Alloyce PR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 803
- 868
Viongozi, kumbukeni kwamba mwaka 2030 bado uko mbali. Kazi yenu kwa sasa ni kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na kutekeleza wajibu wenu kwa matokeo yanayoonekana.
Mkianza mbwembwe za kisiasa mapema na kujenga taswira ya kutafuta umaarufu binafsi, mnaweza kujikuta mkirudia makosa yaliyowahi kuwagharimu wanasiasa wengine kama Edward Lowassa na Bernard Membe.
Tambueni kuwa CCM ni chama chenye mfumo mpana na wenye ushindani mkubwa wa ndani. Hivyo, badala ya kujitangaza kupitia mambo madogomadogo, elekezeni nguvu zenu katika utendaji, huduma kwa wananchi, na kujenga imani ya umma. Mwisho wa siku, matendo ndiyo yatakayowatambulisha kuliko kelele.