Liwale, Lindi: Wazazi huwachoma Watoto Sindano za kuzuia Mimba na kuwaweka Vijiti wanapovunja Ungo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi amesema kumekuwepo na tatizo la wazazi wilayani humo kukwepa majukumu ya kuwasomesha watoto wao hali inayopelekea kuwachoma sindano za kuzuia mimba watoto wenye umri wa miaka 12 na kuwawekea vijiti watoto pindi wanapovunja ungo.

Ameeleza "Mtoto akishavunja ungo wanamtengenezea kajumba kake kwa nje na wanawachoma sindano za kuzuia mimba watoto wadogo na kuwaweka vijiti, sasa kwa kufanya hivyo unakuwa umewaruhusu wao kufanya mapenzi na ukishamruhusu anakuwa hana hamu tena na shule kwahiyo changamoto ni hiyo wanakimbia mzigo wa kusomesha"

"Mimi kama DC nimeweka utaratibu, nikikuta mtoto ameacha shule eneo flani au ameozwa hayupo shule namchukua kuanzia Mtendaji, Mratibu wa Elimu Kata ndani, Mwalimu Mkuu ndani, baba na mama wa mtoto ndani, nikikuta mtoto ameolewa nachukua hao niliowataja pamoja na wazazi wa kijana, jukumu nakuwa nimelicha kwa kijiji kizima kwa sababu wanakuwa wanaogopa kwa hiyo wao wanakuwa mabalozi wa kwanza"


SupaBreakFast
 
Back
Top Bottom