Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Man Utd ana kiporo cha Burnley, City nadhani kiporo chake ni cha Astonvilla, na hiki kilichoongezeka cha Everton.
Maisha yanabadilika sana.

Muda kama huu msimu uliopita tayar ligi imeisha mapema tu.

Mechi zikilingana na hawa wa juu washinde zote..ligi itakua na ladha!

Viporo vinakera sana mana unajiaminisha kama liverpool kua uko juu kumbe mwingine ana mechi 2 mkononi na anazidi kushinda.
 

Huu msimu naona dalili za kulikosa kombe kwa kukimbiza upepo kama ilivyokuwa 2018/19 dhidi ya City.

Unakaa juu, unazembea watu wanapita ndo akili inakuja.

Nakumbuka baada ya kupitwa na City hatukutoa sare hata moja, zote ilikuwa ushindi.
 
This where we are so far this season..



The attacking side of Robbo is the deal this season.. Trying and trying..



YNWA
 
Huu msimu naona dalili za kulikosa kombe kwa kukimbiza upepo kama ilivyokuwa 2018/19 dhidi ya City.

Unakaa juu, unazembea watu wanapita ndo akili inakuja.

Nakumbuka baada ya kupitwa na City hatukutoa sare hata moja, zote ilikuwa ushindi.
Sasa msimu huu eti nae Aston Villa yuko serius kuhusu kombe!

Au Aston Villla huifaham?
 
Ndio maana me nawashangaeni munao muomuogopa Man city.
City ana viporo vigumu vitupu.
Apo kwa Evaton hakatizi, mungu mmoja.
Man Utd ana kiporo cha Burnley, City nadhani kiporo chake ni cha Astonvilla, na hiki kilichoongezeka cha Everton.
 
Mkuu Don Clericuzio ukweli ni kwamba Manchester City na Manchester United ndio competitor wetu aisee hawa Chelsea na wengine nafasi zao zitaanza kuonekana soon..

YNWA

Man city ndio mshindani wetu,huyo United mashabiki wanapiga tu kelele hawana lolote hao.kelele za mashabiki zisikutishe.

Wako kama timu zingine nilizowahi kuongoza ligi ,wakasema tunachukua kombe.

Wataanza kupoteana tutakapo washushia kipigo kwenye Mechi yetu . Hapo ndio watajiona hawawezi.
 
.Namuamini Kloo kwenye Game kubwa Anajua kuzicheza vizuri karata
Villa hawataweza kutufunga Tena huko hatujawekeza ila kwaajili Villa lazima tusonge tutolewe na wengine ila cyo Villa

Man From House of God
#LFC
#LFC4LIFE
 
Jamaa ana wachezaji wake na mfumo wake hapangiwi.

Alishakwama Lijinder ndo kamrudisha kwenye reli naona asaivi kiburi kimerudi tena ngoja tuporomoke.
 
Eti tutatokaje kwa Soton!

Yaani unamzungumzia bingwa mtetezi kama unavyoizungumzia timu ambayo ndo imepanda daraja!

Haya bana, sasa hivi uwanja wa kupiga domo ni wa kwenu.

Hapo soton wanayoiwazia ni ya kina mane ,Virgil.

Hao jamaa kuna muda wanajitoa akili kabisa.

Sasa hivi waache wapige kelele tu,watatulia tu.
 
Siwachukulii poa wako vizuri kiasi chake..
Lakini Umefikiria pia kwamba Yani Manure achukue ubingwa mbele ya Man city hii! bado kuna balaa lao linakuja juu pale kama kawaida.

Mi nimefikiria msimu huu timu mwenye kikosi kipana atachukua ubingwa plus experience (kuhimili presha ya kuwa juu pale)
Still bado timu za ubingwa ni mbili tu
Liverpool na Man City..hakuna mapya .

 
Mkuu kwa kuangalia mpira sawa ila ukitazama data zao zinaonyesha winning kwa 2020 performance yao ipo juu yetu na wameonyesha kuonyesha resilience, character n instant decision making whats its matters...

Sijasema watakua bingwa nimesema tusiwadharau..

Wakati sisi tuna drop points wao wanajikusanyia pointi na ndio maana leo tupo sawa.. Ina maana kama hali yetu ikiwa bado inaedelea hivi na wao hali yao ikazidi kuimarika na kujikusanyia pointi basi mbio za ubingwa ni zao na wengine..

Mpaka sasa ubingwa upo wazi mno hakuna timu yenye uhakika nao ndio maana every 3 points won feels like a jackpot won...

Tuanze kuweka mazingira sawa na ushindi wa leo..

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…