Kesho watu tunaenda kwa ushindi wa 81!
MANCHESTER UTD vs LIVERPOOL - 1915
Ilikuwa ni siku ya tarehe 2 Aprili 1915, ambapo timu ya Manchester United ilikuwa ikikipiga na klabu ya Liverpool katika mchezo wa Kombe la ligi EFL, enzi hizo ikiitwa "Football League First Division".
Mechi hiyo imeacha alama kubwa sana katika medani za soka nchini Uingereza, kwani kulifanyika 'mchezo mchafu' ambao hautokuja kusahaulika kwenye historia ya soka la uingereza.
Katika mchezo huo, timu ya Manchester United ilikuwa imekalia kuti kavu kwani endapo ingefungwa, ilikuwa inashuka daraja. Hivyo ilibidi itumike mbinu mbadala ili kuweza kuiokoa timu yao isishuke daraja.
Ndipo kukafanyika mchezo mchafu ambao ulipelekea jumla ya wachezaji saba (7) kutoka timu zote mbili kufungiwa kujihusisha na soka kwa maisha yao yote.
Ilikuwa hivi..
Siku moja kabla ya mechi, baadhi ya wachezaji wa Manchester Utd walikutana na baadhi ya wachezaji wa Liverpool katika baa fulani iliyoitwa 'Dog and Partridge' iliyopo pale mjini Stretford, Manchester. Kutoka Manchester alikuwepo *Sandy Turnbull*, Arthur Whalley na Enoch West..huku kwa upande wa Liverpool alikuwepo Tom Miller, Bob Pursell, Thomas Fairfoul pamoja na nahodha *Jackie Sheldon*.
""Walipokuwa hapo, kuna mambo walijadili""...
Siku ya mchezo ikawadia.. ambapo Game ilipigwa katika uwanja wa *Old Trafford* na tulishuhudia Man U ikipata ushindi wa 2-0, magoli yote yakifungwa na George Anderson.
**
Kasheshe ilikuja kuibuka siku chache baada ya mechi hiyo, ambapo tuliona vipeperushi vinasambaa mitaani, vikifichua siri kwamba kuna mbinu chafu zilifanyika katika mchezo huo.
Chama cha soka cha uingereza kwa kushirikiana na vyombo vya dola vikaanza kufanya uchunguzi kuhusu uvumi huo.
Kweli bwana!!..baada ya uchunguzi, ikabainika kwamba ni kweli wachezaji kutoka timu zote mbili walishiriki katika mbinu chafu ya *kupanga matokeo, pamoja na kuBet.*
Ifahamike kwamba michezo hii ya KuBet haikuanza leo, bali ilikuwepo tokea zamani ambapo watu hubashiri matokeo ya mechi kwa lengo la kujishindia fedha.
Sasa basi, ilibainika kwamba siku ile kabla ya mechi, wachezaji kutoka timu zote, walikutana katika baa, na kukubaliana kwamba Manchester Utd ishinde mchezo huo ili isishuke daraja..Lakini, pamoja na kupanga matokeo hayo, pia waliBet, kwa lengo la kujipatia kipato.
Inaelezwa kwamba, katika 'Betting' hiyo, walicheza 'odds ya 7/1' kwamba Manchester Utd ishinde magoli 2 - 0..Goli moja kipindi cha Kwanza, na lingine kipindi cha Pili.
Watu wote walikuja kuamini kutokana na sababu zifuatazo;
-katika mchezo ule, wachezaji walionekana hawana morali kabisa ya kucheza mpira, hususani wachezaji wa Liverpool.
-Liverpool ilizawadiwa kupiga penati, lakini cha ajabu ni kwamba aliyepiga penati hiyo alijikosesha makusudi kwa kupiga nje..hadi refa wa mchezo akashangaa kwa jinsi penati ile ilivyopigwa.
-mchezaji wa Liverpool aliyeitwa Fred Pagnam alipiga shuti lililokwenda kugonga Mwamba, lakini cha ajabu ni pale wachezaji wenzie walionekana wakimzonga na kumfokea kwa ukali, wakihisi kwamba 'anataka kuvuruga dili'.
***
Inaelezwa kwamba, sababu zilizopelekea wachezaji wale kupanga matokeo na KuBet ni kama zifuatazo:
Mosi, Kutaka kuiokoa timu yao Manchester Utd, ili isishuke daraja.
Pia kujipatia fedha. Wachezaji kutoka timu zote mbili waliamua kubeti ili kujipatia hela.
Ikumbukwe kwamba hiyo ilikuwa ni Mwaka 1915, ni wakati ambao nchi za Ulaya ikiwemo Uingereza zilikuwa katikati ya 'Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia'...Kwahiyo kulikuwa na dalili zote kwamba baada ya kumalizika kwa msimu huo, ligi ingehairishwa, hivyo wasingeendelea na kazi yao ya Mpira. Kwahiyo waliamua kuBet ili 'kujihakikishia mkwanja' hata baada ya ligi kusimamishwa.
Pia kutokana na uchumi wa klabu kuyumbishwa na vita iliyokuwa inandelea, wachezaji walihisi kwamba, huenda hawatalipwa mishahara yao kama ipasavyo..hivyo waliamua kuBet..
**
Baada ya Chama cha Soka kujiridhisha na mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili wachezaji hao saba, Adhabu Kali ilitolewa dhidi yao, ambapo tarehe 27 Dec 1915 walifungiwa kujihusisha na soka.
Mmoja ya wachezaji waliokumbwa na adhabu hiyo, ni huyu *Sandy Turnbull.*
Mchezaji huyu ana rekodi kubwa sana pale Manchester Utd kwani huyo ndie mtu aliyeandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kupachika goli katika uwanja wa old Trafford.
'Ligi ilisitishwa kutokana na vita kuu ya kwanza ya Dunia'.
Wakati wa vita ya kwanza ya Dunia, raia wengi waliingizwa jeshini kwa lengo la kwenda vitani kuipigania nchi yao. Hapa tuliona watu wengi sana wakiwemo wachezaji wa timu mbalimbali za uingereza wakiingia jeshini. Miongoni mwa watu waliongia jeshini ni huyu Sandy Turnbull.
Lakini mwaka 1918, baada ya kumalizika kwa vita, tuliona chama cha soka cha uingereza kikiwafutia adhabu wale wachezaji waliofungiwa..kwahiyo wengi wao walirudi kikosini isipokuwa Sandy Turnbull ambaye alikuwa kashafariki mwaka mmoja nyuma baada ya kuuwawa akiwa kwenye uwanja wa vita huko ufaransa.
Naam!!..Na hivyo ndivyo ilivyokuwa mnamo Mwaka 1915 kwenye kombe la ligi msimu wa 1914-15 ambapo Manchester ilishika nafasi ya 18 huku ubingwa ukienda kwa Everton.
Tottenham Hotspur ilishuka daraja baada ya kushika mkia katika nafasi ya 20.
Chelsea aliashika nafasi ya 19, lakini alisamehewa kushushwa daraja kwakua nafasi aliyoshika imesababishwa na Manchester Utd kupanga matokeo.
***
Mwisho.
Sent using
Jamii Forums mobile app