Mtu wa Kwao
JF-Expert Member
- Jan 15, 2008
- 258
- 21
Jamani sasa tumeanza kuona wale waliohongwa na lowassa ila wamtetee.UNAJUA WATU WENGI HAWAJASOMA ILE RIPOTIsasa wanasikiliza tu mtaani kumesemwa nini jamani someni na uzuri iko humuhumu jfsMkuu Pope,
Uwe muangalifu sana usijejipaka matope wakati unataka kumwosha mtu.
1. Kama umesoma vizuroi ripoti ya bunge (maana kuna uvivu sana wa kusoma ile, hata RA aliambiwa asome yeye akarukia jambo lingine) utaona kwamba kuna sababu kwa nini hakuhojiwa. Kama wawakilishi wa wananchi walijiridhisha na ripoti ile, wewe inabidi ujenge pointi za maana sana ili tukusikilize.
2. Edo alifanya jambo la ajabu sana kutumia nafasi aliyopewa bungeni achangie mjadala unaomhusu, nafasi ambayo angeweza kujitetea, kuwa alisingiziwa kwa sababu hii na ile, badala yake yeye akatangaza kwa jazba kuwa ana resign. Amefika wapi?
3. Amegundua sasa kuwa uamuzi wake utagharimu maisha yake yote yaliyobaki kisiasa, na ameanza kukuru kakara kuanza kujitetea, tena kwa kuwasingizia wenzake.
4. Lakini ukweli ni kuwa, hata ripoti haijasema yeye alihusika kwa namna unayoielezea...soma ripoti uelewe, na ujue kuwa we are watching guys like you who comes up with attractive threads to cleanse the Richmond scandal guys. Tumejadili kwa mapana sana juu ya mambo ya Lowasa et al, kabla hujajiunga hapa.
5. Edo ameshindwa hata kujitetea jana kwenye TvT. Alichoongea kwa kweli hakina mantiki kwa ku settle dust la Richmond. Huwezi kusema sasa umegundua Edo alionewa na kamati, na ukatupa sababu za maana.
Tu convince kwa hoja tukuelewe, si kwa blah blah tu, Mkuu. Karibu sana.
Jamani sasa tumeanza kuona wale waliohongwa na lowassa ila wamtetee.UNAJUA WATU WENGI HAWAJASOMA ILE RIPOTIsasa wanasikiliza tu mtaani kumesemwa nini jamani someni na uzuri iko humuhumu jfs
Jana usiku nimesema hila na ghilba za wana CCM, system na JK mwenyewe kutumia watu na vyombo kumsafisha Edo. Leo mmeanza kuona nadhani Pope hajasoma mabandiko yangu . Wakati niko mtaani naona Pope kaja na yale niliyo yasema .Haya kazi kwenu .
LUNYUNGU ushindi ni lazima kwa gharama yoote ile.Sasa tumeanza kuwaona na bado wale wa magazet yani waandishi wenye tamaa wataandika maajabu huko yetu macho.jamani kama kuna mwenye kufahamu site ya mwanahalisi anisaidie wakuuJana usiku nimesema hila na ghilba za wana CCM, system na JK mwenyewe kutumia watu na vyombo kumsafisha Edo. Leo mmeanza kuona nadhani Pope hajasoma mabandiko yangu . Wakati niko mtaani naona Pope kaja na yale niliyo yasema .Haya kazi kwenu .
Ndugu Kishaju,
Pole kwa tatizo la kushindwa kunukuu.
Ukitaka kumnukuu mtu, (quote) fanya hivi,
1. bonyeza "Quote",iliyo chini ya posti ya huyo unayetaka kumnukuu maoni yake.
2. Kutakuwa na maandishi uliyonukuu, sasa wewe andika chini kabisa ya maandishi hayo pahala penye nafasi tupu.
3. Ukishamaliza kuandika maoni yako, Bonyeza "Post reply"Mpaka hapo utakuwa ushamnukuu mtoa maoni na maoni yako yataonekana chini yake.
Kama nilivyosema huko nyuma, Mwakyembe ilibidi amhoji Lowassa.Sababu zilizotolewa katika ripoti haziridhishi.
Naelewa Lowassa anahusika kama sio moja kwa moja katika rushwa basi anawajibika kama Waziri Mkuu, mtu aliyetakiwa kuhakikisha mambo yanaenda sawa.Kwa hiyo kusema "Lowasa kaonewa" inakuwa kwenda mbali kwa sababu inatoa picha kwamba Lowassa hakuhusika kabisa, au hakupewa nafasi ya kujitetea hata bungeni, which is not the case.
Tatizo ni kwamba kutomhoji kwa Mwakyembe na wenzake kumepelekea ripoti kutolewa bila input yake.Lowassa anaweza kusema kuwa ripoti ile ambayo ndiyo ime influence yeye kutoka uwaziri mkuu ilikuwa biased na yeye hakupata nafasi ya kujitetea as far as that report is concerned.It is important that justice not only be dispensed, but also that justice appears to be dispensed.The fact that in this case at least in the context of the report there is room for justice to appear as not dispensed is troubling. Mimi naona Mwakyembe angemhoji Lowassa, halafu Lowassa angejitetea kwamba "nilijaribu kuvunja mkataba lakini watendaji walinishauri vinginevyo" na ripoti ingeyafanyia uchunguzi zaidi madai hayo, ripoti ingetoka ikiwa imekamilika zaidi.
Tatizo linalojitokeza sasa ni kuwa Lowassa anasema alishauriwa vibaya na watendaji, watendaji wanasema walikuwa pressured na Lowassa, moja kati ya pande mbili hizi haisemi kweli.Mwakyembe alikuwa na nafasi nzuri sana ya kuangalia mambo kama timeline na vitu vingine muhimu kwa kuzihoji pande mbili zote.Inawezekana kabisa Lowassa anajikosha tu na kutaka kwake kuuvunja mkataba kulikuja baadaye sana alipoona mambo yanaenda arijojo.
Mwakyembe angemhoji Lowassa leo hii tungejua vitu kwa mwanga mzuri zaidi na pengine Lowassa angekosa cha kusema to the point ya kukubali guilt ya kuwa pressure watendaji.
Hoja kwamba Lowassa alikuwa na nafasi ya kujitetea bungeni ni nzuri lakini kama mtu anaipotray ripoti ya Mwakyembe kama a well concocted witch hunt iliyokuwa na nia moja tu ya kumtoa Lowassa kwa kukusanya circumstantial evidence nyingi sana na kuchukua public opinion miongoni mwa wabunge, then regardless ya utetezi wa Lowasa alikuwa ameshamalizwa kisiasa na ripoti na utetezi zaidi ungeweza hata kukigawa chama na serikali, so in principle angeweza kujitetea lakini in reality ilibidi awajibike at least kwa uongozi mbovu au hata kwa involvement, lakini hata kama hakuwa involved directly utetezi zaidi ungelipua mgawanyiko zaidi.
Kamati ya Mwakyembe ilifanya kazi nzuri.Ingefanya kazi nzuri zaidi kama ingemhoji Lowassa kabla ya kuwakilisha ripoti bungeni.
Hivi Lowassa hana washauri? kama anao basi wamwambie anyamaze anatuchefua. kila nikikumbuka milioni 152 kwa siku namkumbuka yeye hata kama alikuwa hachukui yeye lakini kafanya uzembe usiovumilika. Asiendelee kuongea anatupandisha hasira.
Kama nilivyosema huko nyuma, Mwakyembe ilibidi amhoji Lowassa.Sababu zilizotolewa katika ripoti haziridhishi.
Naelewa Lowassa anahusika kama sio moja kwa moja katika rushwa basi anawajibika kama Waziri Mkuu, mtu aliyetakiwa kuhakikisha mambo yanaenda sawa.Kwa hiyo kusema "Lowasa kaonewa" inakuwa kwenda mbali kwa sababu inatoa picha kwamba Lowassa hakuhusika kabisa, au hakupewa nafasi ya kujitetea hata bungeni, which is not the case.
Tatizo ni kwamba kutomhoji kwa Mwakyembe na wenzake kumepelekea ripoti kutolewa bila input yake.Lowassa anaweza kusema kuwa ripoti ile ambayo ndiyo ime influence yeye kutoka uwaziri mkuu ilikuwa biased na yeye hakupata nafasi ya kujitetea as far as that report is concerned.It is important that justice not only be dispensed, but also that justice appears to be dispensed.The fact that in this case at least in the context of the report there is room for justice to appear as not dispensed is troubling. Mimi naona Mwakyembe angemhoji Lowassa, halafu Lowassa angejitetea kwamba "nilijaribu kuvunja mkataba lakini watendaji walinishauri vinginevyo" na ripoti ingeyafanyia uchunguzi zaidi madai hayo, ripoti ingetoka ikiwa imekamilika zaidi.
Tatizo linalojitokeza sasa ni kuwa Lowassa anasema alishauriwa vibaya na watendaji, watendaji wanasema walikuwa pressured na Lowassa, moja kati ya pande mbili hizi haisemi kweli.Mwakyembe alikuwa na nafasi nzuri sana ya kuangalia mambo kama timeline na vitu vingine muhimu kwa kuzihoji pande mbili zote.Inawezekana kabisa Lowassa anajikosha tu na kutaka kwake kuuvunja mkataba kulikuja baadaye sana alipoona mambo yanaenda arijojo.
Mwakyembe angemhoji Lowassa leo hii tungejua vitu kwa mwanga mzuri zaidi na pengine Lowassa angekosa cha kusema to the point ya kukubali guilt ya kuwa pressure watendaji.
Hoja kwamba Lowassa alikuwa na nafasi ya kujitetea bungeni ni nzuri lakini kama mtu anaipotray ripoti ya Mwakyembe kama a well concocted witch hunt iliyokuwa na nia moja tu ya kumtoa Lowassa kwa kukusanya circumstantial evidence nyingi sana na kuchukua public opinion miongoni mwa wabunge, then regardless ya utetezi wa Lowasa alikuwa ameshamalizwa kisiasa na ripoti na utetezi zaidi ungeweza hata kukigawa chama na serikali, so in principle angeweza kujitetea lakini in reality ilibidi awajibike at least kwa uongozi mbovu au hata kwa involvement, lakini hata kama hakuwa involved directly utetezi zaidi ungelipua mgawanyiko zaidi.
Kamati ya Mwakyembe ilifanya kazi nzuri.Ingefanya kazi nzuri zaidi kama ingemhoji Lowassa kabla ya kuwakilisha ripoti bungeni.
Mpaka muda huu bado Lowasa hajachelewa.Namshauri kwa kuwa Kamati wa a legal thing basi na yeye anaweza kwenda Mahakamani kusafisha jina lake .Haki hii anayo kabisa na ya kimsingi .Lakini Wakili itabidi amuulize juu ya madai yake ya Natural Justice .Maana anaililia yeye lakini alio wahi kuwafukuza kazi tena kujwaani kwa aibu kubwa sijui hawakuwa entitled na hilo ?
.........kwa kuwa yeye mwenyewe EL alidai ripoti ya tume ingekuwa tofauti kama angeitwa na kujieleza.................
sasa tumeona maelezo yake TvT.................hivi wandugu mnafikiri maelezo yake yangebadilisha kitu gani katika ripoti ile??????..........ABSOLUTELY NOTHING!!,
......walio wavivu wa kusoma ndio watakuja na kila sababu za kutaka kuosha huu uovu wa Richmond.............
Bob Mkandara you have said it all my brother............!!!
Process ya ku-procure the so called Richmond ndio TATIZO ambalo lilipata baraka za EL....thats where the PROBLEM IS......................maelezo mengine yooote ni kufurahisha jamvi................na hapa ndio watu waelewe ni kwa jinsi gani WANASIASA WANAVYOWABURUZA WATAALAMU!!!
Imagine this.......kampuni iliyokuwa rated low if not the lowest in the evaluation of tender ndiyo ikachukuliwa kupewa zabuni under EL Influence.................halafu baadaye unakuja kuwauliza makatibu wakuu and senior officers ili hali wakijua kabisa mpaka kufikia hatua hiyo ni wewe EL uliyesababisha........unafikiri wangekuambia nini BOSS wakati wanajua wewe mwenyewe ulikuwa forefront ili Richmond ipate Zabuni.......halafu funny enough swali lako kwao hao makatibu wakuu lilikuwa extremely WEAK.......na wao kujiweka on safe side...."only at that particular moment" (ofcourse not now......because they got to go as well).....na wakakujibu kirahisi within AN HOUR kuwa the CONTRACT is CLEAN!!!.....very funny indeed.................in other words walikuwa (PSs and senior Officers) wanakuambia "....thats your ball BOSS...."
na sasa tunasema hao makatibu wakuu, mwanasheria mkuu, DG PCCB na other senior officers waliohusika wawajibishwe....kwa sababu walishindwa kumshauri BOSS wao amabye tayari keshawajibika........wao wanasubiri nini?.....hatuataki WATU WAOGA WA KUSHAURI SERIKALINI.....ndio maana tunaishia shimoni kila siku kwa sababu za UWOGA
Ni kweli pengine angelihojiwa angelitoa maelezo kuhusu kilichojiri. Kwa kusikiliza maelezo yake TVT kupitia KLHNews, kumhoji kusingelibadilisha ulazima wa yeye kuwajibika. Nikimnukuu H.Truman "The buck stops here", yeye ndiye aliyeichagua kamati hivyo, muwajibikaji kwa mazuri(misifa) na mabaya anabakia yeye wala si akina Mgonja au Mwanyika. Kushituka baada ya mkataba kutiwa sahihi lazima kuwe na vipengere vinavyoruhusu. Kosa la kutokuwa na vipengere hivyo ni la Mwanyika kiutekelezaji. My dear Lowassa you have to bear your political responsibility with humility.
KASHFA ya Richmond iliyomlazimisha aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili kujiuzulu na baadaye kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri imeendelea kuchukua sura mpya kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele.
Ushahidi wa ukweli huu unathibitishwa na kuibuka kwa mambo mapya kila kukicha, kubwa kati ya hayo likiwa ni lile la jana usiku la Televisheni ya Taifa kukatisha ghafla mahojiano yale na Lowassa.
Tukio hilo la jana usiku lililokuja wakati usiotarajiwa linaweza likafungua ukurasa mpya wa kisiasa kwamba, viongozi wa juu serikalini huenda sasa wameanza kuhofia kwamba Lowassa anaweza akaibua masuala mengine yanayoweza kuhatarisha amani au kuimega serikali.
Aidha kukatwa kwa mahojiano hayo kunaweza kukafungua ukurasa mpya wa hoja kwamba, sasa ni wazi kuwa, Lowassa ameanza kutengwa waziwazi na viongozi wakuu serikalini ambao amefanya nao kazi kwa muda mrefu, kiasi kwamba hakuna aliye tayari kumuona mwanasiasa huyo akijaribu kujijenga upya kisiasa au kujisafisha kwa gharama za kufichua kila anachokijua kuhusu sakata la Richmond.
Hadi wakati TvT wakikatisha ghafla mahojiano hayo jana usiku, tayari Lowassa alikuwa ameshaeleza mambo mengi ambayo pia alikuwa ameyasema jana jioni wakati wa mkutano wake wa hadhara alioufanya nyumbani kwao Monduli alikokwenda kuwaleza wapigakura nini kilitokea bungeni hata akalazimika kujiuzulu.
Aidha, mbali ya hayo, wiki hii imeshuhudia kuanza kufunguka au kufichuliwa kwa masuala mengine mapya yanayozingira sakata hilo la Richmond ambalo mbali ya Lowassa, lilisababisha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ibrahim Msabaha, kuondoka madarakani kutokana na majina yao kutajwa katika mzingo wa sakata zima la Richmond.
Katika hatua nyingine, kauli zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete na Sheikh Yahya Hussein kuhusu Richmond zimeanza kuzua mijadala huku baadhi ya wadadisi wa mambo wakiziona kuwa zilizo na ajenda mahususi za kuweka mambo sawa.
Wakati Kikwete akionekana kujaribu kunawa mikono dhidi ya lawama zinazoelekezwa kwake za kuwatelekeza marafiki zake wa siku nyingi, Lowassa na Rostam Aziz, wakishutumiwa vikali hata kutakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria, matamshi ya Sheikh Yahya yanaonekana kuchukua mwelekeo wa kuwa na ushawishi wenye malengo mahususi.
Wadadisi wengine wa mambo wanaiona kauli ya Kikwete aliyoitoa kwa wazee wa Dar es Salaam akimsafisha Lowassa kuwa ilitolewa na mkuu wa nchi ambaye alishindwa kusoma alama za nyakati ambazo zilikuwa zikimtaka kutoonyesha kufungamana na upande wowote katika masuala yanayohusu ufisadi.
Katika hatua ambayo huenda haikutarajiwa na baadhi ya watu, baada ya kimya cha siku kadhaa, Lowassa na Karamagi, wameanza kutoa kauli ambazo zinatoa mwelekeo wa kuanza kujibu mashambuli makali yanayoelekezwa kwao tangu Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, ilipowasilisha ripoti yake ya uchunguzi kuhusu mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kati ya Kampuni ya Richmond Development Company na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Wakati Lowassa akitoa kauli, kwanza kupitia katika mahojiano aliyofanya na Televisheni ya Taifa (TvT) yaliyorushwa jana usiku na pia katika mkutano wa kwanza wa hadhara alioufanya nyumbani kwao Monduli jana hiyo hiyo alasiri, Karamagi yeye ametoa kauli yake katika mahojiano ya ana kwa ana aliyofanya na gazeti hili.
Wakati hayo yakitokea, Karamagi naye katika mahojiano na gazeti hili wiki hii, alitangaza nia yake ya kupambana na watu aliodai kuwa walihusika kuchafua jina lake kwa kumhusisha katika kashfa ya Richmond.
Alisema hatakaa kimya dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake na wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge, iliyochunguza mchakato wa upatikanaji wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura ulioipa ushindi Richmond.
Akizungumza kwa kujiamini, Karamagi alisema hakubaliani moja kwa moja na ripoti ya kamati hiyo kwa sababu baadhi ya aya zilizomo katika ripoti, zinaonekana kuwekwa makusudi kwa ajili ya kumchafua, yeye pamoja na baadhi ya viongozi wenzake waliolazimika kujiuzuru nyadhifa zao baada ya kutajwa kuhusika na kashfa hiyo.
Baadhi ya maeneo katika ripoti hiyo sikubaliani nayo kabisa, yalipotosha hali halisi ilivyokuwa, yalilenga kunichafua na kunidhalilisha mbele ya jamii, mimi pamoja na wenzagu tuliojiuzuru.
Kamati ilisikiliza na kuruhusu maneno ya umbea kuingizwa katika ripoti, inaonekana wajumbe wa kamati walifurahia kuingiza umbea katika ripoti yao. Hili lilivuruga kabisa hata yale mazuri yaliyokuwa katika ripoti hiyo. Ni wazi yalichomekwa kwa ajili ya kutuchafua, alisema Karamagi.
Akizungumza kuhusu kutohusika na kashfa hiyo, alisema alihamishiwa Wizara ya Nishati na Madini Oktoba 19,2006 na alipoingia ofisi alikuta barua kutoka Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO iliyoandikwa Oktoba 13, 2006, siku sita kabla ya kuingia katika ofisi hiyo ikielezea hali halisi ya tatizo la umeme nchini na ilitoa ushauri wa nini kifanyike ili kukabiliana na hali hiyo.
Barua hiyo ambayo Tanzania Daima Jumapili iliiona, imesainiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi wa TANESCO, Balozi Frugence Kazaula pia inaeleza kutambulika kwa utapeli uliokuwa ukitumiwa na kampuni ya Richmond kuihadaa serikali juu ya kuwasili kwa mitambo hiyo ya kufua umeme wa dharura.
Bodi ya Tanesco ilikuwa imeiandikia serikali ikieleza utapeli wa Richmond, hatua za kuchukua kukabiliana na tatizo la umeme na ilishauri kujiepusha na malumbano yoyote kwa wakati huo na kampuni hiyo kwa sababu yangeweza kuharibu mambo.
Mimi nilianza kuifanya kazi barua hiyo baada ya kushauriana na wenzangu na kuona tulikuwa na kila sababu ya kufanyia kazi mapendekezo yaliyokuwa katika barua hiyo. Sikuhusika na kusaini mkataba wa Richmond wala kushinikiza ipewe upendeleo wowote, nilikuta imeshachukuliwa na imeshangulika ni ya kitaperi.
Ajabu ninatajwa katika kamati kuwa nilishikiza Richmond au dada yake Dowans kuendelea na kazi.Inaumiza sana kuona mtu mzima anakuzulia jambo la ajabu namna hiyo, alisema Karamagi.
Karamagi ambaye mahojiano yake yamechapishwa ndani ya gazeti hili leo, alieleza kushangazwa na kitendo cha kamati hiyo kutotumia barua ya Bodi ya Tanesco iliyokuwa ikiishauri serikali cha kufanya katika kukabiliana na tatizo la umeme licha ya kuwasilisha barua hiyo kwa Spika wa Bunge Samuel Sitta, badala yake ilitumia barua ya Mwakilishi wa Net Group Solutions.
Hata hivyo alisema hata baada ya kutokea mambo hayo yeye binafasi hana tatizo na chama chake, Chama Cha Mapinduzi: Sina tatizo na CCM, nina tatizo na baadhi ya watu ambao wameamua kuacha kusema ukweli, wameamua kusema uongo kwa malengo na dhamira wanazozijua wao.
Hawa wataleta matatizo ndani ya CCM na hata katika serikali. Wamenichafua, hawakusema ukweli kuhusu mimi. Nitapamba, kuna vikao vyetu, nitasema ukweli kuhusu watu hawa. Nayasema haya ili Watanzania waelewe ukweli ulivyo. Si kwa sababu nataka kurudi katika uwaziri, alisema Karamagi.
Akizungumza kuhusu sababu za kampuni yake ya TICTS, inayohusika na kupakua kontena bandarini kuongezewa mkataba wa miaka 15 kabla ya ule kwanza kumalizika alisema muda uliongezwa kufuata taratibu.
Alisema kampuni yake iliomba kwa serikali kuongezewa muda huo baada ya kuonekana ulazima wa kupanua shughuli za bandari pamoja na kuongeza mtaji katika uwekezaji eneo hilo.
Alisema maombi hayo yalifanyiwa kazi na serikali likiwemo baraza la mawaziri ambalo baada ya kukubaliana na hali halisi liliielekeza Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma, PSRC kushaurina na TICS namna ya kuongeza mkataba huo kwa ajili ya kuboresha shughuli za bandari.
Kuhusu kutajwa kwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kuwa aliibeba TICS kuongeza mkabata huo wa miaka 15, alisema wakati kampuni hiyo ianongezewa muda hakuwa akifahamiana wala hakuwa na mahusiano ya aina yoyote na Mkapa.
Wakati Lowassa na Karamagi wakitoa kauli hizo za kujitetea kwa mara ya kwanza, wiki hii pia, mnajimu maarufu Sheikh Yahya Hussein alizungumzia kashfa hiyo ya Richmond akisema wahusika katika sakata hilo ndani ya serikali walikuwa ni wengi kuliko mawaziri watatu waliojiuzulu.
Katika hatua ambayo bado inaacha maswali mengi, Sheikh Yahya alisema alikuwa ana uhakika kuwa siku moja Lowassa atarejea katika madaraka ya kiserikali baada ya ukweli kamili kuhusu sakata hilo la Richmond kubainika.
Kauli hiyo ya Sheikh Yahya ilikuja siku chache tu baada ya Rais Kikwete kuwahutubia wazee wa Dar es Salaam na kueleza namna alivyoguswa, kushtushwa na tukio la kujiuzulu kwa Lowassa na kutajwa kwa watu wengine kadhaa ambao alisema amekuwa na uhusiano nao wa kijamaa na kikazi kwa miaka mingi.