Lowassa amuomba Mbowe amsaidie kwenye kampeni!

Lowassa amuomba Mbowe amsaidie kwenye kampeni!

Nilimkataa Lowassa akiwa CCM, ninaendelea kumkataa akiwa nje ya CCM.

Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania achilia mbali udhoofu wake kifikra na kiafya.

Ninapenda bunge liwe na wabunge wengi wa upinzani ili bunge lisiwe rubber stamp na lifanye kazi yake kamili ya kutunga sheria na kuisimamia kikamilifu serikali ya Magufuli.

Kura yangu itakuwa ni moja ya kura zitakazozuia Lowassa kuwa Rais wa Tanzania.

I can’t let our beautiful country go to the dogs!

Upo sawa sawa mkuu
 
Timu ya kampeni inayoambatana na Lowassa
1. Sumaye
2. Ole Medeye
3. John Mrema
4. Mmoja wapo kati ya Mbowe au Lissu (baadhi ya mikutano hawapo kabisa)
5. Mbunge wa jimbo husika kunakofanyika kampeni

Timu ya kampeni inayoambatana na Magufuli
1. Bulembo
2. Kibajaji
3. Mwigulu
4. Makamba Senior
5. Makamba junior
6. Diamond planumz
7. Yamoto band
8. Steve Nyerere
9. Makongoro Nyerere
10. Mkapa (sometimes)
11. Kikwete (sometimes)
12. Wengine wakiwemo kina Warioba, Kinana, nk nk nk nk nk

Hivi kati ya hao wawili ni nani anasaidiwa kuelezea ilani?
Hoja yako ni nini?

Magufuli anahutubia siyo chini ya saa moja wakati Lowassa anatumia mara nyingi katika hotuba zake chini ya dakika tano.
 
Nina wasiwasi na source ya hii taarifa!!!
Na hasa ukizingatia The author (MsemajiUkweli) is the first commenter of his/ her own post!!!
 
Unapost mwenyewe na unakuwa mchangiaji wa kwanza kwenye post yako....unajitekenya na unakuwa wa kwanza kucheka mwenyewe!!!!!!

Tulieni.........
 
Ukitaka kujua CCM haifai hata kwa nukta moja angalia

1. Wanaotegemewa kuwa viongozi ni mafisadi
2. Mfumo wote wa kifisadi

Watu wanaomkataa Lowassa nu kuyarudia matapishi ya CCM wanahitaji ushauri nasaha

Lembu, hebu soma tena maandishi yako na utafakari upya!
Unamzungumzia Lowasa au Magufuli?
 
Niliposoma post ya kwanza nikajua MsemajiUkweli ni bonge la great thinker. Ghafla, naona post yake ya pili (mara tu baada ya kupost) akidhihirisha unazi wake.

Well, the country is already in the dirty hands of the dogs. Voting for Magufuri will further aggravate the matter
 
Ccm bila kuongelea lowassa hawapati usingizi lowassa alipo tupo
 
nakumbuka kutoa pendekezo mapema tu kuwa kama lissu na mbowe wanaamini kabisa katika ushindi wa lowassa walitakiwa waachilie majimbo yao kwa wanachadema wengine ili wao waongoze kampeni ya lowassa. Kwa vile wanauhakika atashinda urais basi angeweza kuja kuwateua zile nafasi kumi na hivyo wangeendelea kuwa wabunge... Bahati mbaya sasa hivi wana ccm wanaendesha kampeni zote mbili za magufuli na ya lowassa.. Think about it!
mzee mwanakijiji kila jambo na wakati wake wakati wako umekwisha huwezi tena kuwa na jipya tunaloweza kulisikiliza ambalo hatujalisikia mbowe akiteuliwa anaweza kuwa waziri mkuu kwa katiba ya nchi yetu!??
mzee umezeeka vibaya sana muombe mungu unaweza kuja changanyiwa ukaokota makopo!!!!!
 
Lowasa tunampenda ila tukienda mbali zaidi tutakula hasara juu ya mtu huyu,ukiachia afya yake lowasa atakapokua rais atachukua muda mwingi kulipa fadhila kwa wadau mbalimbali,kitu hiki ndicho pia kilichomponza kikwete.

Acha usanii.
 
Katika kuonyesha kama haiamini tena timu anayoambatana nayo au anataka mtu wa kumsaidia kuongea zaidi na kufafanua kwa ufasaha, Lowassa amemuomba Mbowe waandamane naye kwenye mikutano yake yote iliyobaki ya kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Lowassa alitoa ombi maalum kwa Mbowe wakati wa kikao maalum cha kutafakari hali ya kampeni na mwerekeo wake.

Lowassa alimsihi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuendelea kuambatana naye kwenye kampeni ili aongeze nguvu kwenye timu yake.

Lowassa alisisitiza na kusema Mbowe anaweza kufanya kampeni zake kwenye Jimbo la Hai na pia kuweka timu ambayo itamsaidia wakati atakapokuwa nje ya jimbo kumpigia kampeni mgombea urais.

Wataalam wa siasa wanabaki na maswali mengi hasa ikichukuliwa uwezo wa Lowassa katika kutoa hotuba na kujieleza kwa wananchi ni mdogo achilia mbali afya yake. Ikumbukwe, Lowassa mara nyingi amekuwa hachukui zaidi ya dakika tano katika hotuba zake.

Lowassa amekuwa akiambatana mara nyingi kwenye mikutano ya kampeni na kundi lake ambalo lilimfuata CHADEMA kutoka CCM. Hawa ni pamoja na Sumaye, Mgeja, Masha na Goodluck Ole Medeye.

Is this Twaweza and Synovate opinion polls psychological effect?

Is Lowassa and his inept team have pushed the panic button?
Tulia hapo hapo dawa iingie utapona tu mamaaa
 
Nilimkataa Lowassa akiwa CCM, ninaendelea kumkataa akiwa nje ya CCM.

Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania achilia mbali udhoofu wake kifikra na kiafya.

Ninapenda bunge liwe na wabunge wengi wa upinzani ili bunge lisiwe rubber stamp na lifanye kazi yake kamili ya kutunga sheria na kuisimamia kikamilifu serikali ya Magufuli.

Kura yangu itakuwa ni moja ya kura zitakazozuia Lowassa kuwa Rais wa Tanzania.

I can’t let our beautiful country go to the dogs!
Tupo wengi wenye msimamo kama wako..Pia huwaga nawasifu Wahariri wa Raia Mwema na Raia Tanzania hawakumkubali Lowassa akiwa ccm na hata alipohamia cdm bado hawamkubali kwa vigezo vilevile ila wengine ni waganga njaa...bendera kufuata upepo
 
mzee mwanakijiji kila jambo na wakati wake wakati wako umekwisha huwezi tena kuwa na jipya tunaloweza kulisikiliza ambalo hatujalisikia mbowe akiteuliwa anaweza kuwa waziri mkuu kwa katiba ya nchi yetu!??
mzee umezeeka vibaya sana muombe mungu unaweza kuja changanyiwa ukaokota makopo!!!!!

Utakuja kumuelewa mzee Baada ya uchaguzi... Maana uelewa wako ni mdogo sana kiasi cha kukufanya uelewe hivi sasa
 
haya mambo yako tanzania tu wametukosea sana hawa ccm muda wa kuwatia adabu ni huu ndio maana wanatumia nguvu nyingi kupiga kampeni tumewapa miaka 50 wamelala tu zamu ya wengine kuongoza wao ni nani?
We kweli nyumbu hujaona tatizo nini..?Tatizo hata huyo mnaetaka atuongoze amekaa CCM miaka 50 sasa mnatuambiaje kama kuna mabadiliko...?jiongeze bhana
 
Back
Top Bottom