Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

A team on transition

Damage ya yule kipara was huge
Kipara tutamuonea tu , ule mfumo wa Modern Head Coach ulikuwa una shida aisee

Tofauti kati ya Traditional Manager na Modern Head Coach: Mabadiliko ya mfumo ya mgawanyo wa Uongozi ndani ya Liverpool

In a Modern football, kuna tofauti kubwa sana kati ya mfumo wa Traditional Manager na ule wa Modern Head Coach.

Mabadiliko haya yanaonekana wazi ndani ya Liverpool, hasa baada ya klabu kurekebisha muundo wake wa uongozi wa soka.

Traditional Manager – Jurgen Klopp

Katika mfumo huu wa zamani, meneja alikuwa na mamlaka mapana katika kila eneo la klabu. Hakuwa tu mtu wa kupanga kikosi na kusimamia mazoezi, bali alikuwa nguzo kuu ya football project nzima.

Klopp alikuwa na ushawishi mkubwa kwenye:

Squad Building: Kupanga aina ya wachezaji na kujenga kikosi cha ushindani.

Player Recruitment: Kushiriki moja kwa moja kwenye utambuzi na maamuzi ya usajili.

Scouting Structure: Kuathiri mwelekeo wa idara ya utafutaji vipaji.

Medical & Performance: Kuwa na sauti kwenye masuala ya afya na utimamu wa wachezaji.

Contract Decisions: Maamuzi ya kimkakati ya mikataba.

Kwa kifupi: Alikuwa na mamlaka mapana zaidi ya uwanja wa mazoezi; ndiye aliyekuwa dira ya identity na long-term direction ya klabu.

Modern Head Coach – Mfano: Arne Slot & Andoni Iraola

Katika soka la kisasa, majukumu yamegawanywa kwa uwazi zaidi kati ya benchi la ufundi na uongozi wa juu (football operations). Liverpool wapo chini ya CEO of Football na Sporting Director.

A) Majukumu ya Head Coach:

Coaching & Training: Kuandaa mazoezi na kuendeleza uwezo wa wachezaji.

Tactical Identity: Kujenga mfumo wa kucheza (playing style, pressing, build-up).

Matchday Management: Kuchagua kikosi, kufanya substitutions na mabadiliko ya kiufundi uwanjani.

Player Development: Kuhakikisha wachezaji wanatekeleza majukumu yao ndani ya mfumo.

Traditional Manager: Anawajibika kwa kila kitu kuanzia usajili hadi matokeo.

Modern Head Coach: Anawajibika zaidi kwa tactical execution, ukuaji wa wachezaji na matokeo uwanjani, wakati uongozi wa juu unawajibika kwa muundo wa kikosi na mkakati wa usajili.

Kwa Nini Hili Ni Muhimu kwa Liverpool?

Mashabiki wanapokosoa usajili, si kila wakati lawama zinapaswa kwenda kwa Kocha. Tunapaswa kujiuliza:

Je, mkakati wa usajili unaendana na falsafa ya kocha?

Je, Sporting Director anasajili profiles sahihi za wachezaji?

Je, kuna uwiano mzuri kati ya ubora wa kikosi na gharama?

Na pale usajili unapofeli, nani anawajibika?

Modern football is no longer just about having a great manager; it is about building a great football structure.

Liverpool inahitaji muundo ambao Sporting Director, idara ya usajili na Head Coach wanafanya kazi chini ya falsafa moja.

Bila alignment hiyo, hata usajili wa pesa nyingi unaweza kufeli.
A successful football project is built on structure, not just star names.

YNWA!
 
IMG-20261108-WA0015.jpg

📸 - Trent Alexander Arnold signed for Real Madrid expecting to be their STAR right back and chase a Ballon D'or...

Instead he's lost his place in the side and is now stuck on the bench while Valverde covers at right back and scores in back to back games.

Rough one.
 
#LFC 🔴 🚨
EXCL: Liverpool and Trey Nyoni have reached a verbal agreement over a new long-term contract.

The midfielder is set to commit his future to Anfield following interest from several clubs during the summer.

Nyoni is viewed as an important part of Andoni Iraola’s long-term plans with Liverpool.
 
🎖️ | @FabrizioRomano: There is a serious possibility this could be Alisson’s last season at Liverpool.

🎖️ | @FabrizioRomano: Liverpool are “really happy” with Giorgi Mamardashvili.
 
😂😂😂😂 Pathetic kulia kulia na penati moja tu na pengine ingedakwa yaaani.
That done and dusted should be aiming to win vs Crystal Palace....my main worry is Crystal Palace are creating lots of chances I guess wapi top 5 kwa chances created, huku Liverpool akiwa nafasi ya 17 ku create chance chache inside the box hivyo tuwe wapole Hali kwetu badoooo.

YNWA
Shame shame shame
Litimu halina hata on target Moja Tena anfield , bila aibu ipo kulilia penati
 
Lile tapeli limevuruga timu mazima
Potential and quality players wote likafukuza.
😂😂😂
Usichume dhambi kwa Slot, yeye alikuwa hanunuwi wala kuuza mchezaji, kama Salah aliomba mwenyewe kuondoka na aliondoka kabla hata mkataba wake haujaisha. TAA ni msaliti alikuwa anajifunza kispaniloa kimya kimya.
 
Yaani sasahivi hizi stori na hizi vizungu sitaki hata kusoma
Ni utapeli mtupu
Unauza kelleher unaanza kumangamanga kama hivi
Kelleher alikuwa hataki kukaa benchi alikuwa anataka aanze mbele ya Becker sasa wangeendelea kubaki naye ?

Timu ilikuwa ni Viongozi matapeli Hughes na Edwards, kipa wa Aston villa sasa hivi eti tunamtaka awe mbadala wa Becker, wakati dogo toka yupo Italy alikuwa na potential kubwa sana ina maana Hughes alikuwa hamuoni ?
 
😂😂😂
Usichume dhambi kwa Slot, yeye alikuwa hanunuwi wala kuuza mchezaji, kama Salah aliomba mwenyewe kuondoka na aliondoka kabla hata mkataba wake haujaisha. TAA ni msaliti alikuwa anajifunza kispaniloa kimya kimya.
Sasa lilianza kumuwekea bifu
Hadi pharaoh wa watu anakuja kutulilia hadharani
Yaani limeweka bifu na wachezaji,,likakomaa na waholanzi wenzie iwe mvua iwe jua.
Huyu jamaa ndiye alikuja kuichimbia Liverpool kaburi,
Mwenzie kaja kusafirisha tu.
 
Kelleher alikuwa hataki kukaa benchi alikuwa anataka aanze mbele ya Becker sasa wangeendelea kubaki naye ?

Timu ilikuwa ni Viongozi matapeli Hughes na Edwards, kipa wa Aston villa sasa hivi eti tunamtaka awe mbadala wa Becker, wakati dogo toka yupo Italy alikuwa na potential kubwa sana ina maana Hughes alikuwa hamuoni ?
Sasa Allison ambaye kudaka penati hata moja hawezi
Unajua kabisa ashakuwa Mzee,
Una Gen Z ambaye miaka 2 mbele atakufaa,,unamuuza.
Hakuthaminiwa,Timu haina Shukurani hii.

Sasa ngoja Mnunue hayo matapeli mapazia utaanza wote kunena kwa lugha moja mpya.
 
Sasa lilianza kumuwekea bifu
Hadi pharaoh wa watu anakuja kutulilia hadharani
Yaani limeweka bifu na wachezaji,,likakomaa na waholanzi wenzie iwe mvua iwe jua.
Huyu jamaa ndiye alikuja kuichimbia Liverpool kaburi,
Mwenzie kaja kusafirisha tu.
Bado tuba hali tete, sijui labda 1892 Holding watampa Iraola full authorities kama ilivyokuwa kwa Klopp hapo tunaweza tukakaa sawa.

Jiulize Hughes alisajili Frimpong, Isak, Wirtz (hawa wote sasa hivi ni magarasa na hawaendani na mfumo wa Iraola) matokeo yake vipaji kina Nyoni na Rio wanaonekana wana kitu. Liverpool huwa hawasjili majina ila huwa wanasajili vipaji vinavyoendana na mfumo wa timu.

Gravenberch sasa hivi mfumo unamfanya aonekane ana struggle, Wirtz chezaji la mabilioni yaani hakuna kitu bora hata ile namba yake acheze Szoboszlai

Matatizo yapo mengi sana kwenye huu mfumo wa Modern Head Coach, Makocha tutawalaumu kwamba wachezaji wazuri na wenye majina wapo lakini kwanini tunakosa hata shot on target?
 
Tukubali tu kuwa hata makocha ni vilaza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom