Liyumba afungwa miaka 2 jela

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Kule mtaa wa pili(Michuzi) kuna habari kuwa Liumba amepatikana na hatia na kuhukumiwa miaka 2 jela kwa matumizi mabaya ya ofisi. Wadau hii nayo imekaaje?
 
Habari nilizozipata sasa hivi liyumba kutumikia miaka 2 kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma

Mhhh hapo mzee mzima PesaMbili Mramba tumbo joto! Akitoka jela arudishe gharama alizoliingizia taifa
 
Habari nilizozipata sasa hivi liyumba kutumikia miaka 2 kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma

Dah! Hiyo kali.

Juzi kuna kijana mmoja mitaa ya Kawe alienda sero miaka mitatu kwa kosa la kuiba kuku watatu! Hapo ndipo huwa naipenda sheria za Tanzania. Tafsiri yake inategemea n'tu na n'tu.
 
Habari nilizozipata sasa hivi liyumba kutumikia miaka 2 kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma

Duh ana bahati kweli....kesi ilivyoanza ungeweza kudhani atafungwa kuanzia miaka kumi na kuendelea!
 
pole liyumba, ila kata rufaa nadhani umeonewa tu
ni kweli ameonewa, na atakata rufaa, na itasikilizwa baada ya miaka 3 mingine, maana amepewa siku 90 za kukata rufaa, mjibu rufaa naye anapewa siku 90 za kujibu rufaa. Msajili anazo ziku 90 kuipangia siku ya kuisikiliza, hakimu naye ana toa siku 90 za kujiridhisha. Halafu siku 90 za kufanya final submission na siku 90 za mwisho za kusoma hukumu!, jumla ni miaka 3!.
 
This is the biggest joke I have ever heard.
Kwahiyo baada ya kifungo what next!!!
 
Habari nilizozipata sasa hivi liyumba kutumikia miaka 2 kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma

Pole sana Amatus Liyumba. Kwa hiyo atatumikia one year? Kwa kuwa kukaa jela wanahesabu siku mchana na usiku? Anyway, vumilia tu Amatus, one year si mbali sana. Kumbuka kuna ambao wamefungwa maisha kama nguza vikings na mwanaye na wengine over 30 years na wengine death penalty so one year or say two zitapita haraka sana. Pole Jennifer kwa kumhangaikia baba yako for over one year and half! Jipe moyo, pangeni mkakati wa kuendelea na maisha baada ya hapo na baba atakuja, tena huenda sikukuu ya uhuru akapata msamaha wa rais.
 
Dah! Hiyo kali.

Juzi kuna kijana mmoja mitaa ya Kawe alienda sero miaka mitatu kwa kosa la kuiba kuku watatu! Hapo ndipo huwa naipenda sheria za Tanzania. Tafsiri yake inategemea n'tu na n'tu.

Lazima sheria zibadilishwe ili watu wa namna hii wafungwe maisha na kazi ngumu juu na wafilisiwe mali zao. Kwa sasa baada ya miaka miwili ataanza kututimulia vumbi na li-Hammer lake
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imesoma Hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba,Katika hukumu hiyo Liyumba amepatikana na hatia na kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili dhidi ya kesi ya utumiaji mmbaya wa madaraka .

===================

Awali Liyumba alifikishwa mahakamani hapo akiwa pamoja na aliyekuwa meneja miradi wa BoT Deogratius Kweka, ambapo kwa pamoja walikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo, jambo lililopelekea serikali kupata hasala ya sh bilioni 221, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.

Hata hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, upande wa mashtaka ulimuachia aliyekuwa mshtakiwa mwenza wa Liyumba {Kweka}, na kumshitaki Liyumba kwa kesi hiyo.Upande huo wa mashtaka uliita mahakamani hapo mashahidi 8, wakiwamo waliokuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa BoT, pamoja na kutoa vielelezo mbali mbali vinavyohusiana na kesi hiyo.

Baada ya ushahidi huo kumalika kusikilizwa, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumfutia Liyumba shtaka la kuisababishia serikali hasala ya bilioni 221 baada ya Upande huo wa serikali kupitia ushahidi na vielelezo vyake kushindwa kuithibitishia mahakama hiyo kama Liyumba alihusika na kosa hilo.Kufuatia uamuzi huo, mahakama ilimtaka Liyumba kujitetea juu ya uhusika wake katika shtaka la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.

Katika utetezi wake Liyumba alijitetea mwenyewe kama shahidi wa kwanza kutoka upande wa utetezi, na baadae alimwiita shahidi wa pili ambaye ni Bosco Ndimbo Kimela, aliyekuwa katibu wa BoT.Baada ya kumaliza usikilizwaji wa ushahidi huo, mahakam hiyo ilizitaka pande zote mbili kuwasilisha hoja zao za kisheria, ambapo alipanga kusoma hukumu dhidi ya Liyumba ifikapo May 24, 2010.

source: michuzi blog
 
So jamaa kama ameshakaa huko one and a half or 2yrs then atakuwa huru....

I like tz where kila kitu kinawezekana.

Watu tutaumiza vichwa weee kusoma magazeti, kutafsiri, kutafakari lakini at the end of the day vitu vinakuwa nje ya mategemeo...anyways.
 
Atatumikia takribani miezi mitatu na siku kadhaa tu kwani tarehe 9 Desemba atatolewa kwa msamaa wa Raisi.
 
Back
Top Bottom