"JURGEN KLOOP ANALALA SYRIA, ANAMKIA YEMEN"
Nayaangalia Maisha ya raia wa Syria na Yemen nawaonea huruma kimyakimya... Yes wanaishi kwenye mabara yasiyolaaniwa Sana kwa umaskini lakini nchi zao zinapitia kwenye mateso ya vita ambayo yanakuwa makali zaidi ya umaskini... Wamezungukwa na visima vya mafuta lakini raia wao wanalala njaa kwa Sababu ya vita.
Kwangu huo ni Mfano wa Maisha ambayo Jurgen Klopp ataenda kuishi msimu ujaona wa Ligi pale Uingereza. Huwezi kuyaona hayo mateso yake Kama wewe siyo rafiki yake wa Karibu.
Mwalimu Jurgen Klopp atatakiwa apeleke ndoo kubwa kwenye viunga vya Anflied kwa njia yeyote ile msimu ujao Kama Anataka kibarua chake kubaki salama.
Usione Liverpool FC wanafanya usajili mkubwa na gharama kubwa ukadhani ni maamuzi pekee ya Jurgen Klopp...
Kwenye usajili huu mkubwa na uwekezaji kwenye soka la vijana kuna maamuzi ya wakurugenzi fulani waliokulia Maisha yao yote kwenye jiji la Liverpool.
Jurgen Klopp akiwa na kiburi chake angeamua kuwaambia Liverpool Bado Namuamini Karius, au msimuuze Emre Can Kama alivyofanya kwa msaidizi wake waliotoka naye mbali sana kwenye Maisha ya soka.
Kufungua pochi kwa kiwango hichi kwa Liverpool ni dhahiri kuwa wanahitaji kombe Anfield na anayetakiwa kulilete kombe hili pasipo kuwa na kisingizio chochote ni mjerumani kiburi Jurgen Klopp..
Kama management ya timu imeweza kumnunua Naby Keita, Fabinho, Shaqiri, Van Dijk na Alisson yupo njiani ,na wote hao wamenunuliwa kwa pesa ndefu sana basi Klopp afanye kazi inayotakiwa kufanya.
Hapa ndipo naona Maisha ya Jurgen Klopp yanakuwa magumu Sana Kama raia anayeishi Syria Au Yemen.
Uwanja wa Anfield Utakuwa muhimu kwake kwenye Maisha ya kutetea kibarua chake Anfield.. Anatakiwa kukusanya point nyingi za kutosha.
Huu ndio wakati ambao wale walevi wa Anfield hawataweza kuvumilia mechi kuisha suluhu na Watford au na Arsenal. Huu ndiyo Wakati ambao walevi wa Anfield hawatakuwa tayari kuona timu inapomkosa Mohamed Salah inayumba.
Hayo yote walishamsamehe pale Kiev alipoamua kumbebe mjerumani mwenzake Loris Karius.
Hayo yote walishamsamehe pale walipoona timu Kama West Brom inaitoa Liverpool kwenye FA cup.
Najua Wakati Jurgen Klopp atakapokuwa USA kwenye Pre season atakuwa busy Sana kuimarisha mifumo yake ya Gengen klopp pressing kuepuka Maisha ya kulala Syria na kuamkia Yemen.
Tuisubiri EPL ianze tuone nani atazichanga karata zake kwa umakini.
Tayari mropokaji Josee Morinho ashalalamika ratiba inaipendelea Liverpool FC.
[emoji767] KEY THE DON