Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Ni kweli Julian Ward ametoa notisi kuodoka na pia Ian Graham mkuu wa utafiti nae vile vile anaodoka.

Hii habari imewastua mno Liverpool kwa sababu sio siku nyingi ameodoka Edwards na huyu dogo kumridhi sasa hata kabla ya msimu haujaisha huyo anasepa zake.

Amesema japo anaodoka ni kwamba hana mpango wa kuajiriwa popote hivi karibuni.

YNWA
 

Hii taarifa ni kweli. Ward end of the season anaondoka. Yeye ameamua kukaa pembeni kimpira na sio kuondoka tu Lfc. He has personal issues.

Za chini chini inasemekana huenda mmiliki mpya ameanza kujilikana hivyo mabadiliko na mipango tofauti itatokea. Mkuu wa utafiti wa klabu naye ataondoka. Huenda kuna ka ukweli maana Klopp kwa sasa hana ya kusema β€œwe will sign but if the right player is available” Hana ile kuficha ficha tena. Anasema tunahitaji kusajili.

Swali la kujiuliza, ilikuwa bobby aondolewe summer hii, nini kimepelekea bobby kupewa mkataba mpya? Kama FSG wameshaweka timu sokoni je, wao wanahusuka na mikataba players kubaki?

Huenda tukashangazwa na watakaondolewa.
Ox
Milner
Keita
Hawa mkono wa kwa heri unawahusu.
 

Naungana na wanaohisi mmiliki mpya huenda amepatikana.

Klopp anajiamini kutamka usajili (tunahitaji kusajili)… kitu ambacho kilikuwa nadra kukiona huko nyuma kabla klabu haijawekwa sokoni.
 
Naungana na wanaohisi mmiliki mpya huenda amepatikana.

Klopp anajiamini kutamka usajili (tunahitaji kusajili)… kitu ambacho kilikuwa nadra kukiona huko nyuma kabla klabu haijawekwa sokoni.
Klopp hua na siasa nyingi sana. Alishajua kwa FSG alikosea sana kwenda nao mwendo wa kujibana hivyo hapa anatuma ujumbe kwa wamiliki wapya wakija waelewe kwamba hakuna sell to buy tena mbali ni buy buy buy...

YNWA
 
Hao uliowataja hata bure wasepe tu.

YNWA
 
Safi sana
 
Ward & Graham wataondoka mwishoni mwa msimu, Hunter pia ataondoka nadhani.

Klopp, alikuwa na last say kwenye transfers, but kwa miezi michache iliyopita amechukua power zaidi kwenye upande wa Transfers.

Ishu ya Mike Edwards kuondoka ilikuwa ni kufanya kazi under tight budgets za FSG, na kingine kikubwa zaidi ni MAPISHANO baina yake na Klopp kuhusiana na new contract ya Henderson, Edwards wanted Hendo gone, but Klopp refused, na tangia hapo kukawa na rifts, Klopp akaanza ku-overturn kila maamuzi ya Edwards, tofauti na walivyokuwa wanafanya kazi mwanzo.

I think kwa Ward inaweza kuwa the same, maana Klopp refused plan Bs zote za Ward kuhusiana Tchouameni (Nunes, Vitinha etc)

But on the other hand, yawezekana labda suala la takeover linaweza kuwa limefikia sehem nzuri, na new owners wanakuja na model yao AU kuna internal conflicts (power struggles) at the club, YOTE YANAWEZEKANA.

But, kwa 100% kuondoka kwa Edwards, then Ward na Graham, kunatoa picha pana zaidi kuhusiana na mgawanyiko wa majukumu at LFC, kama Edwards, Ward & Graham wanaondoka LFC kutokana na kuhisi kutokuwa valued na coaching stuff, especially Klopp, then muelekeo tunaoenda nao ni m-baya na utatuumiza, but tuombee tu iwe ni new owners, na suala nzima la kubadilisha model ya usajili.
 
Sitaki kusema mengi, but Klopp anampa power kubwa sana Lijnders, na inatuumiza.

I know tusingefika hapa bila Klopp, but Edwards & Ian Graham wame-play part kubwa sana kwenye mafanikio ya Club, na hii mara nyingi inatokea kunapokuwa na mgawanyiko mzuri wa majukumu, Edwards ndiyo kawaleta LFC kina Salah, Mane, Alisson, Fabinho, Robertson, Kostas, Jota, Shaqiri, Wijnaldum etc, when Klopp came in at LFC, his first choices kwenye attacking dept walikuwa ni Brandt & Gotze, he wanted Jonas Hector kwenye upande wa RB, Zielisnk at CM, and i'm not saying kuwa Klopp asingewa-improve hawa wachezaji kama alivyofanya kwa kina Salah & Mane, but kupitia hii scenario unaona ni jinsi gani inavyo-matter kuwa na transfer department nzuri, because plan Bs za Edwards & Graham (Salah, Mane, Gini, Robertson) ndiyo zimetufikisha hapa, hii inamaanisha kazi waliyokuwa wanaifanya ni nzuri na ya uhakika, ndiyo nilishangaa Klopp alivyokataa Plan Bs za Ward this summer, je anaweza kuwa Lijnders ndiyo alizikataa?

Lijnders ni assit. Coach but kila siku anazunguka kwenye medias, sidhani kama tunaona assit. coaches wa City, Utd, Chelsea, Arsenal etc wanazunguka kwenye pressers kila siku, matter of fact wengi wetu hata hatuwajuhi assit. coaches wa hizi Clubs, but Lijnders mara aandike kitabu kuelezea our training drills na how tunajiandaa na games, mara aende kwenye medias kuongea upuuzi, Buvac ulikuwa hata humskii kwenye medias, sishangai kuna hizi tensions za kutosha ndani ya Club, kuna watu wamepewa power kubwa sana at the Club, ambayo hawastahili.

I love Klopp, but kama kuondoka kwa hii mizizi iliyomsaidia sana off the pitch kunatokana na migogoro ya ndani kwa ndani, atapotea na ataipoteza Club, he needs to fix up, he needs to fix this na bad enough reports zinasema Klopp tried so hard kumuomba Ward abaki at the club, hapo unaona tu kuwa its not Klopp, kuna mtu kapewa power kubwa na anaharibu vitu.

Moyo wangu unaniambia kuwa ni suala linalohusiana na new takeover, because sitaki kuamini kuwa Club ina-fall apart internally.

Ward alikuwa in Qatar juzi tu, kushughulikia deal ya Caicedo, na bado anashughulikia deal ya Jude behind the scenes, alianzisha mazungumzo na Camp ya Enzo Fernandez tayari, sasa sijajua tunaelekea wapi baada ya hapa, ndiyo maana nataka kujiaminisha kuwa hii fiasco yote ni kutokana na new takeover, na i pray niwe right.
 
Mahala popote kazini ili mambo yasonge lazima mipaka ya kazi iheshimiwe lakini kukiwa na mfanya kaze kimbelembele kazi hua inaharibika sana na utaona hapa kwa tetesi unazo sema kuna muingiliano wa kazi pengine na majukumu ya hawa supporting staff wetu... Lijnders kweli kigeugeu huyu ndio alietuaminisha usajili wa June 2022 unaedana na dhana kwamba tunatoka kutumia 4 3 3 attacking akisema hii ishajuliwa na wengi na kuhamia kwenye mfumo mpya unaoedana na usajili mpya matokeo yake tupo nafasi ya "ajabu" tukipigika mpaka na mshika mkia N Forest.. Kwa maana nyingine ni kwamba huyu msaidizi anatoa taarifa kuchwani bila kuweka maneno ya akiba.

Edwards ni moja ya wafanyakazi waliofanya makubwa Liverpool bila kutaka credits yaaani jamaa alikua ni yeye na laptop yake tu na kazi kazi... Alifanya mengi mazuri kuliko mambaya na bila input zake wala hii klabu isingekua ilipo... Akaja Ward ana network ya kutisha nchi zenye wachezaji wa maana sishangai kusoma Klopp alilkomaa sana jamaa abakie kwenye nafasi yake lakini amegoma na anasema ana achana kabisa na ishu za mpira kwa sasa mpaka baadae. Sio kawaida ya hawa wenzetu kukumbali kazi aafu aachie ngazi kabla hata ya kumaliza mwaka.. Inaonyesha kuna tatizo mahala ama mmiliki mpya anakuja na mkakati wake kama kashapatikana na kwa hawa jamaa wawili Edwards na Ward ni top cream young behind the scenes gurus popote pale watapata ajira wakihitaji kwa kua credentials zao zinajitosheleza....

Ward kwa sasa atuachie zawadi murwa sana atatua changamoto pale katikati angalau anunue wawili wa kuingia 1st 11 huku akiwatema Henderson, Milner, Keita, Oxlade-Chamberlain ili tuanze upya kabisaaaaaa.

Muda utasema usishangae na Klopp akavutiwa na project ya Barcelona πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…akasepa zakeπŸ€”πŸ€”

YNWA
 
Ngoja tumchukue Michael Edward summer pindi Mapumziko yake yatakapokuwa yameisha[emoji16][emoji16] aje atufanyie kazi watoto wa darajani
 
Ngoja tumchukue Michael Edward summer pindi Mapumziko yake yatakapokuwa yameisha[emoji16][emoji16] aje atufanyie kazi watoto wa darajani
Darajani bhana mbona mshamaliza hayo mambo, nyie mmechukua supporting staff wa Brighton karibia wote.


YNWA
 
Haha tunaplan tofaut,
Lengo nikuhakikisha tunampata Edward hata kama tumewapata hawa matechnical director kutoka Brighton,Monaco na Liepzig

Edward aje kuwa Sporting Director
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ Kwa kweli mkipata huyo bwana Edwards mtakua tishio balaa.

Sie hapa tumpate Monchi ndio tutakwenda sawa tu.

YNWA
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kwa kweli mkipata huyo bwana Edwards mtakua tishio balaa.

Sie hapa tumpate Monchi ndio tutakwenda sawa tu.

YNWA
Ngoja tuone ila mpk sasq tumepata ma Technical director wazuri, nadhan hata Edward akija hatopata kazi ngumu.

Japo tulikuwa na mfumo mbaya wa usajili tangu aondoke Emiliano tumehangaika sana.
 
Ngoja tuone ila mpk sasq tumepata ma Technical director wazuri, nadhan hata Edward akija hatopata kazi ngumu.

Japo tulikuwa na mfumo mbaya wa usajili tangu aondoke Emiliano tumehangaika sana.
Kwa kweli kwa sasa huyu Yankees hakutaka kubahatisha na usajili tena amesuka kiksosi kamili sana cha kazi na soon mtaanza kuona matunda powa sana... Timu inasukwa na kua idara yenye mbinu tofauti za usajili na wenye kua na mawasiliaono powa na kocha..

Kwa sasa hatujui sie tutaamkia kwa nani hakuna cha Ward wala Edwards

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…