Inashikitika sana tunakosa kushiriki Champions league kwa Uzembe wa BR. Man utd amepoteza 3 consecutive matches, tumeshindwa ku- capitalize kwenye hizo game ambazo opponent wetu wanapoteza,
Mkuu Mr. Wise, hawa analyst mbona wanataa kufanya kama Balotelli kama ndo sababu ya Liverpool kufanya vibaya. Wasitake kumtwisha Mario mzigo wa lawama wakati kuna watu kama Sterling wamecheza mechi nyingi za ligi kuliko Mario.
Mario anashindwa kufanya vizuri kwa maana ni mipira michache sana Countinho anakuletea kwenye miguu zaidi anacheza space. Pamoja na kupata matokeo mabaya bado naangalia game zetu kwa sababu ya Emre Can na Countinho. Naona Lovren anaanza kuonyesha angalau kile kidogo tulichokuwa tunategemea kutoka kwake.
Suarez alifanya watu wengi pale liverpool waonekane wanaweza ila uwezo wao ni wa kawaida sana sasa hivi ameondoka Countinho ndo anaonekana ule ndo ulikuwa uwezo wake. Pamoja na mapungufu yake kama binadamu Suarez anabalaa pamoja na kutokuwa focal point ya barcelona ila anafunga kama kawaida yake. Ahsante Dalglish kwa umpitisha huyu mtu anfied
Hizo summer targets sidhani kama tunazihitaji (Benteke, milner???)