Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool ilikua Gerrard na Gerrard alikua Liverpool kimsingi tangu mwaka 2004 dogo alikua anaibeba hii timu kama mali yake, alicheza kwa kuchomwo sidano ili mradi awe uwanjani kuwaamshaamsha wachezaji wenzie na mashabiki kusaka ushindi...

Ndio maana hua nikisikia eti anafananishwa na akina Henderson hua nabakia kutoa macho kama fundi saa maana ni kama maji na oili hawa wachezaji ni tofauti kabisa...

Alikua nebo ya timu ndani na nje ya uwanja akiwakilisha vyema klabu yake pendwa.

Mourinho hakuficha kiu yake kutaka kufanya kazi na Steve akiwa Chelsea na baadae Los Blonco.

Maajabu sasa hawa ma beberu walivyoinunua timu na kuja na mikakati mpaka kumtema Steve huku akiuliza nyongeza ya mkataba kwa msimu mzima bila Rodgers kumpa jibu hakika ilikera sana alivyoodoka Steve lakini ndio maisha na sasa katupa kete yake kwenye ukocha ana safari ndefu lakini ndoto yake ni kutua Liverpool 1 day kama gaffer pengine mridhi wa Klopp.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…