Liverpool FC (The Reds) | Special Thread


Huyo ni wa kuuzwa kabisa January, Mpaka sasa naona kwenye timu yeye ndio anaongoza kwa kupoteza mipira bila sababu.


Halafu mzito sana kwenye kukimbia,mazoezi sijui anafanyaga nini?
 
Sahihi kabisa mkuu na ndie alienifanya niishabikie hii timu nataman siku moja nimpe jogoo la kienyeji apige supu 😃😃
 
Mkuu MosDef habari za siku nyingi long time comrade...

Hii ishu ya Henderson ina mkanganyiko sana ukiachana na umri wake majeruhi yake kuadhiri output yake kwa sasa lipo hili la eti mkataba mpya alisaini huku kuna kipengele acheze 8, je kuna ukweli wowote ama ni bla bla za media...

Ukweli ni kwamba ukisoma kwa wale ma transfer guru which are rarely off the truth FSG hawana mpango wa kutoa ela direct za kununua wachezaji.. Zipo tetesi hata kushindwa kuwauza mapema Shaqiri na Origi kulichangia Klopp ashindwe kumnumua Bowen, Bissouma nk kwa vile selling team waliweka time ya kumaliza dili ili watafute replacement mapema lakini huku FSG wakakomaa na sell 1st buy later policy yaaani hii ndio anguko letu kukosa serial trophies every season...

Ni aibu kubwa sana kua na kocha kama Klopp aafu FSG wanafanya mzaha kwenye kununua wachezaji anaowahitaji, na hua nikisoma timu fulani inamhitaji basi bilo hua linanipicha all that gold is not glitters kati ya FSG na Klopp. Kwa sasa zipo tetesi Anceloti pale Real yupo kwa muda lakini long shot yao ni Klopp meaning wapo wanaojua huyu bwana is born winner with the necessary tools.

Uzembe wa FSG ni kiwango cha kimataifa aisee hivi January 2021 kulikua na haja gani ya kuwa leta wale mabeki wawili Kabak na Davies kama upgrade ya Henderson na Fabinho huku wakijua fika sio anaowahitaji Klopp maana kwa tetesi ni kwamba Klopp aliwa pointi Diop wa Westham, Bremer wa Torino, Duje Caleta-Car kutoka Marseile na huyu nilisoma alishaaga klabuni kwake kwamba anaelekea Anfield.. Yaaani hawa FSG wanatembelea nyota ya Klopp hakuna kingine.

Nadhani hata huyu Edwards kutoongoza mkataba pengine ni haya haya ya FSG kubana ela huku kikosi kikiwa hoi sana majeruhi na umri pia kwa wachezaji..

Gini duuh huyu dogo alikua the unsung hero wa Klopp yaaani rarely uone hata anakua mentioned popote pale ila umuhimu sasa upo wazi ni pengo kubwa. Ajabu kumtom replace mchezaji aliye clock most minutes under Klopp since atue Anfield kisa tu anataka value of his services iedane na pesa anayolipwa na honestly i cant blame him wanting more maana anajua fika pale kati pamejaa ma puncture kibao.. Matokeo yake hata huyo Bissouma kwa £30m walishindwa kutoa hio ela ikabaki bla bla...

Pep pale Manchester City ameshinda 10 trophies, huku Klopp akiwa ameshinda 4 trophies only. Sasa imagine if Klopp was supported by FSG sokoni kama ambavyo Pep anasapotiwa ma Mansour pale Ethad.

Ki ufupi tuedelee kusubiri miujiza ya Klopp maana wenye timu yao hawana mpango wowote kubadili hii model yao ya usajili buy later sell 1st. Bure kabisa.

Na kwa hawa FSG walivyo wajaja usishangae wanatega kumpa Salah mkataba kwa vile wanasubiri Mbappe atimkie Real Madrid aafu wamuuze Salah PSG yaaani, huku pia Mane nae wakimpigia hesabu kali sana yaaaani tunawamiliki very shrewd shaping our downfall..

Hivi unaweza aje kumpa 31 yrs old Henderson 150k aafu ushindwa kumpa same amount dogo Gini the cool ruler na ambae ana miaka 30 na haumii hovyo huku Klopp akisema angependa kuona anabaki Liverpool.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…