MSIMU ULIISHA KABLA HAUJAISHA.
Kwangu msimu wa Liverpool ulimalizika mechi ya Utd FA cup, toka pale niliona hali itakuwa mbaya sana. Mimi ni muumini wa mpira mzuri, sasa kwa tulivyocheza bila PASSION, AGGRESSIVE, COMMITMENT, we were like hey we will score anytime. Tulipoteza loads of chances bila hata kuonesha ishhh.!!!! WTF
Utd waliitaka ile mechi kuliko LIVERPOOL alivyoitaka. That match was supposed to be put on the bed only 1st Half kwa Liverpool. Utd walikuwa tayari baana eh tufungeni tu mnaweza kuliko sisi, tukashindwa, walipopata magoli wakaona ahaa kumbe its possible lets pushing guys BOOM wakafanikiwa. Again Klopp alizingua ile mechi kwa subs zile.
Mechi zilizofuata yalikuwa yale yale tu nothing new, nikaitoa LIVERPOOL kwenye mbio za ubingwa maana sikuon mabadiliko yoyote ya kimbinu wala kiakili. Wachezaji wanacheza wakiwaza next season itakuwaje? Hawana future baada ya Klopp na jopo lake kuondoka (its a massive clear out, mpaka wapishi wanaondoka), je kama ni wewe utakuwa na utimamu wa akili? Jibu ni Hapana, even Klopp ni kama alishaumaliza msimu tayari kwenye mechi ya Palace (0-1).
Anyway mambo kadhaa naona yametuporomosha kutoka quadruple mpaka kubaki na kikombe kile cha CARABAO.
1. Klopp’s issue
Lawama namtupia Mr.JK kwa sababu kutoka season inaanza tulikuwa na magonjwa kadhaa a) defensively as a team and poor performance 1st half. Hapa akatupa na jina “MONSTER MENTALITY” tukaona Yes, sisi ndio mashujaa tunaweza kutanguliwa na tulamsulubu mtu, tukachukulia ni sehemu yetu ya msimu huu. Mimi mmoja wapo niliona YES sisi ndio wababe YNWA”, kumbe tunapika BOMU na limekuja kulipuka mwishoni, quadruple ileeee.
Ni ngumu sana kuwa bingwa huku mara 21 umetanguliwa kufungwa kati ya mara 35. Record mbovu sana hii mbaya sana hii. Hatustahili kubeba EPL kama vile ambavyo tayari imeshatokea. Arsenal deserve alot especially 2nd round of the season. They are deserving ahead of City but always City is City, Pep is just Pep anapoona kuna uwezekano.
Klopp alishindwa kuiset timu yake kimkakati, unajua ukituangalia tunavyofikiwa kwenye final third kiwepesi na baaada ya hapo ni mipira inapenya nyavuni tu kwa sababu tunakosa hata Individual brilliance. Kwa nini inakuwa hivi? Patterns zetu zinakuwa mbovu sana, Hatuna mapafu ya mbwa pale kati, tayari Endo amechoka (excessive game time) Szobo isnt the same too, Jones amerudi kwenye asili yake ya kichezaji (to hodl ball too much even kwenye moves za maana). Graven akili inataka mwili hautaki, Macca
ndio kiungo tunayemtegemea zaidi, akifuatiwa na ELIIOT akicheza as RCM na akitokea sub. Nafikiri ilikuwa vyema Klopp acheze na double pivot (Endo & Macca, Endo as anchor and Macca as Play marker) kisha mpr Szobo free role offensively, change 4-3-3 to 4-2-3-1 uangalie itakulipa au lah.!!
Mpira wa Klopp ni SPEED & ENERGY ila kwa Sasa mwenye uwezo wa kufundisha matumizi ya SPACE & TIME anafanikiwa zaidi. (Pep, Arteta,Amorim, Alonso, De Zerbi n.k) kwa Klopp imekuwa tofauti kidgo.
Embu angalia Liverpool wakicheza halafu angalia na timu kama City, Arsenal, Brighton, Fulham, angalia moves zao ni za hatari kuanzia build up mpaka final third ya mpinzani. Sasa inatokana na uwezo wa kocha kuunda patterns mbali mbali za miondoko. Liverpool tukicheza kila mchezaji lazima atapigiwa pasi atapokea atakaa nao atleast 1-2 seconds, wengine watatumia even 2-4 seconds hawa ni attackers wetu. Sas tunakosa hizo moves za hatari kwa kishindwa kutumia SPACE & TIME vyema.
Klopp yupo na sisi kimwili ila kiakili hayupo nasi. Toka game ya FA mpaka ya Westham hatujabadilika kitu kiuchezaji. Aisee ilibidi nimuelewe Klopp na kauli ya kuishiwa nguvu ya kufundisha ni 100% True tusimuhukumu hata kidogo. Angalia Line up vs Atalanta, angalia subs zake dah.!!
Nafikiri niseme tuThank You Klopp for everything, ulitupa furaha na huzuni japo furaha ilidumu kuliko huzuni. Best of luck.
2. Kwa wachezaji.
Pamoja na Klopp na mapungufu yake yakujirudia rudia (2020/2021) last season na msimu huu, ila kwa sasa lawama wabebe wachezaji nao kubwa tu.
Embu angalia mechi ya utd EPL (Nunez alivyokosa)
City at Anfield (Diaz with one Glorious chance and second chance looks min glorious chance) Gakpo vs City vs Utd Yaani hii imeenda mpaka kwa Salah toka arudi kutoka injury hajawa Salah yule yule anakosa magoli ya kipuuzi, anapiga mashuti unashindwa kuelewa ndio anajifunza kucheza au ni mzoefu huyu? Jota (clinical ila injuries sasa dah.!).
Kuna moves tunazitengeneza za 5v2 4v2 lakini end product ni 0. Ila cha ajabu kwetu inatokea 4vs 3 lakini tunaruhusu, yaani tuna wachezaji wanne kwenye eneo letu la mwisho na wapinzani wapo watatu ila wanafunga. Ndio ile inaitwa MWAKA WA NJAA.
Ona hizo chances. Yaani hakuna mchezaji ana nafuu awapo golini wanakosa utulivu wa akili.
Hii picha nimeambatanisha huko juu kwenye maelezo ya shida ya Klopp, ona hao Fulham walivyonipanga, kawaangalie Atalanta both matches, angalia, palace, Everton miundo ni hiyo hiyo tu. Hapo wana deal na wachezaji wawili tu ENDO na Macca Basi kina Vvd, Quansah, Konate, Robbo, Alison watajipigia mipasi weeeeee wao wakipata ni quick moves tayari tumefikiwa.
Anyway Thanks Klopp anaondoka kwa sababu hawezi kutu offer kingine kipya.
YNWA.