Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Kwa Sasa liverpool ni timu Bora sana muko kwenye peak na hii chance kwenu ya kufanya vizuri msimu huu ..hongereni kwa Hilo ..sisi Chelsea bwana alaah tunajipanga msimu ujao.
#CFC[emoji170][emoji170][emoji170]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Darwin Núñez on potential Premier League move in the summer: “I really don’t know what’s gonna happen. But I’m not gonna speak about my future before the end of the season”. [emoji1257] #transfers

“Cavani - he’s my idol”, Darwin also added. Benfica want around €75/80m to sell Núñez.
 
T
Asante mkuu kwa majibu
 
Tatizo unaongea kwa kuangalia mpira kwenye tv ushawahi kwenda hata Ethihad acha zako game yetu uliomba iishe kwa ile sare acha ushabiki wako ongea kimpira wewe
Alafu huyu ni kama OllaChuga Oc ambaye huangalia mpira kwakutumia Livescore achana nae [emoji1787][emoji1787]
 
Tatizo unaongea kwa kuangalia mpira kwenye tv ushawahi kwenda hata Ethihad acha zako game yetu uliomba iishe kwa ile sare acha ushabiki wako ongea kimpira wewe

Ule moto tuliowawashia unasema niliomba draw ?

Wewe umeshaenda anfield mara ngapi ,post picha hapa ukiwa anfield vinginevyo wewe ni mamruki tu unatafuta sifa ....

Narudia Tena post picha ukiwa anfield...!!!!!!!!!!!!!!!😕😕😕😕
 
Klopp huyu amgempata huyu dogo Darwin na Bissouma tutakua fire sanaaaaa. Nadhani hata jibu la ile high line lingepatikana maana dogo pamoja na urefu ni mwepesi balaa pia anakaa na mpira vyema sana kusubiri wengine watue mashambulizi yaanze.

Manchester City wakimkosa Erling Hallaad naona wakishuka mazima kwa huyu dogo Darwin.

Come on Klopp sapraizi us.

YNWA
 
Hili la kutopata ushindi nyumbani kwa Klopp ni kama vile ni "dead rubber " maana anakua kashapata ushindi ugenini hivyo Anfield anakua anamaliza tu ratiba kuvuka hatua ya inayofuata.

Gemu ya Benfica ilikua kile kikosi hata hakijawai cheza pamoja ki ukweli sikutegemea hata tutoke sare nao maana unavyoweka pedestrian MFs ya Keita, Milner na Henderson lazima maumivu yawepo na ukitazama vyema magoli yote ilikua MF hawako in position ya kuzuia zile kaunta.. Kimsingi hata Benfica wenyewe hawakuamini kukutana na kile kikosi aisee.

Mkuu ukiwa na CMF butu kama ya Liverpool minus Thiago unategemea basi LB na RB wawe watengenezaji wa nafasi kwa ma straika wako ndio maana hat ile gemu dogo Tsimikas katoka na assist nadhani 2. Mpaka pale Klopp atapata ACMF ndio tutapata jawabu la haya mambo ya high line otherwise namsapoti mpaka sasa. Kingine pia Bremer wa Torino lazima atue pale nyuma panahitaji a real bull tuko softi sanaaa aisee. Baada ya kumpata Fabio ngoja tuone kama ni 4 3 3 attacking ama ni 4 3 2 1 msimu ujao...

Kuanzia robo fainali nani anavuka mpaka kufika fainali inategemea pia na bahati maana kama El Cholo wakicheza mpira sana yaaani kwa mara ya kwanza nimeona Pep akibadilika kabisa kutoka na ule ubishi wake na kukumbali kuweka maslahi ya timu. Ingekua na Pep wa zamani ile gemu walikua wamefungwo kabisa lakini sasa aidha ameamua kuja kivingine akianza Jumapili ile vs Liverpool Kimsingi alituvuruga na kucheza mchezo wetu yaaani ilituvuruga sanaa maana kwa kawaida Pep hua ni muumini wa kumiliki kila eneo la uwanja lakini kwa sasa anachofanya ni amiliki pale kati na mipango yote ya mpinzani inakufa. Sasa kwa uchezaji huo nayo bahati na kipa kujituma lazima muda wote. Utabiri wangu naona Liverpool vs Manchester City tutakutana pale Paris kufunga mjadala nani kidume msimu huu.

YNWA
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tunaishia tu kuassume kwamba Chelsea naye angekuwepo.
Aisee Mendy alichowafanya sicho kabisa[emoji23]
 
Kwa Sasa liverpool ni timu Bora sana muko kwenye peak na hii chance kwenu ya kufanya vizuri msimu huu ..hongereni kwa Hilo ..sisi Chelsea bwana alaah tunajipanga msimu ujao.
#CFC💙💙💙
Hatupo vzuriiiiii ki hivyo tuna mapungufu mengi tu lakini tunapambana kadri hali inavyoruhusu na kutumia vyema zile nafasi tunazopata kusaka ushindi.

Mpaka sasa binafsi namuona Allison ndio kete yetu ya mafanikio msimu huu maana ametuokoa vya kutosha huyu jamaa. Akiwa fiti sina shaka na makombe yatakuja.

Haya kazi kwako Jumapili mzima Patrick maana jamaa kwa Big games yupo vzuriiiiii sana kocha wako kambania dogo Gallagher asicheze hio gemu na hio inaweza kuwabeba maana yule dogo mapafu ya paka hachoki hata hua sijui anacheza CM ama RM au LM au AM hua namuona yupo uwanjani kote..

Mipango ikikaa sawa tukutane fainali Wembley... Hahaha kama namuona Klopp akisugua kichwa bila KDB atakuja aje...



YNWA
 
Mie nalia tuu na mfumo wa high line na offside trap, watu wanamfikia sana Allison
 
Mie nalia tuu na mfumo wa high line na offside trap, watu wanamfikia sana Allison
Mpango wa Klopp ni kwamba we win the second balls muda wote yaaani pale tunanyang'anywa mpira basi fasta tu regain possession chap sasa unakuta muda mwingi hilo limeshidikana na kama mechi ya Benfica uliona pia Jota alipoteza mipira mingi bila kufanya recover hivyo hii high line inaumizwa na wachezaji wetu kutofuata maelekezo ya mwalimu vyema. Ukitaka kuona Klopp anavyotaka pale mbele wacheze mtazame Mane na Firmino pale wanapochukuliwa mpira yaaani chap wataanza kuusaka mpaka waupate especially Firmino hilo hua anafanya vyema sana.

Kingine ujue pia timu pinzani sasa wanafanya mazoezi ku by pass pale kati ili mipira ifike mbele so Benfica walifanikisha hilo kwa kuwatoa muda mwingi Keita kwenye nafasi yake na wao kupiga kaunta chap. Lazima tuelewa pamoja kwamba hii high line inawapa advantage Trent na Robbo kutengeza nafasi za kufunga lakini umakini pale nyuma ukipungua basi tunapigwa.

Kwa mfumo wa attacking 4 3 3 hua tukishambulia inakua hivi 2 1 2 5 ambapo pale nyuma anakua anabaki VVD na Matip mbele yao anasimama Fabinho na mbele yake anakua Thiago na Henderson pale front sasa inakua ni Robbo, Mane, Jota, Salah na Trent ina maana hapo 1 mistake tukapoteza mpira na ukapigwa kaunta ukampita Fabinho basi maumivu lazima tuyaone na hapo ndio umuhimu wa sweeper keeper unapoonekana maana mara nyingi anatuokoa Alison ama Matip na VVD wacheze offside trick kama we are lucky basi tunapona.

Kingine mechi ya 3 sasa Fabinho kama ameishiwa upepo hivyo ufahamu bila kazi ya Fabinho DM kua na siku njema basi tegemea kuona mashambulizi yakifika kwetu muda mwingi na tena ya hatari sana.

Klopp ana dirisha la usajili kuja na jawabu ya hili janga maana kwa high line ya mita 40+ kutoka kwa Alisson ujue ni hatari na nusu.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…