Gini kazidiwa statistics za chances created na Henderson msimu huu
We kiungo gani umecreate chance moja tu yaani unazidiwa hata Na holding mid(kiungo mkabaji) Fabinho
Mkuu naona umekomaa na GINI?
Elewa hivi! Sio kwamba sisi hapa tunamuona GINI ni Messi! But kwenye kikosi chetu kuna baadhi ya Positions tuna mchezaji mmoja mmoja tu! Kwa mfano:-
LB tuna Robbo pekee
RB tuna TAA pekee
LW tuna Mane pekee
RW tuna Salah pekee
DM tuna Fabinho pekee
CM tuna GINI pekee
Sehmu tulizokuwa tuna angalau mbadala ni:-
AM tuna Hendo na OX
CB tuna VVD, MATIP, GOMEZ na LOVREN.
FW tuna Bobby na Origi
GK tuna Alison na Adrian
Kwanini sikuwaeka hawa Lallana, Keita, Xhaqiri na Milner?
Lallana simuhesabu kuwa ni mchezaji
Keita ni injury prone kwahiyo kabla ya kupona vizuri anarudi tena kwenye injury! So, ni vigumu kurejea kwenye ubora wake.
Xhaqiri hayupo kwenye mipango ya Klopp
Milner kutokana na umri wake 34yrs ni Backup player tu.
Sasa Mkuu katika positions hizo zenye Mchezaji mmoja tu hata ulalamike basi Klopp hana la kufanya ndiyomana humu wengi wetu tunamlilia Hendo na Lovren tu kwasababu Mbadala wa hawa yupo.
Hendo vs OX
Lovren vs Matip and Gomez
Lakini GINI kuanza ni Lazima kwa sababu hana mbadala.
Tuliyemtegemea kucheza position ya GINI ni Keita tu, Lakini kwasasa kumchezesha Keita ni kujirisk kwa baada ya mechi 2 tu tutamrudisha Wodini. Tusubiri apone kwanza.
Ni sawa na wanaomponda Salah! Hata aharibu kiasi gani bado ataendelea kucheza tu coz hakuna mbadala wa kumueka benchi.
Kwahiyo kwasasa tuendelee na GINI wetu tu.