LOWASA ALICHAFUKA WAPI WAPI MPAKA ASAFISHWE?
Nilisoma uzushi mkubwa katika moja kati ya magazeti yatolewayo mara moja kwa wiki siku chache zilizopita.
Pamja na mambo mengine, gazeti hilo liliorodhesha viongozi kadhaa wa CCM na serikali wakiwemo mawaziri, naibu mawaziri na wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa (NEC) ya chama cha Mapinduzi.
Katika orodha hiyo ya wajumbe wa NEC wamo wenyeviti na makatibu wa CCM wa baadhi ya mikoa nchini.
Kilichopotoshwa na gazeti hilo ni madai kuwa eti aliyekuwa waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Edward Lowassa ambaye alijiuzulu wadhifa huo mapema mwaka huu anasafishwa na viongozi hao kutokana na kile kinachodaiwa eti alihusika na mkataba wenye utata wa kampuni ya Richmond na serikali kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura mwaka 2006.
Wazushi wanajaribu kupotosha kwa kadri wawezavyo kuhakikisha kuwa ionekane Lowaqssa alifanya ufisadi katika suala hilo ingawa wanafafahamu ukweli kwamba hakuhusika hata kidogo.
Hata kujiuzulu kwake kutoka katika nafasi aliyokuwa nayo ni hatua ya kisiasa inayoweza tu kufanywa na viongozi wanatanguliza mbele maslahui ya nchi badala ya maslahi yao wenyewe.
Kama angekuwa na maslahi binafsi katika mkataba huo kamwe asingetaka kuuvunja mara mbili na kukataliwa na wanasheria, badala yake angejitahidi kuutetea kwa nguvu zote.
Kwa hiyo, ni uzushi uliovuka mpaka na pia ni uongo mkubwa kudai eti Lowassa anasafishwa wakati hajachafuka chochote.