Liverpool FC (The Reds) | Special Thread



Haiyaa tazameni wenyewe kuelekea kupatikana goli la Diaz, Liverpool walicheza pasi 34 bila kupoteza hata moja...

Pasi ya tatu akipiga Thiago kwa Henderson, nae Henderson akapiga kwa MOTM wa jana dogo Tsimikas akatoa assist kwa Mane.

Hii ni rekodi mpya kwetu tangu Opta wameanza kutoa hizi data EPL tangu msimu wa 2006.

Liverpool utaipenda tu.

YNWA
 


Vita ishaanza haha hii ndio sifa ya moja ya Fergie na Mourinho kuwatumia wachezaji wao kuwatia uoga wapinzani haha hatutishiki hivi kweli tukiwa kamili hivi na ile high line ya Manchester City tuwashindwe jameni...

Washaregea japo hawachelewi kushinda tena mechi 12 kama walivyo shinda kabla ya kipigo cha jana. Mara ya mwisho walifungwa EPL October 2021 na jana Conte na ile shangalia yake haha akafanya jambo ..

YNWA
 
Kuna shida mbili hapo
Lukaku anakuwa static, kandanda la sasa hivi linamuhitaji kila mchezaji awe na movement kwenye space ili apewe mpira, akiwa static wenzake inakuwa ngumu kumpasia mpira. Game na Aston Vila mwezi wa 12 alikuwa na movement nzuri na alibadilisha kule mbele.
Tatizo lingine wacheza wa Chelsea hawajui kuwachezesha forwards akiwemo Lukaku. Back and sideways passes ndizo zinazoharibu game
Haya makosa mawili ni ya kocha, kocha ampush awe an movement na wenzake wajue kupeleka mipira mbele, Ziyech anajitahidi wengine hakuna kitu. That is all
 
Elliot tumuweke kundi la akina Keita , Thiago, Fabinho , Ox , Jones na Le Captain sio?

Hapana! Elliot na Jones bado sijawahesabu kama Wachezaji wa ushindani bali nawahesabu Talented Young boys wanaojifunza! Huwezi kuwa na Mechi serious may be hizi za Knockout za UCL ukamuanzisha Elliot na Jones kama huna Majeruhi.
 
Aisee ile assist ya Allison mpaka nilibaki nacheka mwenyewe maana sikuwa namsikiliza mtu akiniambia chochote.

Hata game v/s Manure Alisson alipiga the same assist kwa Salah! Hivyo ni wazi Alisson akipata mpira mtu wa kwanza anayemuangalia ni MO Salah.
Na MO Salah mpira kutoka kwa Alisson basi lazima afunge.
 


Umesema kweli kabisa hapa tatizo ni kocha lakini pia wachezaji japo hapo wachezaji wanatekeleza maelekezo ya mwalimu kwani mechi maadalizi huanza mazoezini kabla ya mechi husika..

Ukisoma hio attachment utaona influence ya Lukaku ambae pale Inter Milan alicheza kama alivyocheza Kane jana vs Manchester City, kwa Lukaku hapa Chelsea imeshidikana kabisa ku link play ama ku recycle mashambulizi yawe brutal amekua yupo yupo tu.

Ushauri wangu maana hawa walimu wa Kijeremani ni hard knocks balaa wapeni Tottenham ela kiasi mbadilisheni na Kane 😁.. I mean Thomas hatabadili mfumo ili Lukaku awe kama Lukaku wa Inter..

YNWA
 
Mazingira na wachezaji na kocha ni tofauti kabisa kwa Inter na kwa West London. Hizo stats lazima zibadilike kulingana na wachezaji anaocheza nao, kocha anayemfundisha na motivation environment elements anazokutana nazo.
Factor nilisoitaja mbili ndizo zinazomfanya Lukaku asicheze vizuri. Yeye mwenye hana motivation ndio maana anakuwa static kibolingoli, pili wenzake, kocha na mazingira mengine ya Darajani naona kama hayampi motisha kama alivyokuwa Inter
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…