Hivi JK hawezi kusoma nyakati????? hii nchi kweli itakuja kubadilika kweli?????
JF hureeeeeeeeeeee nimekuwa nikisikia tu, Asante Mwema na Manumba!!
Lowasa awe fair enough aruhusu na maswali itapendeza sana
Week end njema
Kwanza nianze kwa kuwapongeza hawa wenzetu waliofanikisha kurudisha mtando wetu hewani na nesema mwema na mafisadi wote walaaniwe daima.Lunyungu,
Mimi sishangai hata kidogo.Lowassa kupewa muda TVT maana yake ni kuwa JK amekubali. JK kukubali kujiuzulu kwa Lowassa ni kwa sababu alikuwa hana jinsi.Wale wote waliomsifu JK hawakuelewa kwamba JK hafanyi move kama hii ila kwa sababu ya kujisafisha ili approval ratings zipande, sasa zishapanda wanataka kuleta makida makida kwenye kuendesha serikali.
Ingekuwa inakera vya kutosha kama angestaafu bila kuchukuliwa sheria, sasa wanataka kumrudisha kwenye uongozi? Wakifanya hivyo watakuwa wametutukana Watanzania wote matusi ya nguoni.
Umahiri katika kazi hauji kwa watendaji kutaka tu, unakuja kwa watendaji kuwajibishwa na wananchi.Tuendelee kufuatilia kwa karibu na kuwawajibisha ipasavyo.
SAA TATU KAMILI USIKU WEWE SUBIRI WAKISEMA TUPIGE SIMU WAMEKWISHA NAKWAMBIA.lowassa atajuta kilichompeleka kuho tvtLunyungu hiyo press conference itakuwa saa ngapi?
Mwache tu Lowassa ajieleze,unajua kujisafisha kunaweza kuwa na matokeo ya aina mbili. Anaweza akajikuta badala ya kujisafisha ndio kajipaka ile mbaya.
Ndio maana ni muhimu mno kuwaruhusu watu waseme, kwani kwa kusema, ni rahisi kugundua pumba na mchele.
Ningependa kweli kusikia mahojiano hayo ya Lowassa. Ningelikuwa mimi mshauri wake, ningemwambia aende kwanza Monduli na kupumzika. Wahenga walisema ng'ombe akiumia malishoni, hujikokota zizini kusaidiwa, kwa yeye zizi lake ni kule Monduli. Huko ndiko kuna watu wanaoweza kumsamehe kwa makosa yote. Huku kwingine sisi tutamlima tu bila kumwangalia usoni.
Nina mashaka hii kitu si live mana nllibahatika jana kuona vijipande kwenye tvt akiwa anajitetea na kusema muda mwingi sasa atakuwa akichunga ng'ombe.Tusubiri mana kama si live watakuwa wameshaedit mambo mengine.
...Lowasa huenda akaenda Ubalozini...
Na Askofu KKKT haoni aibu..Naskia EL huwa anatoa fungu kubwa sana kanisani!