Yanayotokea Mtwara na muendelezo wake kwa muda mrefu sasa ni dalili kuwa hakuna link effective kati ya wananchi wa sehemu hiyo na serikali ikiwakilishwa na vyama vya siasa yaani chama tawala na vya upinzani. Huu ubishi wa Mtwara na Lindi hata kama unachochewa na watu wenye malengo yao, kitendo cha kushindwa kutengeneza forum ya maridhiano kama watanzania, si ishara nzuri. Kama watanzania tumekosea wapi? na chama tawala na serikali vimekosea wapi? Itisheni mijadala na wadau halisi wa swala hili tusiadhirike na tusiathirike kwani fujo zilizopo wakati serikali tayari ina makubaliano na mikataba ya fedha nyingi inaweza kuleta vita na mauaji makubwa na kulitia doa taifa letu kwa kuwa na civil war kwa mara ya kwanza, baad ya uhuru. Sitaku ku-speculate lakini kuna mtu au watu wenye akili kubwa, malengo makubwa na wenye kuaminika katika dola hii ambao wana abuse knowledge au information kuhusu hizi project za gesi na wameamua kumwaga sijui mboga au ugali. Tujiangalie sana. Kama zilivyo nchi nyingine kulikowahi kutokea ma-dictator wa ajabu, tuna watu wabaya sana nchi hii na baadhi yao huenda wana miss vitu au muda mchache sana kuchukua au kuuza nchi hivyo tuwe makini. Hii siyo bure.