Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

👀GOLI LA KWANZA LA EPL KWA KOCHA ARNE SLOT LILIFUNGWA NA DIOGO JOTA...

✍️Tarehe kama ya leo mwaka, 2024, marehemu Diogo Jota alifunga goli la kwanza la EPL chini ya kocha Arne Slot katika ushindi wa goli 2 bila dhidi ya IPSWICH.

🏟️Portman Road – 17 Agosti 2024

⚽ Ipswich Town 0–2 Liverpool

🥇 Dakika ya 60 – Diogo Jota
🥈 Dakika ya 65 – Mohamed Salah
 
FB_IMG_1755437871991.jpg
 
Liverpool wamewasilisha ofa ya pili na iliyoboreshwa kwa ajili ya kumnasa Alexander Isak, kwa mujibu wa mtangazaji mmoja ambaye pia amedokeza kuwa Real Madrid wanaonyesha nia ya kumsajili straika huyo wa Newcastle United, huku kocha Eddie Howe akifanya mtazamo wake kuhusu suala hilo kuwa wazi kabisa.

Isak amekuwa gumzo kubwa katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi, ambapo Liverpool wako makini kuhakikisha wanamsajili straika huyo, huku Newcastle wakisisitiza – angalau hadharani – kwamba hastahili kuuzwa.

Mwandishi wa masuala ya usajili wa TEAMtalk, Fraser Fletcher, ndiye aliyefichua kwa mara ya kwanza mnamo Julai 24 kwamba Isak amewaambia Newcastle anataka kuondoka na kujiunga na Liverpool, na hali hiyo imezidi kuchukua sura mpya tangu hapo.

Taarifa zinaeleza kuwa Isak tayari amekubaliana masharti binafsi na Liverpool na hajajiunga na mazoezi ya kikosi cha Howe, huku ripoti zikidai pia kwamba mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden ameondoka nyumbani kwake Newcastle.

Liverpool tayari wamewahi kutoa ofa ya pauni milioni 110 (€127.2m, $148.5m) pamoja na nyongeza, lakini Newcastle walikataa, wakiamini Isak anagharimu pauni milioni 150 (€173.8m, $203.3m).

Kwa mujibu wa TEAMtalk, Liverpool wako tayari kutoa ofa ya pili, lakini mabingwa hao wa EPL wanasubiri Newcastle wapate mchezaji mbadala kwanza.

Hata hivyo, mtangazaji wa beIN SPORTS, Richard Keys, amefichua kuwa chanzo chake kimemwambia kuwa Liverpool wamewasilisha ofa ya pili ya pauni milioni 140 (€162m, $190m) kwa ajili ya Isak.

Keys pia amesema kwamba vigogo wa Hispania na Ulaya, Real Madrid, nao wameonyesha nia ya kumsajili Isak, ambaye alifunga mabao 23 na kutoa asisti 6 katika mechi 34 za Premier League msimu uliopita akiwa na Newcastle.

Keys alisema kwenye beIN SPORTS mnamo Agosti 15:
“Nimesikia leo kuwa Liverpool wamewasilisha ofa ya pauni milioni 110. Ofa ya pili ni pauni milioni 80 sasa na milioni 60 msimu ujao.
“Chagua unayoitaka. Lakini pia nimesikia kwamba Real Madrid wanaweza kuhusika.
“Siwezi kuamini kama angefanya uamuzi wa namna hiyo bila kuwa na uhakika mkubwa kwamba ataondoka kabla ya dirisha la usajili kufungwa.”
 
Mumekutana na wavimba macho ,kutaneni na wanaume kama crystal palace ndio mujue munaruka ruka tuu🤣🤣🤣
 
Mohamed Salah, au "Mfalme wa Misri": Ni vipi mvulana mdogo akawa "nembo ya taifa"?

"Kila ninapoingia hapa, siwezi kujizuia kumkumbuka namna alivyotembea, alivyotawala mpira. Lilikuwa jambo la kipekee kabisa; tofauti na lolote nililowahi kuona."

Hayo ni maneno ya mmoja wa makocha wa kwanza waliogundua kipaji cha mchezaji Mmisri, Mohamed Salah, akiwasimulia waandishi huku akisimama mbele ya lango jipya la kijani kibichi la Kituo cha Vijana cha Kijiji cha Nagrig.

Katika kijiji hiki cha Nagrig, kilichoko takribani saa tatu kufika kaskazini mwa mji mkuu wa Cairo, ndipo historia ya mmoja wa washambuliaji mahiri zaidi duniani ilipoanzia.

Salah ndiye aliyewezesha klabu ya Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) mwezi Mei 2025.

Mitaani mwa Nagrig, Salah alianza kucheza soka akiwa na umri wa miaka saba, akiigiza mashujaa wake wa utotoni: mshambuliaji wa Kibrazili Ronaldo, kiungo fundi wa Kifaransa Zinedine Zidane, na gwiji wa Kiitaliano Francesco Totti.

Mohamed alikuwa mdogo kimwili ikilinganishwa na wachezaji wenzake, lakini aliweza kufanya mambo ambayo hata wavulana wakubwa hawakuweza kufanya," anasema kocha wa kwanza wa Salah, Ghamry Abdel Hamid El-Saadani, akionyesha uwanja wa nyasi bandia uliopewa jina kwa heshima yake.

Mohamed alikuwa mdogo kimwili ikilinganishwa na wachezaji wenzake, lakini aliweza kufanya mambo ambayo hata wavulana wakubwa hawakuweza kufanya," anasema kocha wa kwanza wa Salah, Ghamry Abdel Hamid El-Saadani, akionyesha uwanja wa nyasi bandia uliopewa jina kwa heshima yake.

Salah, mwenye umri wa miaka 33, anakaribia kuanza msimu wake wa tisa akiwa na Liverpool kama winga na amefunga mabao 245 katika mechi 402 za ligi na vikombe tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2017.

Nyota wa kwanza wa Misri kung'ara katika soka la kimataifa, Mohamed Salah, ametwaa mataji yote ya ndani akiwa na klabu ya Liverpool, pamoja na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (Champions League).

Hata hivyo, bado hajafanikiwa kutwaa taji akiwa na timu ya taifa ya Misri.

Kwa kuwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) linatarajiwa kufanyika Desemba 2025, na Kombe la Dunia mwaka 2026, BBC Sport ilizuru Misri kuchunguza maana halisi ya Salah kwa taifa hili lenye watu milioni 115 wanaopenda soka kwa moyo wote na jinsi kijana kutoka familia ya kawaida alivyoibuka kuwa almasi ya taifa.

"Nakumbuka furaha ya baba yangu kila tulipomtazama Salah," anasema Lamis El-Sadig, akiwa katika Dentist Café, eneo la mashariki mwa Cairo.

"Baada ya Salah kujiunga na Liverpool, baba yangu na mimi tulikuwa hatukosi mechi yoyote kwenye runinga."

Kahawa hiyo maarufu, iliyopewa jina kutokana na taaluma ya awali ya mmiliki wake daktari wa meno imekuwa kitovu cha mashabiki wa Liverpool wanaokusanyika kutazama mechi kwenye skrini kubwa.

Lamis, akiwa amevaa jezi ya Liverpool yenye jina la baba yake mgongoni, anasema kwa hisia:

"Kwa masikitiko, alifariki miaka miwili iliyopita."

Anakumbuka:

"Kila wiki, tulikuwa na saa mbili za furaha zaidi nyumbani wakati wa mechi za Liverpool. Na hata nilipokuwa shule au kazini, baba alikuwa akinitumia ujumbe kunieleza kinachoendelea."

Lamis anaeleza kuwa Salah hakukulia katika familia yenye uwezo mkubwa:

"Lakini alijituma mno na kujinyima sana hadi kufikia mafanikio haya. Wengi wetu tunajitambua kupitia yeye''.

Nagrig ni kijiji kidogo cha kilimo kaskazini mwa Misri, kilichojaa mashamba ya jasmini na tikiti maji.

Barabarani, magari, pikipiki, mikokoteni na wanyama hutumia njia moja.

Hapa ndipo Mohamed Salah, anayejulikana kama "Mfalme wa Misri," alikulia.

"Familia ya Salah ndiyo msingi na siri ya mafanikio yake," anasema El-Saadani, kocha wake wa kwanza, aliyemlea tangu akiwa na umri wa miaka minane.

"Wanaishi hapa kwa unyenyekevu na heshima, watu wanawapenda sana."

Kituo cha Vijana cha Nagrig kimekarabatiwa kwa heshima ya Salah, na sasa uwanja wake unafanana na wa mazoezi ya wachezaji wa kulipwa.

"Familia ya Salah ilijitolea sana kwa ajili yake hasa baba na mjomba wake," anasema El-Saadani, akiwa karibu na bango la Salah na Kombe la Ligi ya Mabingwa.

Mitaani, watoto wamevalia jezi za Liverpool na Misri zenye jina lake.

Nje ya shule yake ya zamani kuna picha ya ukutani, na tuk-tuk hupita kwa kasi huku likiwa na bango la uso wake.

Kijijini humo bado kuna kinyozi aliyekuwa akikata nywele za Salah alipokuwa kijana.

"Mimi ndiye niliyempa nywele za msokoto na ndevu," anasema Ahmed Al-Masry.

"Marafiki walimshauri asinyoe kijijini, lakini aliendelea kuja kwangu. Kesho yake, walimuuliza: 'Kinyozi wako ni nani?'"hii ni kutokana na utanashati aliokuwa nao.

Kinyozi wa kijiji anakumbuka ustadi wa Salah katika soka, alipokuwa akicheza katika Kituo cha Vijana na mitaani mwa Nagrig.

Anaongeza:

"Kumbukumbu yangu kuu ni tulipokuwa tukicheza PlayStation. Salah kila mara alichagua Liverpool. Wengine walichagua Manchester United au Barcelona, lakini kwake ilikuwa Liverpool tu. Sasa hivi, watoto wote wadogo wa kijijini wanataka kuwa kama yeye."

Salah alipata mafunzo rasmi ya soka kwa miaka sita katika klabu ya El Mokawloon El Arab, yenye makao yake mjini Cairo, maarufu pia kama El Mokawloon.

Aliijiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 14, na safari yake ya kucheza kandanda huku akiendelea na masomo iligeuka kuwa hadithi ya kipekee, si tu nchini Misri bali hata kimataifa.

Katika gari dogo la abiria aina ya Suzuki lijulikanalo kama "tonaya" lililosimama pembezoni mwa kijiji cha Nagrig, abiria wanangoja kwa wasiwasi.

Safari haiwezi kuanza hadi gari lijazwe.

Hapa ndipo safari ya kila siku ya Mohamed Salah kuelekea mazoezini ilipoanzia akiwa kijana.

"Ilikuwa safari ngumu na ya gharama kubwa," asema El-Saadany, kocha wake wa kwanza.

"Alisafiri peke yake mara nyingi. Fikiria mtoto anaondoka saa 4 asubuhi na kurudi saa 6 usiku. Safari hii ilihitaji mtu mwenye nguvu na malengo ya kweli," aliongeza.

Safari ya Salah ilikuwa kupitia Basyoun, kisha Tanta, hadi Kituo cha Ramses jijini Cairo, ambako alibadilisha tena usafiri kufika klabuni kwa mazoezi.

Baada ya mazoezi jioni, alianza safari ndefu ya kurudi kijijini kupitia njia ile ile.

Safari yetu fupi hadi Basyoun ilikuwa ngumu kutokana na joto kali na hali mbaya ndani ya basi, hivyo unaweza kufikiria jinsi Salah alivyovumilia safari ndefu kama hizi mara kwa mara alipokuwa kijana.

Hany Ramzy, aliyewahi kucheza katika timu ya taifa ya Misri na ligi ya Ujerumani, anaamini kuwa hali hizi ngumu zilimjenga Salah kuwa na akili ya ushindani na mafanikio.

"Kuanza soka nchini Misri ni vigumu sana," anasema Ramzy, ambaye alimpa Salah nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwaka 2011, na pia alimfundisha kwenye Olimpiki za London 2012.

"Nami nilitembea kilomita kadhaa kwenda mazoezini, na baba hakuweza kuninunulia viatu vya mpira," anakumbuka Ramzy.

"Ufanisi wa Salah unatokana na maisha haya magumu hali hizi humjenga mchezaji kuwa imara."

Kapteni Diaa, aliyemfundisha Salah katika timu ya taifa ya vijana ya Misri kwenye Kombe la Dunia la U-20 mwaka 2011 huko Colombia, anakumbuka changamoto walizopitia:

"Wakati huo kulikuwa na mapinduzi nchini, maandalizi yalikuwa magumu sana," anasema.

Anamkumbuka Salah kama kijana mwenye kasi na umakini wa hali ya juu:

"Alikuwa msikivu, hakujibizana, alisikiliza na kufanya kazi. Anastahili kila alichofikia."

Diaa alimtaka Salah asishuke hadi katika safu ya ulinzi, bali aelekeze nguvu kwenye mashambulizi.

Anakumbuka kwa kucheka:

"Katika mechi dhidi ya Argentina, alisababisha penalti kwa kurudi kutetea. Nilimwambia: 'Huwezi kuwa beki! Kaa mbele!'"

Baadaye, Salah alisema kocha wa Liverpool, Arne Slot, alimwambia asirudi katika eneo la safu ya ulinzi"Lakini mimi ndiye niliyemwambia hivyo kwanza!" asema Kapteni Diaa kwa tabasamu.

Katika kijiji cha Nagrig, mama mzee anayeitwa Rashida anasimulia jinsi Mohamed Salah alivyoibadilisha jamii yao kupitia misaada na miradi ya maendeleo.

"Yeye ni kama kaka kwetu, mkarimu na mwenye heshima," anasema Rashida, mmoja wa wanufaika wa Taasisi ya Misaada ya Mohamed Salah.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa taasisi hiyo, Hassan Bakr, taasisi hutoa msaada wa kila mwezi, milo, na pakiti za chakula kwa mayatima, wajane, maskini, na wagonjwa.

Mbali na misaada hiyo, Salah pia amechangia ujenzi wa posta, kituo cha ambulansi, taasisi ya kidini, na ardhi ya mradi wa maji taka.

Anapokuwa kijijini, Salah hubaki mnyenyekevu, huvaa mavazi ya kawaida na hujichanganya na watu bila majivuno.

Wakati Liverpool ilipotwaa taji lake la 20 la EPL mwaka 2025, kijiji kilisherehekea mafanikio ya mwana wao.

Hata hivyo, licha ya mafanikio makubwa akiwa na Liverpool, Salah bado hajashinda taji na timu ya taifa ya Misri.

Misri ilifika fainali za AFCON mara mbili akiwa ndani ya kikosi, lakini walifungwa na Cameroon (2017) na Senegal (2021).

Huku AFCON 2025 ikitarajiwa kuanza Desemba 21, na Kombe la Dunia 2026 kufuata miezi sita baadaye, baadhi wanauliza kama Salah anahitaji kuthibitisha ubora wake kimataifa.

Lakini kwa Mido, nyota wa zamani wa Misri:

"Salah tayari ni gwiji wa Liverpool na Misri. Hana haja ya kujithibitisha kwa yeyote."
 
🚨 Kostas Tsimikas exit, expected to accelerate as Liverpool could also open to potential initial loan proposals.

The left back is prepared to leave as Kerkez and Andy Robertson will be the LBs for Arne Slot.
 
Maelezo ya Arne Slot kuhusu sababu za kufanya mabadiliko katika ushindi wa Liverpool wa mabao 4-2 dhidi ya AFC Bournemouth kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu:

Wachezaji wapya wa majira ya joto Jeremie Frimpong, Milos Kerkez, Florian Wirtz na Hugo Ekitike – ambaye alifunga bao la kwanza – walicheza kwa mara ya kwanza Anfield kwenye mchezo huo wa Ijumaa usiku.

Wanne hao, pamoja na Alexis Mac Allister, walitolewa kipindi cha pili kwa sababu mbalimbali ambazo Slot alizieleza baada ya mchezo kupitia Liverpoolfc.com.

Kocha Mkuu alisema:

“Si kwa sababu tu ya kasi ya ligi, Jeremie alihisi misuli ya paja lake (hamstring) kidogo, hilo ni hatari – hasa ukizingatia kuwa beki mwingine Conor Bradley tayari yuko nje kwa majeraha.

Kwa Joe Gomez ambaye amefanya mazoezi mara mbili tu, sikuona kama angeweza kucheza dakika 30 kwa kasi hiyo, hivyo nilianza na Wataru Endo katika nafasi hiyo, nikiwa najua ningeweza kumuingiza Joe baadaye kwa dakika 10, 15 au 20.

Milos Kerkez anacheza kila pambano kana kwamba maisha yake yanategemea, jambo ambalo ni zuri sana, lakini unapocheza dhidi ya winga mzuri kama Antoine Semenyo ukiwa tayari na kadi ya njano, hilo ni hatari – hasa tukijua pia tunaye Andy Robertson, kwa hiyo hapo ndipo sababu.

Hugo Ekitike alijiunga baadaye kwenye maandalizi ya msimu, anatoka kwenye timu nzuri lakini siwezi kulinganisha na Liverpool wala ligi hii. Kwa hiyo yeye kuweza kucheza dakika 70 tayari ni faida kubwa kwetu – lakini kumchezesha dakika 90 ingekuwa hatari.

Mabadiliko mengine ni Macca, ambaye amekuwa nje kwa miezi miwili au miwili na nusu [na] ameanza mazoezi wiki mbili na nusu tu zilizopita, hivyo bado hawezi kucheza dakika 90.

Na mabadiliko mengine yalihusu Florian mwishoni, hilo lilikuwa kwa sababu nilitaka kumleta mshambuliaji wa kati (No.9) kwa kuwa tulikuwa 2-2.”
 
🚨Liverpool have submitted a second bid of £140 million (€162 million, $190 million) for Alexander Isak.

Isak has informed Newcastle that he wants to leave and join Liverpool, and the situation has escalated.

(Richard Keys - Bein Sports)

If this is true I’d drive him there.
 
Guéhi Could Join Liverpool

Talks Ongoing at Around £35 Million
Liverpool and Crystal Palace are in direct negotiations over the transfer of Marc Guéhi. Liverpool have submitted an offer of around £35 million, while Palace are holding out for closer to £40 million. No agreement has been reached yet, but official reports indicate that discussions are continuing, with the next few days expected to be crucial in speeding up the process.

Contract Situation and Player’s Plans
Guéhi has just one year left on his Palace contract and has shown no willingness to sign a new deal. This situation makes a summer exit highly likely, with Liverpool strongly interested for both sporting and financial reasons.

Strategies and Possible Delays
Some analysts, including Football Insider, have suggested that Liverpool might delay this signing until next year, especially after acquiring young defender Giovanni Leoni. However, Guéhi still appears to be Liverpool’s top defensive target.

Liverpool’s Urgent Defensive Needs
Liverpool are currently short in central defence, following Joe Gomez’s injury and Jarell Quansah’s departure. This makes Guéhi a timely and suitable solution to strengthen the team’s backline.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom