Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool inajitupa kesho Jumatano uwanjani kukamilisha mchezo wa mwisho wa makundi ambapo itakutana na Spartak Moscow, huku ikihitaji sare tu kujihakikishia kutinga hatua ya 16 bora.

Liverpool imejiweka kileleni baada ya kukusanya pointi 9 na ikifuatiwa na Sevilla yenye pointi 8 katika nafasi ya pili.

Vita ya kutinga hatua ya 16 bora pia imeikumba klabu ya Spartak Moscow ambayo ushindi wowote itaiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu iwapo tu Sevilla itatoka sare.

Liverpool ipo kwenye hatari ya kukosa kuwa kileleni kwenye kundi lakini bado ina nafasi ya kuvuka kwenda hatua ya 16 bora.
 
Wewe binti nakukubali sana
 


Sisi hatuwazi Tena Suala la 16 bora kwasababu Kuqualify Ni lazima kwetu...
Labda Tunachoweza Kuwaza Kwa sasa Je
kwenye 16 bora tutakutana na mjinga gani!!!!
 
Tetesi

Nyota wa zamani wa Juventus Alessandro del Piero, anaamini mchezaji wa safu ya kati wa Liverpool mjerumani Emre Can, 23, atakuwa bora zaidi katika klabu hiyo ya Italia. (Liverpool Echo)
 
Kama tuko serious tutaweza kumlipa huwez jua hatak kubak kweny team yke ya sasa labda anataka kubadl upepo wenda akawa na mapenz na liverpool
 
wewe!hivi unadhani kuna timu itakayo vuka 16 inayo ogopa kukutana na Liverpool?kila timu inapenda ikutane nawewe ili wapandie kwako.


Acha Kuweweseka Sijaona Timu Ya Kumfunga Liverpool Katika 16 bora....
Sasahivi nafikiria Fainali sijui Nitacheza na Nani!!!!!
 
Tetesi
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa hana uhakika ikiwa mchezaji wa kiungo cha kati Philippe Coutinho bado atakuwa Anfield baada ya mwezi Januari. Barcelona ilitoa ofa mara tatu kwa raia huyo wa Brazil msimu huu. (Daily Star)
 
Tetesi
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa hana uhakika ikiwa mchezaji wa kiungo cha kati Philippe Coutinho bado atakuwa Anfield baada ya mwezi Januari. Barcelona ilitoa ofa mara tatu kwa raia huyo wa Brazil msimu huu. (Daily Star)

Hizi Ni Habari za Udaku tu lakini hazina lolote!!!
Kama Kuondoka Basi Coutinho ataondoka Summer lakini Si Hii January...
 
Wakuu, natumai vijana wetu wako vizuri na tayari kwa kazi ya leo....tuko pamoja. YNWA.
 
Kikosi Chetu Cha Leo

Karius
Gomez
Klavan
Lovren
Moreno
Can
Wijnaldum
Coutinho (C)
Mane
Salah
Firmino

Subs:
Mignolet, Milner, Henderson, Sturridge, Oxlade-Chamberlain, Solanke, Alexander-Arnold.

Formation: ↓↓
4-3-3


Referee: Szymon Marciniak (From Poland)
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…