Lowassa anasafishwa!

Lowassa anasafishwa!

Mvua....atawapelekea wamasai wenzake wakati anachunga nao...hakuna cha mvua wala manyunyu hapo....

Msee K, ikiwezekana pungusa ukali ya maneno yako sidi ya jamii ya Kimasai, nafikiri mfua ni jambo muhimu kwa makabila yote!! Hiyo mfua ya Richmond hatuitaki huku lengai
 
Mvua....atawapelekea wamasai wenzake wakati anachunga nao...hakuna cha mvua wala manyunyu hapo....

Nimecheka sana na usiku huu mnene basi majirani watakuwa wamesikia ama kama kuna vibaka walikuwa wanataka kuja ndani wamejua niko macho .Duh!!

Wale wa maandamano ni njaa zao na njama za CCM .Umesikia kwamba kapokelewa na Viongozi wa Mkoa wa CCM sasa hapo ujue nini CCM inafanya juu yetu .Hadi sasa hawajasimamisha mkataba jamani sisi kweli ni Nchi ?
 
Lunyungu,

Lete habari zaidi. Ila jamani acheni kuwaita Wamasai wote Richmond. Hii ya kuadhibu Wamasai wote shauri ya kosa la mtu mmoja sio sahihi kabisa.

Waliomshauri wamekosea, angetulia kwanza kama miezi kabla ya kujitetea kwenye TV. Watanzania sasa bado tuna hasira za kutuibia, hata aseme nini, hatuwezi kumwamini.

Bila kujali katendewa haki au hapana, kujiuzulu kwake kwa scandal ni somo zuri mno kwa viongozi wa TZ na faida yake ni kubwa kuliko hasara chache
kwa Lowassa.

Muda wake umepita na sasa tuangalie hao walioingia madarakani.

Mbona Pinda sasa karibu wiki mbili na hatuoni hata strategies mpya za kuifanya Tanzania ipae?
 
hapo sasa naona iwe off limit na mambo ya kupakazia wamasia la sivyo mnatangaza vita humu na mada zote zitaharibika na ukabila,lakini uhuru wananchi kila kitu sawa ila ukijibiwa usikasirike na wewe
 
Lunyungu,

Lete habari zaidi. Ila jamani acheni kuwaita Wamasai wote Richmond. Hii ya kuadhibu Wamasai wote shauri ya kosa la mtu mmoja sio sahihi kabisa.

Waliomshauri wamekosea, angetulia kwanza kama miezi kabla ya kujitetea kwenye TV. Watanzania sasa bado tuna hasira za kutuibia, hata aseme nini, hatuwezi kumwamini.

Bila kujali katendewa haki au hapana, kujiuzulu kwake kwa scandal ni somo zuri mno kwa viongozi wa TZ na faida yake ni kubwa kuliko hasara chache
kwa Lowassa.
Mbona Pinda sasa karibu wiki mbili na hatuoni hata strategies mpya za kuifanya Tanzania ipae?


Mtanzania
The man was on a defensive side all the time and seeking merrcy from you guys.Amesema yeye si wa kulaumiwa ila Mwanasheria wa Sirikali na wengine walimpinga openly na hata waziri wa Nishati he refused to heed his call alipo m summon.Inaonekana kuna ujinga mwingi kule Ikulu lakini sisi tupo tutasema tu .

Muda wake umepita na sasa tuangalie hao walioingia madarakani
 
Wapi collective responsibility??......huyu kwa kweli anadiriki kuwaanika Chief Secretary, Mwanasheria Mkuu, katibu Mkuu Madini na Hazina kuwa eti niniiii????...........hivi hii ina tofauti gani na ile sababu aliyoitoa Bi Meghji kuwa “nilidanganywa”!!!!

Waziri Mkuu with all the Intelligence kuwepo at your disposal…….leo unakuja kutuletea eti ulishauriwa kuwa Richmond ni safi…………still you are the weakest link

Lowassa alijitetea kuwa, wakubwa hao wakaomba awape muda wa saa moja kupitia vipengele vya mkataba huo na baada ya hapo walikuja na maneno kuwa isingewezekana kuvunja mkataba huo kwani serikali ingepata hasara.

suala siyo kuvunja mkataba, suala ni the process ya ku-procure the company na uhalali wa hiyo kampuni kupewa zabuni……………ukishaingia Mkataba na kampuni iliyo fek i(alaah kumbe hata wewe mwenyewe ulijua kuwa Richmond ni feki)…..ndio tayari umeshaula wa CHUYA…..na kama ulijua kuwa Richmond ni feki kwanini usitumie your top most powers kama ulivyotumia kwa City Water….ulikuwa na uwezo wa kupima ushauri mzuri na ushauri mbovu as an individual in the first place……..bado sikuelewi………and still you are the weakest link!!!

"Niliona nisipoachia ngazi hali ya mambo katika chama changu ingekuwa mbaya. Napenda niweke jambo hili sawa kuwa sikuwajibika kwa sababu nilipata chochote Richmond.

Hayo ni yenu huko huko chamani…….ita has nothing to do with us as long as you have kept it as your secret!!

Well tunajua kwa sasa kutokana na kauli zako umetuthibitishia kuwa wafuatao inabidi wafuate Nyayo zako
Chief Secretary - Luhanjo,
PS Fedha - Mgonja,
PS Madini - Mwakapugi,
Mwanasheria Mkuu - Mwanyika

and ofcourse bila kumsahau DG wa PCCB Bw. Hosea + wale maofisa wote waliokuwepo kwenye hicho kikao cha ushauri ulichoitisha


Kwa upande wake, Askofu wa Dayosisi ya mkoani Arusha ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Thomas Laizer alitumia nafasi huyo kuwapiga vijembe wale wanaodhihaki kujiuzulu kwa Lowassa.
Ukuni ulioko kwenye kona usiucheke ukuni ulioko jikoni ukiungua kwa sababu nao unasubiri kuungua,
alisema Askofu Laizer bila kufafanua lakini akashangiliwa na mamia kwa maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Wewe Askofu…….please stay aside…………huu MZIKI (JF) huuwezi….ni mzito kweli kweli, tukiingia anga zako usije lalamika….maana ndioukuni huo huo unaosema……kwani itakuwa zamu yako kuungua
 
Ogah said:
Well tunajua kwa sasa kutokana na kauli zako umetuthibitishia kuwa wafuatao inabidi wafuate Nyayo zako
Chief Secretary - Luhanjo,
PS Fedha - Mgonja,
PS Madini - Mwakapugi,
Mwanasheria Mkuu - Mwanyika

and ofcourse bila kumsahau DG wa PCCB Bw. Hosea + wale maofisa wote waliokuwepo kwenye hicho kikao cha ushauri ulichoitisha


Katusaidia kututajia wengine, naona mpaka kila mtu akishamaliza kujitetea, serikali nzima itakuwa imeshahusishwa. Muda sio mrefu tutaambiwa hata rais, aliambiwa kuhusu RICHMOND kuwa fake na akakataa.
 
kwanini asikubali tuu Taifa limeingia hasara under his watch and take responsibility kuliko kuja na hizi unnecessary excuse...Mr former PM just say sorry and move on tutakuheshimu sana kuliko hizi spin unazojaribu!
 
Alipofika Jimboni kwake alikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwake na kupumzika kwa muda kisha alikwenda katika eneo aliloandaliwa kuhutubia huku akiwa ametandikiwa zulia jekundu kama viongozi wa kitaifa.


Ukisikia kupagawa ndio huku sasa....
 
Mvua....atawapelekea wamasai wenzake wakati anachunga nao...hakuna cha mvua wala manyunyu hapo....

Kishaju,

Hiyo juu haijapendeza. Ukabila tena ndugu yangu duh. Tupunguze hasira katika kujenga hoja na tufikishe ujumbe pasipo kuwaumiza wasiohusika.

Back to the Topic.
Ingependeza sana kama hayo mazungumzo ya Lowassa yangerushwa live na wananchi wakapewa nafasi ya kumuuliza maswali kwa kupiga simu studion ama popote alipokuwa wakati wa hayo mahojiano/Mazungumzo.
Aliyeandaa kipindi hiki sijui alikuwa na maana gani? Aliangalia upande mmoja tu wa shilingi?????????, Still, dunno.
 
Eeeeh Mwenyezi Mungu!!! Tulidhani ulituletea Mh. John Samuel Malecela, kwa ajili ya viongozi wote wajue nini maana ya uvumilivu kwenye siasa?

Kumbe wengine bado hawajajifunza kwa hili, pamoja na mja wako. Mh. Edward Ngoyai Lowassa???!!!

Mimi namuomba Mh. Edward Ngoyai Lowassa, akaongee na Mh. Malecela akafunzwe umuhimu wa kuwa na uvumilivu na subira!!!

Yale yaliyosemwa kwamba staili yako ya uongozi ni kweli,,, Mh. Lowassa unafanya mambo kwa pupa sana!!! angalia yafuatayoo...


1. Eti wataalamu waangalie mkataba kwa saa moja na kutoa uamuzi...
maana ya saa moja kwa watanzania... dakika 15 kusalimiana, dakika 15 vicheko,,,, dakika 15 kusoma, dakika 15 kuelewa bado ngapi tena... walahi kaka ulistahili kuondoka..

2. Kwa kweli ulitakiwa kuja kwetu after 6 month... lakini kwa sababu ya uongozi wako wa pupa tena,,, umeleta issue hii mapema mno... Nakuheshimu sana lakini ume-justify kwamba ulistahili kuondoka.

3. Wish you all the best kwenye kazi yako ya Ubunge wa Kudumu wa Monduli.
 
Nadhani mchango wake ungekuwa na maana zaidi angechangia bungeni akiwa kama mbunge wa kawaida.

Haya mambo ya kukimbilia vichochoroni ( Yes.. TvT ni kichochoroni ) hayamsaidii chochote kujisafisha.

Ili mtu ujisafishe kwanza unatakiwa utumie maji safi, vyombo/nyenzo safi, na mikono yako iwe safi. Lowassa huwezi kujisafisha kwa kutumia tope unajichafua zaidi, better remain quite unawatia machungu watu bure..
 
Mambo ni shida kwa kweli, iko kazi na kwa wale waliokuwa wakifuatilia ili sakata la Richmond naomba mjaribu kufuatilia tangu miezi ya nyuma kuna uwezekano ukakuta hawa jamaa wanajichanganya...sasa inaonyesha kwamba anasema yeye alishutukia hii richmond. wakati huo kuna kipndi walikuwa wakitetea...hivyo kuna siri kubwa ambazo zimejificha juu ya ili. Na sasa wataanza kuumbuana wao wenyewe...
 
kwanini asikubali tuu Taifa limeingia hasara under his watch and take responsibility kuliko kuja na hizi unnecessary excuse...Mr former PM just say sorry and move on tutakuheshimu sana kuliko hizi spin unazojaribu!

Precisely Koba

....the former PM Lowassa need not to move around to spin........ni bora akanyamaza kama mwenzie Sumaye.....thats my advise
 
Kweli siasa ina wenyewe:

Tangu sakata la Richmond lipasukie bungeni mpaka sasahivi hakuna mahali popote kwa namna yeyote JK ameonyesha hata by implication kuwa EL ana "DOSARI" yeyote ya Kiutendaji kwenye nafasi aliyokuwa nayo!

Ukimsikiliza EL anacheza exactly ngoma ile ile ya JK. Ni mtakatifu isipkuwa watendaji wengine!

Utafikiri hawa watu wawili ni mapacha wa kuzaliwa katika kucheza na fani ya siasa.

Kwao wote ni kama wameshikilia "UTAKATIFU MKUBWA" na kila mara kwa namna tofauti ni kutafuta maneno na media mabalimbali kujustfy UTAKATIFU WA MATENDO NA MIOYO YAO!

Hakikia kuna kazi nzito.

Furaha na bahati yetu ni kuwa NYAKATI ziko upande wetu. Furaha zaidi ni kuwa they are completely blind to the game they r trying to play.

They have to stop IT very soon!

Na ninafikiri God Loves them Na atawatumia malaika kuwahabarisha kuwa TZ wanayoishi sio "ILE"

We hope they will behave!
 
Hii kauli "sijala hata senti tano" inadhihirisha jambo moja kuwa huwa anakula ktk madeal mbalimbali lakini hili jamani waliokula wengine...

The Verdict: Kwa kauli hiyo unathibitisha beyond reasonable doubt kuwa Mh saaaa Ngoyai ni MWIZI by implication, tulia huko Monduli ubunye mihela yako...
 
Kishaju,

Hiyo juu haijapendeza. Ukabila tena ndugu yangu duh. Tupunguze hasira katika kujenga hoja na tufikishe ujumbe pasipo kuwaumiza wasiohusika.


oooh samahani sana....kwa kweli sikuwa na nia mbaya na kosa kama ilo halitajitokeza sana....samahani kwa wote ambao wameguswa moja kwa moja...na ninaapa kwamba kosa kama ili ili halitatokea tena maana mafisadi wanatoka pande zote za Tanzania,,,

Ima, imaaaaaaaaa... tuijenge Tanzania isiyokuwa na mafisadi ifikapo 2025...
 
Duh jamaa mi sikumwelewa anaongea nini pale, na niliwaambia ile kitu si live mana hata yeye anajua wananchi wana hasira naye. yani tulijiandaa na simu ana bahati sana huyu baba yeye anadhani anaweza kubaili mawazo ya watanzania kw sasa?na hao waliompokea nina mashaka ufisadi uliwapitia, mtz mwenye akili hawezi kwenda pale. wewe kiongozo wa ccm [mkoa unampokea kamanani kwa kweli sipati jibu na hao waliotandika red carpet sijui wamedata au?yetu macho ila 2010 si mbali watanzania tutachagua tunayeona atafaa.Ati kamati haikumtendea haki,alitaka aulizwe nini wakati alikubali yote yatokee chini yake.halafu anasema ndege ya tz inapaa?sasa imeanguka naye na asubiri hata huo ubunge atakosa mana original wamasai wataamua wanamtaka nani kati yake na sokoine
 
Lowasa anasema alijua kwamba RDC ni matapeli .Anasema kajiondoa Ukuu kwa ajil ya wadogo .Anasema wanasheria wote walimweleza kwamba mkataba na RDC was perfect.Luhanjo na wengine waliitwa akawaambia lakini wakasema kisheria hatuwezi kuvunja mkataba .Fuatilia .

Kasheshe

kwa CS kusema the contract was perfect!!!.........pia kumbuka uchunguzi wa tume ulivyotaarifu......nachelea kusema kama tuna CS makini, ilikuwa ni rahisi sana kwa CS kutambua kuwa mkataba ule una matatizo kibao kama yalivyoainishwa na tume ya Mwakyembe.

....hivi kweli mtu unaingia mkataba na kampuni isiyona uwezo kabisa na ikajulikna hivyo mapaka Government ikatoa LoC..........ni kitu gani hapo ambacho CS hajui kuwa ni mkataba wa hovyo

ktk any Contract kuna kipengele cha "determination".........hilo neno PERFECT lina uzito sana kutoka kwa mtu kama CS kwenda kwa PM.......tena pengine hawa ndio waliompa JEURI Lowassa kushinikiza hii kampuni iendelee

tuendelee kujadili
 
Back
Top Bottom