Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Kamwambiaje ?
amesema liverpool ni moja wapo ya timu kubwa duniani, wanalipa vizuri, wanafa base bora kabisa, rangi nzuri, uwanja mzuri, akasema sababu pekee ya kumfanya mchezaji ahame liverpool labda hali ya hewa.

akatiririka tena kuwa mtu akitaka kuondoka hawawezi mlazimisha kubaki

akamalizia na ile ishu ya u captain, akasema kwa walivyojiwekea wao wale makapteni wanne wakikosekana wote basi atayevaa kitambaa ni yule mwenye longest career, hivyo kwa ile mechi anasema aliyestahili kuvaa ni Divock Origi, hivo kumpa TAA alikosea
 

Lesta 1 - 2 Manure

82'
 

Hayo maneno hajamjibu Salah bali kuwajibu Wandishi wanaovumisha kuwa MO hana furaha ndani ya Liverpool.

Mkuu usimfananishe Klopp na Mourinho kupigana vijembe na Wachezaji.

Hata siku moja Klopp hawezi kukaa akajibizana na Mtoto mdogo kama Salah.

Klopp hakuwahi kujibizana na Coutinho na Emre Can walioondoka kwa kulazimisha aje ajibizane na Salah? Serious?

Kocha Wetu ni mtu mwenye nidhamu ya hali ya juu kiasi ya Kwamba hajibizani hata na Makocha wenzake kina Guardiola na Mourinho pale wanapomchokoza aje ajibizane na Salah?

Hebu rejea mechi yetu na Spurs Kabla Mourinho alibwatuka sana na kutaja kikosi chetu kumpiga vijembe Klopp eti asilielie na injuries, na Baada ya Mchezo alibwatuka tena kubwa Timu bora (Spurs) Ndiyo imepoteza mchezo! Lakini Klopp hakujibizana nae.

Hivyo Klopp hana kawaida kujibizana na mchezaji wake usimvishe sifa aliyokuwa hana! He's best manager inside and outside the pitch.
 
Mpaka hiyo tar 17 January wanapokuja Machinjioni Anfield Manchester United tutakuwa na tofauti si chini ya point 10 kati yao na sisi,Na ndio siku ambayo tutawazika wazima kwenye Title Race tutapigilia msumali wa mwisho kwenye Jeneza.

Kwani ulishawaingiza Manure kwenye Title Contender?

Mimi sikuzote nilikuwa bado nawahesabu kuwa ni Top Four Contender kwasababu naamini Man City na Chelsea atamaliza ligi juu ya Manure.
 
Tofauti ni kwamba Klopp anatumia indirect method sio direct kama kina mourinho mfano zile blunder za Karius tulijua kabisa klopp lazima amfurushe tuu, na akamfurusha indirect tofauti ingekua Mou angebwatuka
 
[emoji16][emoji16]noma Sana
 
Mapundamilia yamepunguzwa speed huko.....

Yalikuwa yameanza kuchonga chonga ati yapo kwenye mbio za ubingwa....

viva Rodgers kwa kuyakata ngebe
 
Maneno kuntu yanahusu team kwa ujumla.yatasaidia wachezaji wasitikise kiberiti.

Ila hii ya Origi kaniacha hoi ha ha haa kumbe si ubora wa mchezaji aibu nimeona mimi
 
Excellent man....

Klopp in few words..

YNWA
 
Niendelee tu kumuonea huruma Arsenal

Kwakweli hali yake ni mbaya! Naikumbuka hali yetu ya 2014/2015 ulivyokuwa na maumivu tuliyokuwa tukiyapata.
Mpaka DullyJr na Aaron Arsenal wameacha kutua humu kwa kweli hali yao sio powa kabisa...

Mikel wamteme tu hakuna namna amechemka...

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…