dini, tofauti na viongozi wengine wa kisiasa amekuwa mtu tegemeo katika shughuli za kijamii iwe za kanisani au msikitini.

Ukitaka kumjua Lowassa ni kiongozi wa namna gani, tembelea jimboni kwake Monduli ukaone namna alivyowezesha makundi ya vijana na wazee kiuchumi.

amekulipa sh ngapi uje kumpigia kampeni hapa, ht mtoto mdogo anajua rowasa hafai hta kuwa diwani we unasema anakubalika sana, halaf huo utafiti wako sijui umeufanyia wapi mi nimeuliza watu km 20 wote hawataki hata kulisikia hilo jina
 
Hayo ndiyo yametoka huko kwenye kamati ya mazishi ya ccm inayokutana huko idodomya?
 
Mwaka 1995 wakati anrejesha fomu Dodoma akiambatana na msanii mwenzake. Mwalimu Nyerere alimnyoshea kidole asiendelee zaidi ya hapo yaani kuota urais kwa sababu kuu moja nayo ni mali alizonazo hawezi kuzitolea maelezo juu ya uhalali wake. Naye Lowassa alikaa kimya ikiwa ni jibu la wazi kwamba; kilichosemwa na baba wa Taifa dhidi yake ni kweli tupu. Mtu ambaye hawezi kutoa maelezo ya jinsi alivyopata mali zake yaweza kuwa aliua, aliiba, alidhurumu nk.

Mnaomshabikia kwamba ni jembe, inawezekana mko sawa isipokuwa tu Lowassa anaweza kuwa jembe la kuzolea mavi. Mungu hamfichi mnafiki. Alichokisema Baba wa Taifa kilipuuzwa, kwani alianza mikakati na msanii mwenzake ya kuchukua nchi mara tu baada ya uchaguzi Mkuu 1995.

Kweli mwaka 2005, wakafanikiwa kuingia Ikulu, Lowassa akapewa nafasi ya Waziri Mkuu. Kama nilivyosema awali Mungu hamfichi mnafiki; ili kuthibitisha kuwa alichokisema Baba wa Taifa juu ya uadirifu wa Lowassa ni cha kweli; akaingia kwenye tope la Richmond iliyozaa Dowans, madudu yanayoliangamiza taifa kiuchumi na kijamii.

Kwa kashfa hiyo akaangukia pua pwaaaaaaaa!!!!. Nape na wenzake kwenye chama cha mafisadi wakaanza wimbo wa magamba huku wakimgusa Lowassa. Alipoona hawezi kufa peke yake; Lowassa akamnyoshea kidole msanii mwenzake kwamba anajua kila kitu kuhusu Richmond.

Baada ya hapo Nape na wapiga debe wenzake wamekaa kimyaaaa wakijidai kusahau wimbo wao wa magamba. Baadhi yetu tumeanza kusema eti alitolewa kafara ili kumlinda mkulu. Mtu anayeliangamiza taifa kiasi hiki hata kama kama kaambiwa na mkulu, kama anauchungu na watanzania kwa nini asingekataa?

Hicho hakikuwa kipimo cha uadirifu wake mbele za Mungu? Hata kama alihofia kitumbua kuingia mchanga; si heri kuliko kuangamiza roho za wengi? Hajakaa sawa akadai ataleta teknolojia ya mvua ya kutengeneza kutoka Thailand. Mara baada ya kuangukia pua, mradi huo haukuendelezwa lakini jumla ya shilingi bilioni 1.5 zikawa zimeshabebenwa. Kama mradi ungekamilika ungegharimu shilingi bilioni 14.

Je, kama mradi ulikuwa na tija kwa taifa kwa nini haukuendelezwa? Je, hii nayo inawezekana ilikuwa ni Richmond nyingine? Yaani yeye kila anayoyaita maamuzi magumu ni ya kuliangamiza taifa tu? Mwalimu Nyerere alimkataa mwaka 1995, 2005 akapewa u PM, muda mfupi akaondoka kwa kashfa ya Richmond, tumeshajifunza na kuamini alichokisema Nyerere. Huyu hafai hata mkimsafisha kwa tindikali.
 
Mwaka 1995 wakati anrejesha fomu Dodoma akiambatana na msanii mwenzake. Mwalimu Nyerere alimnyoshea kidole asiendelee zaidi ya hapo yaani kuota urais kwa sababu kuu moja nayo ni mali alizonazo hawezi kuzitolea maelezo juu ya uhalali wake. Naye Lowassa alikaa kimya ikiwa ni jibu la wazi kwamba; kilichosemwa na baba wa Taifa dhidi yake ni kweli tupu. Mtu ambaye hawezi kutoa maelezo ya jinsi alivyopata mali zake yaweza kuwa aliua, aliiba, alidhurumu nk.....i.

Mkuu Mwalimu Nyerere ni binadamu kama mie na wewe sio kila kitu akisema kinakuwa sahihi, Mwalimu alituchagulia Benjamin Mkapa, kafanya nini zaidi ya kuuza rasilimali zetu kwa wazungu.
 
amekulipa sh ngapi uje kumpigia kampeni hapa, ht mtoto mdogo anajua rowasa hafai hta kuwa diwani we unasema anakubalika sana, halaf huo utafiti wako sijui umeufanyia wapi mi nimeuliza watu km 20 wote hawataki hata kulisikia hilo jina

Hii dhana sijui Pro-Chadema mmeitoa wapi mtu yeyote ambaye Against Chadema mnasema analipwa vipi na nyie mnalipwa na Chadema kumtetea Dr Slaa humu JF.
 
Sasa hayo ni matusi kwa jamii ya kimasai, ni sehemu gani ambayo akuna ombaomba hata Ulaya na Marekani ombaomba wamejaa sio Monduli peke yake, au Dr Slaa akipewa nchi Tanzania itakuwa aina ombaomba.

Mi ni mmasai wa simanjiro mkuu............ najua ninachosema

kuna kuvaa vazi la kimasai kwa heshima na kuvaa vazi la kimasai kusiko kwa heshima..... Ninajua ninachosema; ukiamua kubisha endelea... ndio maana nimeweka kauli kali ili tujitazame upya kwa kusifia ujinga; hivi wajua ndugu zetu kule zanzibar wanachofanywa?? je wajua pia yanayoendelea kati ya meserani na mto wa mbu na wazungu wachache wanaotumia naivety ya vijana wetu??

TUENDELEE NA HOJA YA UBORA NA STRENGTEHNING YA EL KWENYE DURU ZA SIASA JAMII YANGU NIACHIE NAJUA NATAFUTA NINI HAPO
 
Back
Top Bottom