Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Dec 7, 2018
730
1,653
Sababu kuu ya kuwatoa wangu shule ya kiingereza nakuwarejesha kayumba ni uchumi lakini kama unavyo jua tena ukitaka kumuua paka lazima kwanza umpe jia baya. mimi sababu zifuatazo ndizo ambazo zinanifariji katika kipindi hiki ninacho watoa watoto wangu english medium kuwaleta kayumba.

Kwanza nina watoto watatu. Form 3( girl) std 3( boy) na std1 ( boy)

History: Huyu wa form 3 kuanzia la kwanza hadi la saba alisoma english medium na akafulu vizuri kwenda secondary. Akiwa primary alifanya mtihani wa seminary ambayo ni private na alifaulu but ulipofika wakati wa kuingia form one hela ikakata nikaona wacha nimpeleke kwanza kayumba ( ambayo alichaguliwa ) kwa matarajio kwamba baadae ninge muhamisha but uchumi bado haujakaa sawa mwisho wa siku nimeamua kumuacha hiyo hiyo kayumba ( bahati nzuri anajitahidi sana darasani/shule ipo karibu na nyumbani ana anasoma masomo ya arts/ niliona kulipa mamilioni ya hela ili mtoto asome history na kiswahili ni hesabu mbaya/ plus mtoto ananionea huruma baba yake anataka aseome shule hiyo hiyo, ana marafiki na ameizoea) so kwa huyu nitampambania tu atapata division one form four without a doubt.

SSasa kwa hawa wadogo zake. sababu zangu za kujifariji ni hizi hapa:

1. Nita save pesa nyingi., mtoto mmoja kwa mwaka hesabu zote ni four millions plus point, wawili inakuwa almost nine millions. nine millions times 7 is almost 63 millions. hii 63 millions bora niipeleke kwenye nyumba ili by the time wanamaliza form four at least kila mtoto awe ana nyumba yake japo ya thamani ya milioni 25 to 30. Namshukuru Mungu Alhamdulilahi nina nyumba moja. But hii ni ya kwangu, nataka watoto wangu wote watatu kila mmoja awe na nyumba yake. Kuendelea kuwaweka english medium nitatumia pesa nyingi ambazo ningeweza kuziweka kwenye ujenzi.

2. IMANI ZA KISHIRIKINA KWA BAADHI YA WAMILIKI WA SHULE : Kuna mdau alishawahi kuandika humu kwamba mtoto wako ni bora umpeleke shule zinazo milikiwa na serikali kama vile olympio na diamond au zinazo milikiwa na taasisi kubwa kubwa lakini sio hizi zinazo milikiwa na kina mr and mrs fulani kwa sababu wafanya biashara binafsi wa kitanzania wana kasumba ya kufanya makafara kwa ajili ya kukuza biashara zao... u can never tell siku gani waganga wao watawaambia wawatoe kafara watoto kadha wa kadha. Mtoto wako anaweza kuwa miongoni mwao pia. Ile ishu ya ajali ya watoto wa shule ile ya arusha watu wengi wana ihusisha na ushirikina...

3. Walimu kuhamahama : Kwenye shule zetu za private zinazo milikuwa na watu binafsi kuna mchezo wa kuibiana waalimu au walimu kuhamahama kwa sababu ya kfuata maslahi. Kuhama kwa mwalimu ( hasa mwalimu mzuri) kunaweza kumuathiri mtoto kisaikolojia na kimasomo pia.

4. Wanafunzi kuhama hama( hii ni kwa sababu ya wazazi kutafuta unafuu wa ada ) believe or not , kampani ya wanafunzi ina nafasi kubwa sana katika 'furaha' ya mtoto shuleni. Mimi nakumbuka nikiwa darasa la tatu nilikuwa napenda kwenda shule kwa sababu ya msichana mmoja classmate wangu ambae nilikuwa nampenda sana, siku asipokuja shule ilikuwa ni siku mbaya sana kwangu. Mwaka 94 nikiwa darasa la tatu mwezi wa kumi na mbili nikasikia tetesi amehamishiwa lindi kwa mama ake, ulikuwa mwezi mgumu sana kwangu mwaka huo.. luckily kumbe walisafiri tu baadae walirudi tena mjini daslamu na furaha yangu siwezi kuielezea kwa lugha ya kiswahili.

4. Mtoto kukaa nyumbani kwa muda mrefu ( kwa sababu ya kukosa ada ya shule, watoto mara nyingi wanakuwa wanakaa nyumbani kwa muda mrefu.) hakuna kitu kiliniuma mwaka huu kama watoto wangu kukaa nyumbani kwa mwezi mzima kwa sababu baba nadaiwa ada.

5. Kujifunza ukakamavu : kusoma shule ya kiswahili kuna mpa mtoto ( hasa wa kiume) nafasi ya kujifunza ukakamavu na ustahimilivu. Anaamaka nyumbani asubuhi anaenda mwenyewe shule kwa miguu kisha anarudi nyumbani kwa miguu.

6.. Watoto kufundishwa malezi ya kizungu kwenye shule za english medium.

7. walimu wa english medium wengi wao walisoma shule za kayumba.

Please ongezea na wewe sababu zako.

Pia soma
: Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba
 
Kinachokusumbua ni umaskini ulio nao ila sio swala cha msingi jua kwamba elimu ni haki ya msingi ya mtoto hivyo jitahidi uwape haki ya msingi sehemu bora hizo sababu zinakuja baada ya kua maskini kwani dada yao aliposoma EM alitolewa kafara? Na kusema mtoto anakuonea huruma nakataa hakuna mtoto anaekataa shule nzuri kisa marafiki kwani huko EM asingepata marafiki? Wazazi tujitahidi sana watoto wetu wasome sehemu nzuri kuna manufaa baadae.
 
Kinachokusumbua ni umaskini ulio nao ila sio swala cha msingi jua kwamba elimu ni haki ya msingi ya mtoto hivyo jitahidi uwape haki ya msingi sehemu bora hizo sababu zinakuja baada ya kua maskini kwani dada yao aliposoma EM alitolewa kafara? Na kusema mtoto anakuonea huruma nakataa hakuna mtoto anaekataa shule nzuri kisa marafiki kwani huko EM asingepata marafiki? Wazazi tujitahidi sana watoto wetu wasome sehemu nzuri kuna manufaa baadae.
aisee
 
Mi niliwahi poteza kazi nikakaa miaka minne mtaani naungaunga,na hapo sikua na kwangu. Ila namshukuru Mungu kati ya vitu ambavyo nilipigana ni kuhakikisha mtoto wangu anaendelea na shule ya English medium alioanza nayo japo alikua na vipindi vingi vya kukaa nyumbani na hata ndugu walikua wananisema sana eti nimrudishe St. Kayumba ila nilikomaa hadi mwisho na mambo yakarudi sawa.

Kwa mtoto kusoma secondary za serikalini haina shida kabisa kama alisoma English medium. Ila kusoma shule za serikali primary school kwa usawa huu ni kumpa wakati mgumu sana. As long as upo kwako wapiganie wasome shule za bei ndogo ambazo unalipa hata 1.5m each kwa mwaka mbona zipo nyingi. Mpambanie elimu achana na mipango ya nyumba.
 
Mara ya kwanza kuibuka kwa shule hizi mlizishokea na kuziona ni za maana kuliko shule zilizokuwepo, mkadhani watoto wenu wakihitimu huko watajua sana kiiengereza na kufaulu sana kisha kupata ajira kumbe ulikuwa ni ulimbukeni tu. Sasa naona wazazi wengi wanaondoa watoto wao huko na kuwapeleka za kawaida, sijui ni kupunguza gharama au shule hizo zimepoteza umaarufu na hazileti matumaini kwa wahitimu wake
 
Katika pitapita zangu nimepitia shule hizi nyingi nikitaka kujua kama kweli watoto wanajua kiingereza hata cha kawaida tu. Nichokikuta ni kituko na ubabaishaji tu, watoto hawajui kuongea kiingereza fasaha, wanaongea kama walimu wao ambao wengi ni hawahawa ngumbaru wasiojua kikutafuna kiingereza vizuri. Walimu wao hawana misamiati ya kutosha kuweza kufundisha kiingereza fasaha.

Walimu wenyewe ni form six plus diploma na wengine ni form four plus certificate ya ualimu, wapi wamejua kuongea lugha ya kiingereza? Ni ubabaishaji tu unaofanyika kwenye shule hizo za kiingereza. Wazazi wengi wenyewe tu lugha ya kiingereza hawaijui wanafikiri watoto wao wakijua kutamka dady, mom ndiyo tayari wamejua kiingereza. Wanaojua kiingereza ni wale wanachokitumia muda mwingi hata wakiwa nje ya shule
 
Kuna jamaa humu aliwahi kutoa ushauri ambao mimi binafsi ulinifurahisha na nitautumia mbeleni huko. Alisema, badala ya kutoa 1.5m kulipa ada ya mtoto wa chekechea, kama unapenda sana mtoto asome english medium, Weka bajeti ya 1.5m Tshs, ila tafuta basi hata zile za kanisa, zenye ada ya Tshs. 800,000/= kwa mwaka halafu Tshs. 700,000/= nunua viwanja vilivyopimwa vya Halmashauri za Wilaya mikoani huko au nunua ng'ombe wawili wadogo wa kufuga.

Kila mwaka mnunulie mtoto kiwanja 1 au ng'ombe 2, mpaka anamaliza darasa la 7 atakuwa na viwanja 7 ama ng'ombe 14 bila kuhesabu watoto wao. Sekondari asome hizi za umma (serikali) ila uendelee kumnunulia viwanja, mpaka form 6 atakuwa na viwanja 13 au ng'ombe 30 hivi.. huyo tayari ushamuandalia njia nzuri ya kujiajiri. Mtaji upo kwa kuuza viwanja vyake kadhaa au ng'ombe kadhaa.

Sababu kubwa ni kuwa unamwamsha mtoto aende shule huku mdogo wako amelala ndani kwa kukosa ajira na huku ana digrii. Unafanya kitu ambacho matokeo yake huna hakika nayo, unabet. Sasa ya nini kubet kwa kuweka madau makubwa???
 
Your level of honesty imenifurahisha sana,
Uchumi umekupiga ila ukaamua utafute sababu za kujiridhisha
Nimejikuta naishia kucheka tu!
Mwl wangu wa literature aliwahi niambia hiki kitu , kwamba unapokuwa kwenye shida, jaribu kuzipenda shida hizo na kuzipa positive attitudes!
Yaani hata kama umelala na njaa usiku hujapata usingizi unajiambia "ninachoipendea njaa hata mwizi hawezi kukuibia usiku maana unakua macho na utamsikia"
Mdau kafulia ila sababu anazotoa za kuwahamishia watoto shule za kayumba nazo pia zina mashiko
 
Katika pitapita zangu nimepitia shule hizi nyingi nikitaka kujua kama kweli watoto wanajua kiingereza hata cha kawaida tu. Nichokikuta ni kituko na ubabaishaji tu, watoto hawajui kuongea kiingereza fasaha, wanaongea kama walimu wao ambao wengi ni hawahawa ngumbaru wasiojua kikutafuna kiingereza vizuri. Walimu wao hawana misamiati ya kutosha kuweza kufundisha kiingereza fasaha. Walimu wenyewe ni form six plus diploma na wengine ni form four plus certificate ya ualimu, wapi wamejua kuongea lugha ya kiingereza? Ni ubabaishaji tu unaofanyika kwenye shule hizo za kiingereza. Wazazi wengi wenyewe tu lugha ya kiingereza hawaijui wanafikiri watoto wao wakijua kutamka dady, mom ndiyo tayari wamejua kiingereza. Wanaojua kiingereza ni wale wanachokitumia muda mwingi hata wakiwa nje ya shule
barikiwa
 
Mwl wangu wa literature aliwahi niambia hiki kitu , kwamba unapokuwa kwenye shida jaribu kuzipenda shida hizo na kuzipa positive attitudes
Yaani hata kama umelala na njaa usiku hujapata usingizi unajiambia "ninachoipendea njaa hata mwizi hawezi kukuibia usiku maana unakua macho na utamsikia"
Mdau kafulia ila sababu anazotoa za kuwahamishia watoto shule za kayumba nazo pia zina mashiko
barikiwa
 
sababu kuu ya kuwatoa wangu shule ya kiingereza nakuwarejesha kayumba ni uchumi lakini kama unavyo jua tena
Hapa sababu ya kuwatoa ni moja na ya msingi, bahati mbaya au kwa kutokuwa na umakini na janjajanja ya WaTz, kipato kimekata.
Kama tangu uwatoe mpaka sasa hizo shule zipo, na zinaendelea, basi ujue hakuna cha kutolewa kafara, waalimu wakihama wengine hutafutwa n.k.
 
Mimi kama wewe tu. Nilikuwa na watoto 2 wote private.

Nilienda nao vizuri kwenye ada mpaka ilipokuja CORONA. Shule zilipofunguliwa walipandisha ada kufidia ile miezi waliokaa nyumbani.

Hapa ndipo nilipoona maisha magumu maana hata shughuli zangu za kipato zilitetereka. Nilijikuta na stress kuhusu ada kuliko hata kula.

Mwisho wa siku nikasema sina yeyote wa kumridhisha zaidi ya uhalisia wa maisha yangu.
Nimepeleka wote Diamond (ada laki 4 kwa mwaka, school bus ya kurudi tu 35,000 kila mmoja kwenda nawepeleka mwenyewe asubuhi), maisha yanaenda na zile stress tupa kule.

Tunachopambania hasa kwenye English medium ni lugha, nashukuru wanangu wana msingi mzuri wa lugha kabla hata ya shule sababu ya muingiliano katika familia yetu.

Mmoja anamaliza la saba September, Mungu akijaalia ataendelea St. Kayumba atakapochaguliwa.

Kubwa na la muhimu, tuepuke sana kusikiliza wake zetu. Mara nyingi wana hofu mno juu ya watu watasema nini kuliko uhalisia wa kipato.

By the way huko Diamond nimekuta watoto wa walimu wa shule niliowahamisha wanangu nao wanasoma hapo hapo. Nililijua hilo baada ya kukutana na hao walimu wakipeleka watoto wao.
 
Back
Top Bottom