Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Acha tupambane ya hali yetu 😀 ila kabla ya dirisha la usajili kufungwa tukifanikiwa kuleta CDM na LCB wa ukweli tunarudi kupambana na City pale juu. Balaa ni kama tutafeli kusajili hizo sehemu mbili, naona kama tutaendelea kucheza Europa na msimu ujao.
 
Diaz sio wa kumtegemea timu ikiwa inasaka ushindi. Ana mambo mengi sana uwanjani hasa akiwa kwenye box.
Mnyama ni Jota hana mambo mengi kabisa. Kwaiyo foward yetu ya kutegemea ni Jota, Salah na Gakpo.
Gakpo[emoji7][emoji91]
Salah akishaliotea goli jamaa ni katili sana,ananyanyasa adui hadi adui anatamani kumpiga ngumi.

Diaz chenga nyingi aonekane fundi sana wa kupiga kama spider...sema ni fundi hata hivyo,mfia timu.

Jota hatabiriki kabisa
Anaotea otea tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nketiah mbona anawarudisha champions league fresh tu
 
Kwa mapungufu yote hayo uliyotaja hebu nitajie kocha gani mwengine angeweza kukibebea hiki kikosi mpaka hapo alipofikia yeye tu! Tatizo hapa ni FSG wabahili! hata hao wachezaji wazuri tulionao tuwewanunua kwa kuvizia e.g. Salah, Mane etc. wote wamekuwa wakubwa kwenye mikono ya Klopp.

Bila ya klopp kamanda na sisi tungekuwa kama Chelsea kama sio Everton.
 
Tu

Tunachompendea Nunez urefu na speed nketiah hana na hatokuja kupata, mapungufu ya nunez ni machache sana kulenga goli kuliko huyo nketiah
Kweli ila Nketiah Yuko clinical kulingana na nafasi anazopata.

Halafu Kuna lingine kuhusu Klopp.

Jamani mnamzeesha na kumsababishia presha huyo kocha. Jamaa ni bonge la kocha ila kukosa funds kunafanya amalize career yake vibaya. Mnaonaje mkitupa Klopp aje awe assistant wa Arteta wajichotee Kwa pamoja makombe yote. Sisi si umeona tulivyo vizuri kifedha? Yaani mkwanja mfuko wa shati.
 
Shida yake Klopp ni kwamba hicho kitendo Cha kukosa Fund naye anakifurahia ili ajitwalie umaarufu wa kutenda miujiza ya kufanya njia pasipo njia.


Unadhani mtu kama Pep angekuwa Liver,angekubali na kuchekelea upumbavu wa wajinga FSG kwamba hela hakuna?
Uandhani angetoa zile kauli alizokuwa anazitoa Klopp mwanzo wa msimu uliopita kwamba hakuna haja ya kusajili MF,tunao wa kutosha,yupo Keita,yupo Hendo ,yupo sijui nani,wengine wa nini?

Klopp naye ni mjinga bwana,msimtetee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anajitahidi tu kufuata nyayo za role model wake, Arsene Wenger, mwamba mwenye sanamu lake pale Emirates. Mwamba aliyejenga uwanja mpya Kwa pesa za mauzo ya Anelka. Mwamba aliyepandisha propert prices za Ashburton Grove. Yaani Kwa kifupi Wenger ni The Boss. Sasa si mmuacheni Klopp aje kuendeleza Legacy ya Le Prof?
 
Ni mpumbavu kama wapumbavu wengine asipotaka kubadilika na kujidai baba miujiza wakati msimu wa miujiza ushaisha
Mpira hautaki tena janjajanja za miujiza .
 
Tatizo la Liverpool ni Anold sema ni ngumu kufahamu hadi uangalie mechi nyingi kwa umakini, huyu dogo anapopanda tu lazima tufungwe. Tafadhari bora tuwanyang'anye Chelsea Reece James kwisha...
Dah upo sahihi kabisa! Trent anapaswa kuwa winga au awe-paired na very good CDM kama Tchuameni au Caicedo, nyuma yao kuwe na strong CBs vilele, otherwise atatufungisha siku zote eirther directly au inderictly kwa kuwapa kazi kubwa wenzake wanaomzunguka.

Kiufupi anawafanya wenzake muda wote wacheze kama tupo pungufu kwa mtu mmoja vile. Konate inabidi acheze RB na RCB. CDM inabidi acheze kama lone CDM wakati juu yake kuna two box to box (mzigo mkubwa wa kuwalinda CBs and kupatrol midfield area at the same time.

Fabinho ali-shine alipokuwa anacheza na Wijnaldum na Hendo kwa kuwa Wijnaldum alikuwa anafanya kazi ya kuharibu na kutuliza timu wakati yeye anasafisha, hendo anabakia box to box peke yake. Msimu ule defence ilifanya vizuri kwa kuwa tulikuwa na key strong person kila idara i.e. Allison, Virgil, Fabs, Winaldum.

Msimu huu tunaenda kucheza na box to box wawili i.e. Macca na Szobo, CDM mmoja ambae mpaka sasa hatujasajili specialist, huyu itabidi acheze kama lone CDM kwakuwa his partner Trent ni mzururaji hovyo. Hapa tukishindwa kuzuia kutokea mbele tu basi chance ya kufungwa kwa kila shambulizi ni close to 50% kwasababu ni rahisi CDM and defence kuwa out of position.
 
Hakuna muongeaji sana anayepata mafanikio kwa muda mrefu,

Ni kocha mzuri ila anaendesha timu kwa mahaba na hisia mno kuliko uhalisia, tukipata roho ngumu tutawaachia
 
Mi nadhani he is just being proffesional, kuna makala moja nilikuwa nasoma leo inadai privately amechoshwa na lack of signings na atafikiria his options ikiwa FSG hawatompa support kwenye usajili msimu huu, inaonekana kama ana-consider post ya Germany national team .

Binafsi naamini kunaweza kuwa na ukweli coz jamaa alisema mwisho wa msimu uliopita kuwa anataka kufanya overhaoul ya midfield mapema ili apate muda wa kutosha kufanya nao kazi pre season kitu ambacho hakujatokea zaidi ya wachezaji wawili tuliosajili.
 
Ni mpumbavu kama wapumbavu wengine asipotaka kubadilika na kujidai baba miujiza wakati msimu wa miujiza ushaisha
Mpira hautaki tena janjajanja za miujiza .
Pamoja na hayo. Jamaa ukocha anaujua sana. Naweza kusema kimbinu huenda yeye ndiye kocha Bora kwenye ligi. Akifuatiwa na kina Pep na Arteta na akimuacha mbali 7hag aka Dutch David Moyes.
 
Anold ata winga hawezi, nilibaini hilo siku ya mechi na bayern na wale wajerumani wengine alichezeshwa kama kiungo akapotea na siku ya bayern ndipo kabisa maana hadi coman anamzidi mbio.

Tena siku hizi anatembea kama ameota majipu mapajani, suluhisho ni mtu wa kumnyang'anya namba tu hakuna lingine. Waingeleza wenyewe waliisha mnyang'anya namba ni mwendo wa sub kwenye timu ya taifa.
 
Hakuna muongeaji sana anayepata mafanikio kwa muda mrefu,

Ni kocha mzuri ila anaendesha timu kwa mahaba na hisia mno kuliko uhalisia, tukipata roho ngumu tutawaachia
It seems like the grass is always greener on the other side.

Sisi title contenders Arsenal pamoja na Manyumbu, Chelkenge na hata Citeh wote tunamkubali sana Klopp na ukituambia tumchukue, haswa Manyumbu, ni fasta tu.
 
😄😄 Tena morinho ndiyo angewananga sana yaani sioni mchezaji yeyote ndani ya hao waliosainiwa wanazidiwa na timu ya watoto wakina koumas, Quansah na ben doak
 
Hili swala la kutowapanga wachezaji kwenye namba zao asili namchukia zaidi sijui kwanini anasajili.
 
It seems like the grass is always greener on the other side.

Sisi title contenders Arsenal pamoja na Manyumbu, Chelkenge na hata Citeh wote tunamkubali sana Klopp na ukituambia tumchukue, haswa Manyumbu, ni fasta tu.
Shida siyo kumkubali
Shida Kuna upumbavu anaendekeza ambao unachangia tunakwama.

Klopp has the option to be better than now
but the bad thing is that he does not want to use it ,instead he's depending on miracles.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…