Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Attachments

  • IMG-20250605-WA0010.jpg
    IMG-20250605-WA0010.jpg
    60.9 KB · Views: 10
IMG-20250530-WA0036.jpg


MFUMO WA UENDESHAJI WA USAJILI NDANI YA LIVERPOOL

Barry Hunter 🇬🇧 – Kama Chief Scout wa Liverpool (wa kwanza kushoto), Barry ndiye anayesimamia mtandao mzima wa wachunguzi wa vipaji duniani kote. Wachunguzi wote wanaofanya kazi na klabu yetu hutuma ripoti zao kwa Barry, ambaye hufanya tathmini ya kina kuhusu wachezaji wanaopendekezwa. Lengo ni kuhakikisha tunapata wachezaji wanaolingana na vigezo vya kiufundi na kimbinu vya Liverpool.

Mark Burchill 🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 (wa kwanza kulia) – Akiwa mshirika mkuu wa Barry Hunter kwenye Scouting Department, Mark ndiye anayesimamia ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa kutoka masoko maalum ya kimataifa kama vile Amerika Kusini, Afrika, na Ulaya ya Mashariki. Ana jukumu la kuhakikisha taarifa zote kutoka maeneo haya zinachujwa ipasavyo kabla ya kufikishwa kwa Barry. Mark husaidia kuhakikisha ufuatiliaji wa vipaji unakuwa wa haraka, wenye ufanisi, na unaokwenda sambamba na mahitaji ya kiufundi ya klabu.

Julian Ward 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 (wa pili kutokea kushoto) – Julian ana jukumu muhimu katika kuchuja na kuchambua taarifa za awali kutoka kwa Barry Hunter. Akiwa sehemu ya safu ya kiufundi inayoratibu mipango ya muda mfupi na mrefu ya kikosi, Julian hupokea ripoti za kina na kuzilinganisha na mahitaji ya kikosi, kama vile nafasi, umri, uwezo wa kiufundi, na uwezo wa kimbinu wa mchezaji husika.

Michael Edwards 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 – Akiwa Mkurugenzi wa Kiufundi (wa katikati), Edwards anashirikiana kwa karibu na Julian Ward na Richard Hughes ili kuhakikisha kuwa kila pendekezo la usajili linapitia mchakato wa kina wa tathmini ya thamani ya mchezaji sokoni, uthabiti wa kiuchumi, na athari kwa muundo wa kikosi. Kwa kawaida, mapendekezo kutoka kwa benchi la ufundi, likiongozwa na Kocha Mkuu Arne Slot, hutumwa kwake kupitia timu ya kiufundi kwa ajili ya kupimwa kama yanaendana na sera na mkakati wa klabu.

Richard Hughes 🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 – Kama Mkurugenzi wa Michezo (wa pili kutokea kulia), Hughes ndiye anayekamilisha mazungumzo ya mwisho ya kimkakati na kifedha. Mara ripoti na mapendekezo yanapokamilika, Hughes hukaa na Michael Edwards na uongozi wa juu wa FSG ili kuhakikisha kuwa usajili unaendana na bajeti ya klabu, mahitaji ya timu, na maono ya muda mrefu ya Liverpool.

Kwa ujumla, mfumo huu unahakikisha kuwa kila hatua ya mchakato wa usajili – kuanzia ufuatiliaji wa wachezaji, uchambuzi wa kiufundi, tathmini ya kifedha, hadi uthibitisho wa mwisho – unafanyika kwa ushirikiano wa karibu kati ya idara ya kiufundi, scouting, na uongozi wa juu.

Na mara tu makubaliano yanapofikiwa na bodi ya wakurugenzi na FSG, ndipo tangazo rasmi la usajili hutolewa kwa umma.
 
Huo ndio utofauti wa Manutd na Liverpool may be more specific btn SAF na Benitez (and their fans)...

January kipindi ambacho Liverpool walikuwa kileleni kwa jumla ya tofauti ya saba dhidi ya Manutd kwa Benitez he thought tayari one hand washalishika kombe la EPL, akanza ku-pressurize bodi ya Liverpool impe uhuru zaidi wa kusajili despite the fact that tangu atue Liverpool, within 4 years tu amesajili 51 players na ni kati yao watatu tu, Torres, Mascherano na Skritel wana prove consistency till to date. The rest of the players, wewe mpenzi wa Liva u know what they are doing. What happen later sijui, lakini so far so gud Liva ni WATATU nyuma ya Manutd kwa Pointi NNE na ONE game in hand.

Verbal attacks dhidi ya SAF from Benitez it was a wrong timing na mbaya zaidi ni kuwa yeye 'maneno maneno' hayawezi. SAF alimjibu tu short and clear; Pressure itawaondoa tu pale juu na the fate proves him that he was right.

Benitez, with all respect, timu bora na kocha bora huonekana na kile anacho ki-deliver in terms of silverwares na sio kuwa run-up or kutolewa robo final. Sijui ni nini so substantial Benitez ume-deliver Anfield may be na Europe unataka attention ya watu kihivo, CL na FA cup ulibeba kwa kikosi cha Houllier, Liverpool last time wanachukua EPL(hata haikuwa iikiitwa hivyo) it was almost TWO decades ago, deliver first and start talking.

Gud to see that you guys you are counting off Manutd, just wait and see....

I will be there and plz be there too....

One Love One United.....
Hahahaha 🤣🤣🤣
 
Andy Robertson amesisitiza kuwa “si mjinga,” akitambua kuwa Liverpool wanataka kumsajili beki wa kushoto Milos Kerkez, lakini anaamini ana uwezo wa kukabiliana na changamoto hiyo.

Liverpool wako katika hatua za mwisho kufanikisha dili na Bournemouth kumsajili Kerkez mwenye umri wa miaka 21, ambaye anaweza kuwa usajili wa pili majira ya joto.

Hii inakuja baada ya msimu ambao Robertson alikabiliwa na ushindani wa kweli kutoka kwa Kostas Tsimikas kabla ya kurejesha nafasi yake kama chaguo la kwanza.

Ingawa dili la pauni milioni 45 kwa Kerkez linatarajiwa kusababisha kuondoka kwa Tsimikas, linaathiri pia nafasi ya Robertson kuendelea kuwa chaguo la kwanza katika kikosi.

Akizungumza na BBC Scotland, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alisema:
“Sisi si wajinga, inaonekana kama dili linaweza kukamilika. Lakini hadi litakapokamilika, sijalipa hata mawazo ya pili. Najiamini. Nina imani na uwezo wangu na hilo ndilo linaniongoza mbele."

“Nimekuwa na miaka minane mizuri sana Liverpool kwa upande wa kushinda makombe na kuwa mchezaji wa kudumu kwenye timu, jambo ambalo najivunia sana.
Siwezi kubadilisha umri wangu, lakini bado naamini nina mengi ya kutoa na hilo ndilo ninalipa kipaumbele. Najikita kwangu mwenyewe – huwezi kujikita kwa watu wengine au unaoshindana nao.”

Ingawa Kerkez analetwa kama sehemu ya mpango wa mrithi wa muda mrefu wa Robertson, taarifa zinaeleza kuwa kwa sasa atashindana na Robertson kuwania nafasi ya kuanza mechi.

Hili linaeleweka ukizingatia umuhimu wa Robertson kwenye kikosi cha Arne Slot, ingawa msimu uliopita alionekana kuwa mchezaji aliyepungua kiwango miongoni wachezaji waliotumika zaidi.

Kuwasili kwa mchezaji mpya kunaweza kuchochea tena kiwango cha Robertson, ambaye alitimiza miaka 31 mwezi Machi, na Arne Slot anaweza kufurahia ushindani wa aina hiyo. Kuwa na wachezaji wawili imara katika nafasi moja ni ndoto ya kila kocha wa kiwango cha juu, hasa kama mmoja ni mrithi tayari aliyezoea mazingira na anayesubiri kuchukua nafasi wakati ukifika.

#_anfield1892_kiswahili_updates
 
Mechi ya leo ni moja ya ushahidi kwa nini Liverpool, inashindwa kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu ya England kwa miaka 18 sasa: Wanaangalia zaidi kushinda mechi moja moja dhidi ya vigogo ili kufurahisha fans wao kuliko kuwa na mikakati makini na mahesabu kuchukuwa ubingwa. Kwa mfano Msimu huu Man wamefungwa na timu vigogo tu, yaani Arsenal na Liverpool, lakini siyo zile vibonde ambazo ndizo za kujichotea pointi.

Liverpool imefungwa na timu vibonde tu msimu huu -- M'Borough na Spurs na kutoka sare na timu nyingine 10, nyingi zikiwa vibonde. Kuchukuwa ubingwa siyo kuifunga Man au Chelsea tu (ingawa ina raha yake hasa kwa fans). Kuchukuwa ubingwa ni namna ya kuweka mikakati ya vipi kujilimbikizia pointi katika mechi 38.

Kila msimu kuna mashindano manne yaani PL, CL, FA Cup na carling Cup, lakini inavyoelekea hawajui priorities zao na in the end hutoka kapa kila baada ya msimu. Bila shaka mashindano kama vile FA Cup na Carling yanawachanganya. Hapo ndipo Mzee Fergie huonyesha umahiri wake.

Leo Liverpool wamepata ushindi mnono dhidi ya Man, tena kwao na wataushangilia sana ushindi huo huku wanajua kuwa Man watacheka mwisho kwani sasa hivi kilichobakia ni kila timu kuiombea nyingine ifungwe katika mechi zilizobakia -- kitu ambacho ni mtihani zaidi kwa Liveropool kuliko Man. Kwa mfano Man wanaweza kuafford kufungwa hata mechi mbili kati ya zilizobakia (nafikiria Man City na Arsenal) na bado wakaibuka mabingwa.
Hahahaha 🤣
 
🚨 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: Liverpool are set to complete Wirtz deal in next days, 𝐡𝐞𝐫𝐞 𝐰𝐞 𝐠𝐨 𝐬𝐨𝐨𝐧! 🇩🇪

Negotiations at final stages for package over €130m, details being sorted then Wirtz will travel for medical.

The German star has already all agreed with Liverpool for personal terms, just waiting to get the deal signed.
 
Habari mpya Ndani ya klabu ya Liverpool nikwamba Utambulisho wa wachezaji wapya wawili wanao tarajia kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Liverpool Florian Wirtz na Milos Kerkez unaweza pishana kwa siku chache au masaa

Kwa Sasa Liverpool Wana andaa mazingira ya Vipimo vya afya Kwa wachezaji hao Wawili alafu Utambulisho wao utafuata Kwa mpangilio maalumu , huenda Utambulisho wa Milos Kerkez ukawa wa haraka zaidi alafu Florian Wirtz ukafuatia .

▪️Tukae mkao wa kula Wanangu wa Liverpool
 
Habari mpya Ndani ya klabu ya Liverpool nikwamba Utambulisho wa wachezaji wapya wawili wanao tarajia kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Liverpool Florian Wirtz na Milos Kerkez unaweza pishana kwa siku chache au masaa

Kwa Sasa Liverpool Wana andaa mazingira ya Vipimo vya afya Kwa wachezaji hao Wawili alafu Utambulisho wao utafuata Kwa mpangilio maalumu , huenda Utambulisho wa Milos Kerkez ukawa wa haraka zaidi alafu Florian Wirtz ukafuatia .

▪️Tukae mkao wa kula Wanangu wa Liverpool
enheeee hizi ndo habari nazopenda kuziona, na sio GB zinakata kwa upuuzi wa tiktok
 
𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: Liverpool are set to complete Wirtz deal in next days, 𝐡𝐞𝐫𝐞 𝐰𝐞 𝐠𝐨 𝐬𝐨𝐨𝐧!

Negotiations at final stages for package over €130m, details being sorted then Wirtz will travel for medical.

The German star has already all agreed with Liverpool for personal terms, just waiting to get the deal signed.
130? Mmepigwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom