Kwa hiyo brother, wewe na shetani mmezaliwa tumbo moja au ?Usicheze na kahama na kahama kuna matajiri alafu wenye roho za ajabu? Pili, huyu dada alikuwa mapepe? Tatu, kabla ya kwenda kibaha alifukuzwa kwa sababu za kiofisi ijulikani ni utovu au mengine kiofisi. Nne hakuwa na cheo hiko ni Afisa mikopo.
Tano, matukio ya kahama kesi za kufanyiana unyama zipo sana sio mapenzi, sio biashara na n.k. Uzuri wa huyu dada inaonyesha alikimbia kuofia vitisho kwa mwanamke mwenzake au mapenzi?
Nakuongezea na moja!Hawa wanaonunua simu mpya kariakoo, wanasajili na line mpya za voda wanajua hawatofahamika! Wanasahau kuna operation ya simu feki ilipita nchi nzima, wanasahau kwenda congo au msumbiji kununua simu ambazo imei zake haziwezi kua traced halafu waende congo au Rwanda kusajili line za tigo au airtel ili mawasiliano kwanza kutafutwa mtu asumbuke, wahalifu wa nchi maskini huacha alama kizembe sana ndio maana hukamatwa kama kuku
Kesi itakua wapi?? Kibaha/Dsm/ Kahama??Hii kesi ni tamu kama ile ya annate msuya asee
Nitahudhuria hata mahakamani niisikilize nikiwa na muda
Mawasiliano yao ni Whatsapp na Telegram tu! No video call, no voice call no sms charts!.....Nakuongezea na moja!
Hata IMEI za simh hua zinapigwa nyundo! Wanabadili IMEI kama ni kwenye 5, wanaweka nane!
Line ya simu anasajiri kwa jina la mtu mwingine kabisa, vijana wenye njaa, ukimpa 50,000 ukamwambia sina namba za NIDA naomba nisajirie kwa jina lako anakubali, kumbe anaenda kusaidia mharifu!
Wahalifu wengi huchora tukio hata zaidi ya mwaka!
Mawasiliano yao ni Whatsapp na Telegram tu! No video call, no voice call no sms charts!
Anaweza zima simu siku mbili,na akizimia simu Dar anakuja washa akiwa Dodoma!
Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
End to end encryptionMawasiliano yao ni Whatsapp na Telegram tu! No video call, no voice call no sms charts!.....
Kwenye WhatsApp wanatumia njia ipi??
Kiongozi naona wewe ndo Mchunguzi umeleta humu ili watu wafunguke upate pa kuanziaFamilia iko kwenye msiba mzito. Tunawapa pole. Ni kifo kinachotokana na mauaji hivyo hakiwezi kukosa mijadala na msingi wa hiki kifo cha mauaji lazima kiwe na sababu, kiwe na viashiria.
Kiwe na mhusika/wahusika wakuu
Kiwe na bajeti
Kiwe na watendaji/watimiza lengo. Kwa msingi huu wauaji
Kiwe na mpango kazi
Kiwe na fool proof
Kusiwe na dosari kuanzia kupanga, kutekeleza na hatimaye kutawanyika na kumalizana kama kuna malipo ya mwisho yalikuwa bado
Uchunguzi wa kifo hiki ni rahisi sana na si chini ya watu 20 wanaweza kuhusishwa nacho, ambapo watachujwa mpaka watabaki si chini ya watano .. Na ni uchunguzi rahisi kutokana na makosa mengi waliyofanya wauaji.. Hawakuwa wajuzi maana wajuzi huwa hawaachi alama! Japo kuna kosa moja dogo sana hufanya na kufumua mpango wote.
Uchunguzi wake utaanzia kazini kwake, maisha yake nje ya kazi, marafiki zake, wateja wake, mishe na dili zake, mawasiliano yake pamoja na mahusiano.. Hapa ni kwa ajili ya ku 'establish' Msingi wa kesi na 'motive' ya muuaji/wauaji.
Uchunguzi wa pili ni eneo lilikofanyika tukio.. Pori la Mitamba linalosifika kwa matukio ya mauaji, Mitamba halina tofauti sana na Mabwepande na kama linaweza kuchunguzwa vizuri kuna maiti ngingi mule zinaweza kuwa zimezikwa.
Mitamba liko Kibaha njia ya kwenda Bagamoyo eneo linaitwa Pangani.. Sehemu kubwa ya pori la Mitamba ni eneo la wizara ya mifugo na uvuvi na kuna kipindi matapeli wa viwanja Kibaha walilivamia na kuwauzia watu viwanja mpaka serikali ikaingilia kati.
Marehemu ni mkazi mwenyeji wa Kibaha Kwambonde kakulia hapo, kosoma Tumbi nknk. Wazazi wake wanaishi hapo mpaka sasa na ni watu unaoweza kuwaita maarufu eneo hilo na hata kanisani kwao Tumbi. Kwanini muuaji/wauaji wakachagua kuja kummaliza 'nyumbani kwao'?
Marehemu alisafiri salama salimini toka kituo chake cha kazi Shinyanga mpaka nyumbani Kwambonde Kibaha. Pengine alitumia ndege, usafiri binafsi au wa jumuiya lakini alifika salama.
Je, wauaji walikuwa wanamfuatilia kote huko?
Je, wauaji ndio walimuita aje Kibaha?
Je, lengo lake la kuja nyumbani Kibaha lilikuwa ninini?
Je, mpango wa kummaliza Kibaha pori la Mitamba ulikuwa mpango plan A au B?
Marehemu siku ya tukio alikuwa kanisani na ndugu zake.. Ni wazi alipata wito wa kuitwa nje mara moja ama kwa ishara ya mtu alikuwa ndani ya kanisa ama kwa simu kwakuwa mikoba yake aliacha alipokuwa kaketi. Hakurudi!
Ni wazi walimuita walikuwa nje kabisa ya kanisa barabarani! Kanisa la KKKT Tumbi liko pembezoni mwa barabara ya kuelekea Tumbi hospital. Ni wazi kulikuwa na gari ambalo ama alipanda kwa hiari ama kwa lazima/Kutekwa.
Ni wazi safari ilianza kuelekea Pangani pori la Mitamba.. Macho ya marehemu yata 'reveal' kilichotokea ndani ya gari kwa hicho kipindi chote mpaka kufika Mitamba kumwagiwa Petrol na kuchomwa moto!
Ukurasa wa pili juu ya mpango kazi ambao ninaamini ndio plan A.
Wauaji waliona eneo salama la kummaliza ni eneo la nyumbani alikozaliwa. Wauaji ni wenyeji wa Kibaha wanaofahamu vema jiografia ya Kibaha hasa eneo la Mitamba Pangani ambako hakuna doria za polisi, kuko kimya na mbali na makazi ya watu. Pia ni eneo lenye gate away nzuri kwahiyo ni rahisi kupoteza maboya mtu anayekufuatilia.
Unaweza kutokea Kimara
Unaweza kutokea Baobab
Unaweza kutokea Kibaha maili moja eneo la shell
Unaweza kutokea NIDA
Unaweza kutokea picha ya Ndege
Unaweza kutokea Loliondo nk na kote huko mtu asijue umetokea Mitamba Pangani
Kwa vyovyote mwenye mpango wake alikodi watu wa kumsaidia kuutimiza
Loose ends/makosa ya kiutendaji yasiyotarajiwa
- Dereva
- Mfuatiliaji aliyekuwa kanisani
- Mtu aliyempatia sindano ya sumu
- Backup
- Hapa kuna watu wa kati hawakosekani
- Malazi, kama watekeleza mpango walitoka mbali ni wazi walilala gesti za maeneo ya Kibaha ama jirani na Kibaha.
Wajuzi hufanya rehearsal hata zaidi ya mara tano kutegemeana na mlengwa na bajeti na kila rehearsal hugundua makosa kadhaa na kuyarekrbisha.
Je, makosa makubwa kwenye hili tukio ni yapi?
1. Mtandao wa mawasiliano simu na jumbe za sauti na maneno
2. Kuhusisha watu zaidi ya mmoja
3. Kutochagua wajuzi wa kazi
4. Kutofanya rehearsal
5. Kumchoma sindano ambayo haikuwa na sumu kali au ambayo haikuchomwa kwa usahihi
6. Kudhani amekwisha kufa hivyo kutengeneza fool proof ya kumchoma moto uliomzindua
7. Pengine kuondoka eneo la tukio haraka bila kuhakikisha ameungua vizuri
8. Macho kubaki salama, yalirekodi kila kitu
Kwa dondoo hizo hii kesi ni nyepesi kuliko ya bilionea Msuya ana yule mzungu wa tembo. Marehemu alibaki kuwa hai kuanzia tarehe 3 march mpaka 9 alipoaga dunia. Siku sita ni nyingi sana kuweza kupata na kujua mengi
Damu ya mtu ni nzito na inanuka! Harufu hukoma haki ikitendeka![]()
Yetu macho Mark my word'sHii nayo kwa wabobevu ni rahisi mno. Line ya simu inakupa IMEI namba na inapokuwa mahali simu ikiwa on unajichorea ramani ya matembezi yako. Kifupi utakamatwa. Sisemi mengi bgoja niishie hapo. Hawa wauaji kama alivyosema Mshana Jr watakamatwa kama kuku. Tena familia ina pesa na ndugu zake wana pesa yaani mkate ngumu mbele ya chai hakuna. Tena itakuwa na high level investigation. Mark my words.
Una HOJA usikilizweMi nadhani ni uzushi, sudhani kama watekelezaji wa tukio wanaweza kuchukua riski kubwa namna hii eti kutumia wafanyakazi wenzake ilhali wanajua itakua rahisi kutrace unless kama watu wameiga sauti ya mfanyakazi mwenzake kama alivyosema baba yake kwamba mtu anaweza kuiga sauti akajifanya ni boyfriend wako
Upo sawa wengi hawana uelewaHizi ni story za kijiweni, sidhani kama kuna ofisi inafanya kazi kizembe namna hii
alikuwa mpambanaji has a lot to do na tabia zake. Wanawake wengi wapambanaji wana ile aptitude ya "Getting it regardless" na "Wacha iwe mbaya tu"umeongea ukweli mtupu mkuu. Na hii tabia imewagharimu wadada wengi wa kichaga.
Wewe ni Bush lawyer?Uko sahihi Mkuu Mshana Jr . Damu ni nzito, damu inalia, damu inanena. Wauaji hata wavuke mipaka watakamatwa tu. Wameambiwa wakurudi msibani watakuta mambo mengi yamefukunyuliwa. Baba atahakikisha haki ya Binti haipotei. Binti anazo biashara na Baba ana uwezo. Upelelezi itafanyika wa nguvu kabisa. Hii kesi itakuwa na public interest. Ingekuwa DSM hapa ningehudhuria kabisa. Hivi Kibaha kina High court section? Wailete DSM.
Thus makes sense hapa jamaa walikua wanajua wenzie wanaenda wakatumia nafasi hyo hyo..Wauaji hawawezi kufanya makosa ya kijinga ya kuacha trace wazi wazi namna hiyo ,watu wasichokijua ,wahalifu wana mbinu nyingi sana za kuwapoteza vyombo vya dola....Ni rahisi sana kuwapoteza askari kwa kutumia simu na kwa jinsi wasivyodig deep muhalifu anaweza akawingiza choo cha kike wakaenda kumkamata mtu siyo.(watu wa cyber wanajua hili ,siwezi kuweka wazi mbinu hii).
Kuna softwares/service kibao kwenye simu zinazoweza kubadili sauti ,kuna magic voice ,kuna software za kuitune sauti ifanane na mtu flani ,akikupigia unasikia kabisa sauti yake ,kuna software ukipigiwa inakuja namba ya mtu wako wa karibu kabisa ambapo umasave jina lake ila hapigi yeye.
Si rahisi wafanyakazi wenzake wenye motive ya kumuua wampigie simu kwamba wanakuja kumsalimia maybe a coincidence or muhalifu alitumia mwanya huo baada ya kusikia kwamba wafanyakazi wenzake wanakuja naye akatumia loophole hiyo hiyo kufanya yake.
Elon Musk akiwa twiter.Hili suala la hiki kifo kinanikumbusha mbali sana.Kuna swaiba wangu alisomesha pisi moja ualimu. Pia akaitafutia kazi ...imepata kazi tu ikamtema mshikaji.
Kama isngekua sisi kulikua na mawili ni jamaa kumpoteza ama ile pisi kali kupotea. Hapa ndo niliona faida ya marafiki wa ukweli maana tulishikana kumshauli jamaa japo ilikua ni ngumu lakini tulifanikiwa jamaa akakaa sawa ila jamaaa alikua kaingia unyama wa hali ya juu maana ilibidi tuwe tunamlinda km Elon Musk akiwa twiter.
Jamani utapeli wa mapenzi ama dhuluma tuache tunapo ona haya yawe fundisho kwetu.
za kutoa makafala. Ukila bila utaratibu unatolewa sadakaNa wengine hela zao ni za kutoa makafala. Ukila bila utaratibu unatolewa sadaka
Ushamba Amna cheque ya billion 1 acha ushambaNukuu kutoka chanzo kisicho halisi:
Inasemekana alinayehisishwa na kifo chake ni Boss wake …
Aliaambiwa afoji check ya 1B isemekane imeandikwa kimakosa ili hiyo hela isionekane Bank .. Lakin Binti alikataa..
Boss alimsumbua akakosa amani akaomba ruhusa kuja Kibaha kuisalimia familia yake .. Lakin alikuwa akiwasiliana na Mchumba wake nakumpa taarifa hizo..
Alipokuja Kibaha alimshirikisha Baba yake Mzazi ambaye ni Doctor Mkuu Mwimbili Dar. Siku chache kurudi nyumban Boss wake alimpigia Baba yake huyo Binti kumtaka amwambie mwanaye aache kazi ndani ya masaa 24 . Baba ake akahoji kwakosa gani mwanangu alilolifanya?
Lakin siku ya pili alipigiwa simu na mmoja wa wafanyakazi wenzake Kahama kumjulisha wamekuja Dar kikazi wanapita kibaha wamsalimie… According to that .. Alipokea simu kwamba wamefika wakutane alipotoka ndyo hakurudi tena ..
Kupelekwa porini na kuchomwa moto na sindano za sumu .. Alijitahidi kujikongoja mpka eneo la makazi ya watu .. Nakuonba msaada apigiwe simu Baba ake .. Toka hapo alikata kauli na kukimbizwa Mwimbili.. na siku chache kuaga dunia..
Inasemekana Boss wake ameshakamatwa sheria itafata mkondo wake ..
Mungu ailaze roho ya marehemu Martha.
Mwisho wa Nukuuu.
Upo sawa unahojaHizi Ni speculations, na inawezekana waliohusika ndio wanaeneza hizi propaganda. Sasa Kama aliambiwa afoji cheque kwanini hakwenda polisi.
Yupo sawaHuyu jamaa ni fara sana utamsema marehemu alikuwa hajatulia kama ni ndugu yako unaweza kusema hivyo