Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

HAYA ule utamu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya umerudi tena. Safari hii mambo ni moto kwelikweli, maana ile hatua ya makundi tu inaanza, Liverpool inakipiga na Paris Saint-Germain.

Unaambiwa hivi, huo ni mtihani mzito kwa Kocha Jurgen Klopp, ambaye atapima kikosi chake kama kweli kipo vizuri kwa mapambano mazito baada ya kushinda mechi zake zote tano za kwanza kwenye Ligi Kuu England.

Mechi hiyo ngumu itapigwa leo Jumanne uwanjani Anfield, ambapo kutakuwa na shughuli nyingine pevu huko San Siro, wakati Inter Milan itakapoikaribisha Tottenham Hotspur.

Mechi nyingine kali itazishuhudia AS Monaco ikikipiga na Atletico Madrid, wakati Barcelona itakuwa na kibarua na PSV, huku Club Brugge ikiwa na kasheshe la kuikabili Borussia Dortmund na FK Crvena Zvezda itacheza na Napoli.

Kesho Jumatano kutakuwa na mechi nyingine kali kwelikweli, wakati Manchester City itakapocheza na Lyon, huku Real Madrid ikicheza na AS Roma. Man United nayo itaanzia ugenini kwa Young Boys, wakati Valencia itacheza na Juventus, huku Viktoria Plzen itacheza na CSKA Moscow na Shakhtar Donetsk itacheza na Hoffenheim. Kesho Jumatano pia kutakuwa na mechi kati ya Ajax itakayokuwa nyumbani kucheza na AEK Athens na Benfica itakipiga na Bayern Munich.
 
ahahhaahah imebidi ni like tu hata kama sio shabiki wa Liverpool. Shime shime yasije watokea ya msimu ule na madrid. vinginevyo kila la heri
 
Akikujibu unitaq.
 
Kila siku nyinyi mnapima uwezo na kujenga timu hatari Sana hii. Inamaana bado hamuamini mabeki wenu.

Mkija ugenini muwe mnaweka hashtag za kujitambulisha, maana naona mnabwabwaja bwabwaja, unamuuliza mgeni mwenzio aliyeandika utumbo.

Hivi Uefa mnacheza lini? Au ndo inabidi mshinde kwa majirani kuwanga ili tuwe wamoja.

Huu msimu mtaumiza nafsi kwa kuchukia kitu kizuri.
 
Mpaka sasa hajashinda EPL lakini hajashindwa kwasababu bado yupo anashindana
 
Chelsea katika Harakati Zao Za Kucheza Mechi Za Futuhi (Kila Alkhamis) Wameamua Kujibabaisha na Kuanza Kukomalia Timu Za Watu Zinazoshiriki Ligi Ya Wanaume Ya CL.

Lakini Watambue Tue Kuwa Liverpool Kamwe Haiwezi Kutolewa Hatua Ya Makundi.

Hata Kama Leo itafungwa basi Wajue Mechi ya Leo sio Knockout Stage Bali Kuna Mchezo Mengine inafuata.
 
Haya Maneno Mengine Ni Tofauti Na Kinachotokea Uwanjani. Lakini Game Ya Leo Tutaprove Kama Anachoongea Salah Ni Sahihi au sio Sahihi.

Salah on bond with Mane/Firmino: “There's a real solidarity between us because we don't worry about who's going to score the most or first. Each of us works so that the others score. And as you have seen, we all score." #LFC
 

Nachofurahi ni kwamba ujumbe umewafikia kutoka kila pande ya dunia, ibaki ni akili zao wenyewe.

Nategemea kuona mabadiliko leo.
 
Ukiiangalia Hiyo Video Yapili Hapo Chini Utamuona Na Gini jinsi alivyofanya Ubinafsi Wa Kutotoa Mpira Kwa Wenziwe na Tukapoteza Nafasi.

Ni wazi Kuwa Wachezaji Wetu Wanacheza Kwa Ajili ya Mtu Kufunga na Hawachezi Kwa Ajili ya Timu Kushinda.

Cha kushanga juzi kwenye Instagram Gini Ali like one of the comment written by shabiki wa Liverpool kuponda igotism ya mane yaani uselfish

in no minutes akadete na akapost kua Ali like kwa bahati mbaya!

very strange!!!!
 
Leo Nipo Upande Huu

InshaAllha Waenda Tenda Maajabu Watu Wazidi Shangaa
 


Yule alikuwa mtu wa Sub, Waingereza kama kawaida yao kutetea na kumlinda muingereza mwenzao hata kama uwezo hana ni kama jadi yao. Hii nimeiona sana mitandao yote ya kijamii, watetezi wakubwa wa huyu jamaa ni waingereza
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…