Liyumba afungwa miaka 2 jela

Liyumba afungwa miaka 2 jela

This is the JOke J .e .k.e.i unatutania hapa kuna mkono wako watanzania huwatendei haki
hapa unaruhusu watu washike sheria mkononi
Deus (Jasusi Mafia) out
Zombe out
Next Mramba no case yona no case
EPA case zinafutwa
Hili ni chenga la macho TANZANIA TANZANIA NCHI YANGU
 
ni kweli ameonewa, na atakata rufaa, na itasikilizwa baada ya miaka 3 mingine, maana amepewa siku 90 za kukata rufaa, mjibu rufaa naye anapewa siku 90 za kujibu rufaa. Msajili anazo ziku 90 kuipangia siku ya kuisikiliza, hakimu naye ana toa siku 90 za kujiridhisha. Halafu siku 90 za kufanya final submission na siku 90 za mwisho za kusoma hukumu!, jumla ni miaka 3!.

Yeah akifanya hivyo wkt huo anakuwa tayari yupo nje na mahakama ya rufaa inamsafisha kuwa alionewa na uchaguzi mkuu wa 2015 atachukua formu kwa kupitia CCM kugombea ubunge au urais ataingia bungeni ulaji unaendelea kama kawaida.
 
Kisheria ni tayari ameshatumikia miaka miwili mpaka sasa...hivyo si ajabu akatoka....akina dada mpoooo???
 
Nini kigezo cha kusema "ndogo sana jamani" . Kuna watu wanatumia magari ya serikali kubebea majani ya ng'ombe, kuna wengine wanatumia hela za serikali na kutofanya kazi inayotakiwa au iliyoainishwa, wengine wanachukua imprest au per diem hawaendi, kuna tofauti gani na huyu bwana ambaye jengo lipo na linaonekana kwa nini useme muda ni mdogo.

Tuanze kutoa boriti kwenye macho yetu, huyu hana tofauti yoyote na watanzania wengi walio maofisini.

...utawaweza wadanganyika?
Weshasahau na tena wanasubiria kuwapigia kura 'Mapapa na Manyangumi' wanaotuhumiwaiwa kwa maskendeli ya mikataba feki ya madini, kesi ya Radar, wizi wa EPA na Richmond....wanamshikia bango 'kidagaa!'
 
Hivi kweli watu mlitegemea hukumu tofauti na hii...au hamkufuatilia kesi nzima.
Ni lini mtashtuka na kuuvua Udanganyika!.
 
Kama ndio hivyo basi kesi za trafiki tungeenda jela wote. Kama kifungu cha adhabu kinatanguliza faini na kifungo baadaye ni vyema wakati wa kuhukumu hakimu aanze kama ambavyo watunga sheria wamesema. Kama bunge lingeona kosa hilo ni kubwa kustahili kifungo basi wasingeweka faini wangetanguliza kifungo tu moja kwa moja. Ndo maana awali nilisema mushkeli upo katika adhabu aliyopewa mshtakiwa na inaweza kuwa sababu kupewa dhamana wakati anasubiri rufaa yake kusikilizwa.

Lakini hapa hakimu katoa adhabu kubwa What is Tshs. 5,000,000 kwa Liyumba?. Hii sheria itakuwa haitendi haki pale Liyumba au wale mapapa wa ufisadi watakapopewa adhabu sawa na aliyekamatwa na rushwa ya shs. 10,000 tena hawa hupewa both na maelezo "Liwe fundisho kwa wengine".
 
Ndo maana yake, lakini atatoka na msamaha wa rais kabla ya mwisho wa mwaka huu
..Huyo xmas atakuwa uraiani kama kawaida maana kwenye ile sikukuu ya kusheherekea miaka 49 ya uhuru lazima JK ampe msamaha tu...Ndio njii yetu ya wadanganyika!
 
Nini kigezo cha kusema "ndogo sana jamani" . Kuna watu wanatumia magari ya serikali kubebea majani ya ng'ombe, kuna wengine wanatumia hela za serikali na kutofanya kazi inayotakiwa au iliyoainishwa, wengine wanachukua imprest au per diem hawaendi, kuna tofauti gani na huyu bwana ambaye jengo lipo na linaonekana kwa nini useme muda ni mdogo. Tuanze kutoa boriti kwenye macho yetu, huyu hana tofauti yoyote na watanzania wengi walio maofisini.

Chukua tano!

After all hajasababisha hasara kwa mujibu wa Mahakama hiyo hiyo ofisi kaitumiaje vibaya kama hamkuona hasara aliyosababisha. Tukienda serikalini hukumu kama hizi haziachi mtu. Ila kwa kuwa katolewa kafara kujiandaa na uchaguzi mkuu issue hata akikata rufaa haaishi hadi uchaguzi uishe
 
Mi naona ameonewa kwa sababu, ushahidi wa Daudi Balali haukutolewa. sasa anafungwa kwa lipi? Namshauri Liyumba akubali kifungo hicho ili awahi kutoka na asiwe na hofu kwani Mh JK alishakataa kura za wafanyakazi, ya kwake tutaihifadhi
 
Yaani Bongo kwa unafiki unawerza kukuta wiki ijayo UVCCM wanaandamana kupongeza juhudi za JK kupambana na rushwa. Mfano ukiwa ni huu!
 
mbona mnachanganya mambo?!!
kosa alofungiiwa ni kutumia madaraka vibaya na sio ubadhirifu wa pesa hili lilisha futwa zamani na mahakama.

kwa hiyo hukumu hiyo ni sahihi kabisa..
 
Liyumba hatapata msamaha wa JK. Kuna kisasi hapo. Lakini atatoka jela 23.9.2011. Atakuwa ameshatumikia kifungo chake, pamoja na kuwa
na tabia nzuri na uongozi jela.
 
Nchi hii hamuijui? Wezi wote wanajulikana kwenye vyombo vya dola. Kuanzia wahindi wanaohujumu uchumi wa nchi, wanasiasa wezi wa mali ya umma, wauza unga, matapeli wa kimataifa mpaka majambazi ya kutumia silaha! Wote wanajulikana, ila hawafikishwi kwenye vyombo vya sheria, na wakifikishwa pesa zao zinawatosha kushinda kesi.

Take my words, nchi hii ukiwa na pesa, hata kama ni za wizi hufungwi. Huyu Liyumba kafungwa kama kiini macho tu!

I concur with you, the fact ya kesi zote nchi kama wote wana pesa(mshitaki na mshitakiwa) hakuna hukumu ya halali ni upendeleo kutokana na nguvu ya pesa na tacks za wanasheria, au kama mmoja anapesa(mshitaki aua mshitakiwa) hakuna fair game pia, lakini kama wote hawana pesa( mshitaki na mshitakiwa) hapo ndiyo kuna hukumu fair kwa wote na hao wizi wa kuku ndiyo wanafall kwenye hili group
 
...utawaweza wadanganyika?
Weshasahau na tena wanasubiria kuwapigia kura 'Mapapa na Manyangumi' wanaotuhumiwaiwa kwa maskendeli ya mikataba feki ya madini, kesi ya Radar, wizi wa EPA na Richmond....wanamshikia bango 'kidagaa!'


Laws: We know what they are, and what they are worth! They are spider webs for the rich and mighty, steel chains for the poor and weak, fishing nets in the hands of the government. ~Pierre Joseph Proudhon, quoted in The Match!
 
Liyumba hatapata msamaha wa JK. Kuna kisasi hapo. Lakini atatoka jela 23.9.2011. Atakuwa ameshatumikia kifungo chake, pamoja na kuwa
na tabia nzuri na uongozi jela.
Hilo la kisasi cha JK nalo linazungumzwa sana mitaani, kwani kuna nini hapa....mdau unaweza kurudi na kutupa ufafanuzi juu ya hayo, ama ni yale yale ya kusikia kama ambavyo nami nasikiaga pale kijiweni kwangu SUWATA,
 
Hilo la kisasi cha JK nalo linazungumzwa sana mitaani, kwani kuna nini hapa....mdau unaweza kurudi na kutupa ufafanuzi juu ya hayo, ama ni yale yale ya kusikia kama ambavyo nami nasikiaga pale kijiweni kwangu SUWATA,
Ni yale yale uliyoyasikia kijiweni kwako. Yanahusu yule kisura wa gauni jekundu.
 
Angalia kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, 2007, Na. 11/2007:
"31. Any person who intentionally abuses his position in the
performance or failure to perform an act, in violation of law, in the
discharge of his functions or use of position for the purpose of
obtaining an undue advantage for himself or for another person or
entity, commits an offence and shall be liable on conviction to a fine
not exceeding five million shillings or to imprisonment for a term not
exceeding three years or to both."
Lakini sidhani kama Liyumba alishtakiwa kwa sheria hii ya kupambana na rushwa
 
Back
Top Bottom