Lowassa apanda chati kuelekea uchaguzi mkuu 2015

Hizi ni story za magreen guards baada ya kushikishwa bahasha za kaki.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ndugu usilete porojo huo utafiti umeufanyia wapi? na hiyo sample ilikuwa ni akina nani na wapi? nchi hii kwa sasa CCM haipendwi na imepoteza mvuto na hakuna atakaye simama kuiokoa hapo 2015.
Ritz+Redet [Dr Benson Bana's private company]= Urithi wa mikoba ya Sheikh Yahya!!!
 
Ninategemea wachangia wa jamvi hili 75% wapo chini ya miaka 50 kushuka chini na wana ufahamu wa kutosha kama si elimu ya kutosha. Vile vile wachangiaji wote ni Watz 100%. Hoja yangu hapa ni kwamba kwa mtu mwenye akili timamu na anaipenda Tanzania na watu wake aNATARAJIWA asimfikirie lowasa edward kam-candididate wa kutoka chama chochote. Kama anayewatuma ni yeye,,, basi awatume kupiga kampeini jinsi ya kuendesha business zake ambazo mtaji wake umepatikana kwa mashaka. Otherwise, tuondoleee kichefu chefu na kutulisha ujinga
 
Ebu mtu mwenye ushahidi pasi na shaka juu ya wizi wa mtu huyu ajitokeze hadharani na awe wa kwanza kumrushia jiwe! Napata hofu kuwa hizi kambi ndo tatizo na hazina ushahidi wa mtu makini. Waache wapigane wao kwa wao sisi tunasonga mbele na ikulu 2015 ni ya cdm!
 
Wanabodi,

Wakati mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM unaendelea kuanzia ngazi ya shina hadi taifa. Mbunge wa Monduli Edward Lowassa anaonekana kupanda chati kwa kasi ya ajabu na kuonekana ana nafasi kubwa katika mbio za urais 2015.

Uchambuzi wa kisiasa unaonesha karibu kila kona ya nchi hii, katika watanzania 10 utakaowahoji kuhusu ni nani hasa anayefaa kumrithi Rais wa sasa Kikwete, saba kati yao wanamtaja Lowassa wakidai ni "Jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila Mtanzania.

Makundi makubwa yanayotajwa katika mnyukanakano huo ni pamoja na kundi la Lowassa, Samwel Sitta, na Bernad Membe. Kila mmoja anapambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanaingiza watu wao muhimu katika vikao vya (NEC) na ndani ya Jumuiya za chama hicho, UVCCM, UWT, na Wazazi, katika makundi yote hayo Lowassa anaonekana kuwa ni mtu makini ana nafasi kubwa ya kupenya na kupererusha bendera ya chama hicho.

Kusimama kwa Lowassa kama mgombea Urais ni pigo kubwa kwa vyama vya siasa hasa Chadema, CUF na NCCR Mageuzi. Kutokana na rekodi ya Lowassa, ni mtu wa kufuatilia kila jambo analoamini katika dhamira yake kwamba linafaa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni mwenye hulka ya kusaidia na kuchangia shughuli za kijamii bila kujali itikadi za kisiasa wala dini, tofauti na viongozi wengine wa kisiasa amekuwa mtu tegemeo katika shughuli za kijamii iwe za kanisani au msikitini.

Ukitaka kumjua Lowassa ni kiongozi wa namna gani, tembelea jimboni kwake Monduli ukaone namna alivyowezesha makundi ya vijana na wazee kiuchumi.

Ritz, nitafurahi sana akipita Lowasa kupambana na Dr. Slaa!!!! Atasaidia sana ushindi!!!!!! Welcome Fisadi EL!!!! Rich wa Monduli? Katika kampeni atalieleza Taifa essence ya Richmond and the birth of Dowans. Kibaya zaidi ile fidia tunailipa kupitia jasho letu, hizo billions zingesaidia huduma za afya, elimu na maji.
 
kila mtu anamjua kuwa ni fisadi CCM wakilogwa kumsimamisha kama rais ndio mwisho wao
kila kona ya nchi hata watoto ukiwauliza nitajie mafisadi unaowafahamu lazima utasikia LOWASAAAAA
safi sana natamani 2015 ifike mapema nione mwisho
mlishindwa kuvuana magamba saa mnahalalisha gamba hii kali
 
Mkuu Ritz sikujua na wewe unasapoti kambi ya lowassa,hivi na madudu yote ya Richmond na mvua za kutengeneza unafikiri anaweza kupenya??

Acha wamlete kaka, jamaa anakubalika si mchezo tuleteeni huyo mtu 2015.......M4C tukipange
 
Wanabodi,

Wakati mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM unaendelea kuanzia ngazi ya shina hadi taifa. Mbunge wa Monduli Edward Lowassa anaonekana kupanda chati kwa kasi ya ajabu na kuonekana ana nafasi kubwa katika mbio za urais 2015.

Uchambuzi wa kisiasa unaonesha karibu kila kona ya nchi hii, katika watanzania 10 utakaowahoji kuhusu ni nani hasa anayefaa kumrithi Rais wa sasa Kikwete, saba kati yao wanamtaja Lowassa wakidai ni "Jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila Mtanzania.

Makundi makubwa yanayotajwa katika mnyukanakano huo ni pamoja na kundi la Lowassa, Samwel Sitta, na Bernad Membe. Kila mmoja anapambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanaingiza watu wao muhimu katika vikao vya (NEC) na ndani ya Jumuiya za chama hicho, UVCCM, UWT, na Wazazi, katika makundi yote hayo Lowassa anaonekana kuwa ni mtu makini ana nafasi kubwa ya kupenya na kupererusha bendera ya chama hicho.

Kusimama kwa Lowassa kama mgombea Urais ni pigo kubwa kwa vyama vya siasa hasa Chadema, CUF na NCCR Mageuzi. Kutokana na rekodi ya Lowassa, ni mtu wa kufuatilia kila jambo analoamini katika dhamira yake kwamba linafaa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni mwenye hulka ya kusaidia na kuchangia shughuli za kijamii bila kujali itikadi za kisiasa wala dini, tofauti na viongozi wengine wa kisiasa amekuwa mtu tegemeo katika shughuli za kijamii iwe za kanisani au msikitini.

Ukitaka kumjua Lowassa ni kiongozi wa namna gani, tembelea jimboni kwake Monduli ukaone namna alivyowezesha makundi ya vijana na wazee kiuchumi.

Yap!Ritz tuleteeni basi uwanjani, washauri Magamba wote wamsapoti ...M4C tunasema unacho njoo huna njoo lete Lowasa,leta Membi tunapita mule mule.Huyo babu Arumeru tulikutana nae wala hatuku feel...kama ya mkwewe hakujifunza tuna sema shega tu mleteniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Ninategemea wachangia wa jamvi hili 75% wapo chini ya miaka 50 kushuka chini na wana ufahamu wa kutosha kama si elimu ya kutosha. Vile vile wachangiaji wote ni Watz 100%. Hoja yangu hapa ni kwamba kwa mtu mwenye akili timamu na anaipenda Tanzania na watu wake aNATARAJIWA asimfikirie lowasa edward kam-candididate wa kutoka chama chochote. Kama anayewatuma ni yeye,,, basi awatume kupiga kampeini jinsi ya kuendesha business zake ambazo mtaji wake umepatikana kwa mashaka. Otherwise, tuondoleee kichefu chefu na kutulisha ujinga

Mkuu wangu sijakupata.
 
Something is telling me Ritz and Pasco are one and the same person.

Or is it me??
 
.................Hivi huyo Lowasa hata akishinda huo urais watakoma Chadema au CCM ya akina JK ambao walimtosa wakati walimuahidi watamsafisha?
 
lazima mtu anayegawa unga katikati ya watu wavivu kufikiri apande chati.uvivu huo wa kufikiri unatupeleka pabaya kabisa
 
Pro-Chadema JF wengi wao hawana ujanja mbele ya Lowassa, wapo tayari kumtosa Dr Slaa.
 
.................Hivi huyo Lowasa hata akishinda huo urais watakoma Chadema au CCM ya akina JK ambao walimtosa wakati walimuahidi watamsafisha?

Mkuu naona umekiri mwenyewe kama Lowassa ni Jembe.
 
Ritz, nakubaliana na wewe kuwa Lowassa ni jembe sijui fyekeo akiwa huko ndani ya Magamba ila kwa upande wangu mimi napenda sana CCM wamsimamishe Lowasa ili Chadema ipunguze gharama za kampeni.
 
Mkuu naona umeamua kujiliwaza Lowassa ndio atakae ibomoa ngome yenu ya Kaskazini.
 
Wanabodi,

Kusimama kwa Lowassa kama mgombea Urais ni pigo kubwa kwa vyama vya siasa hasa Chadema, CUF na NCCR Mageuzi.
inaweza pia kuwa pigo kwa ccm kwani upinzani unaweza kupita kiulaini ikiwa EL atagombea kupitia ccm
 
Mkuu naona umeamua kujiliwaza Lowassa ndio atakae ibomoa ngome yenu ya Kaskazini.

Mkuu, natamani haya maneno Mungu ayatie muhuri na tuombe CCM wampitishe Lowasa halafu tuwe na uzima baada ya Uchaguzi 2015 tuwe hapa tunaandika kama hivi. Lowasa ndo atakuwa shrt cut ya ushindi kwa Chadema, akisimamishwa kugombea utatokea mpasuko ndani ya CCM ambao hakuna mtu aliyeweza kufikiria na mtu wa kwanza kukimbia chama atakuwa JK, Sitta, Mwakyembe na wengineo pamoja na Bendera yao(Nape Nnauye).............Lowasa akiwa Rais najua waziri mkuu atakuwa Rostam na Chenge nae lazima apewe nafasi ya juu juu ili wamalizie malizie vijisenti walivyokosa kosa kuviiba.
 
Back
Top Bottom