Kwanini Liverpool haitorudi kwenye banter era hata baada ya Klopp kuondoka ni hizi hapa 😄😄😄
1. Miundombinu ya Kisaasa Imewekwa
Liverpool imewekeza kwenye AXA Training Centre moja ya training centre bora Ulaya.
(Dogo Kerkez aliamua kuwadolishia wenzake mitandaoni na mapicha picha mengi 😂😂😂)
Uwanja wa Anfield umeboreshwa na upo capacity ya karibu watu 61,000 hii ni Liverpool ya modern football, siyo ile ya miaka ya Hodgson kuomba matokeo nyumbani dhidi ya Stoke City.
2. Squad Ina Umri Mdogo na Quality
Klopp ameacha kikosi kikiwa young, energetic and hungry akina Szoboszlai, Mac Allister, Gakpo, Nunez, Diaz, wote bado wana miaka mingi ya kilele cha soka.
Mabeki kama Quansah walionyesha Liverpool ina future nzuri bila kusubiri marquee signings. Pamoja na kuwa alishaondoka na kusajiliwa Bayer Leverkusen
3. Liverpool Sasa Inajitegemea Siyo Klabu ya “Hope and Pray”
Zamani Liverpool ilikuwa inategemea miracle season (2013/14), lakini sasa kuna structure na system ya soka inayoendesha klabu hata kocha akibadilika.
Data-driven recruitment, sports science, na analytics department imara Liverpool inafanya maamuzi ya kiufundi sio ya kihisia.
4. FSG Wamejifunza Hawalali Tena
FSG walipigwa sana mkwara kipindi cha Super League na ukimya wa misimu miwili iliyopita, sasa wamefungua investment channels, mfano wameongeza directors bora kama Richard Hughes na Michael Edwards amerudi kusimamia football operations.
Hii inaonyesha wana strategy ya sustainability and success kwa miaka mingi mbele.
5. Legacy ya Klopp Imejenga Character Mpya
Liverpool sasa inajiona klabu ya winners, siyo “just top four.” Hii mentality ya ushindi imejengeka na haiwezi kufutwa msimu mmoja tu.
Hata kwa Slot, pressure ni kushinda makombe, sio tu kuqualify Champions League kama achievement.
6. Wapinzani Wakubwa Wako na changamoto zao
Chelsea bado wanatafuta kocha mwenye identity.
Manchester United wako kwenye transition ya Ineos.
Arsenal bado wanahangaika na consistency.
Hii inafanya Liverpool iwe kwenye nafasi bora ya kubaki juu kuliko kurudi “banter era” ya kumaliza namba 8 na kutolewa na Aston Villa Carabao round ya pili.
Kwa kifupi: Liverpool haitarudi “banter era” kwa sababu siyo timu ya mood swings tena ni taasisi ya mpira wa kisasa yenye winning mentality, system ya scouting, na squad yenye future. Hii ni Liverpool inayopambana kila mwaka kuwin, siyo kujivinjari tu.