Katika kuonyesha kama haiamini tena timu anayoambatana nayo au anataka mtu wa kumsaidia kuongea zaidi na kufafanua kwa ufasaha, Lowassa amemuomba Mbowe waandamane naye kwenye mikutano yake yote iliyobaki ya kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Lowassa alitoa ombi maalum kwa Mbowe wakati wa kikao maalum cha kutafakari hali ya kampeni na mwerekeo wake.
Lowassa alimsihi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuendelea kuambatana naye kwenye kampeni ili aongeze nguvu kwenye timu yake.
Lowassa alisisitiza na kusema Mbowe anaweza kufanya kampeni zake kwenye Jimbo la Hai na pia kuweka timu ambayo itamsaidia wakati atakapokuwa nje ya jimbo kumpigia kampeni mgombea urais.
Wataalam wa siasa wanabaki na maswali mengi hasa ikichukuliwa uwezo wa Lowassa katika kutoa hotuba na kujieleza kwa wananchi ni mdogo achilia mbali afya yake. Ikumbukwe, Lowassa mara nyingi amekuwa hachukui zaidi ya dakika tano katika hotuba zake.
Lowassa amekuwa akiambatana mara nyingi kwenye mikutano ya kampeni na kundi lake ambalo lilimfuata CHADEMA kutoka CCM. Hawa ni pamoja na Sumaye, Mgeja, Masha na Goodluck Ole Medeye.
Is this Twaweza and Synovate opinion polls psychological effect?
Is Lowassa and his inept team have pushed the panic button?