Wana Chit Chat!!!
Huu uzi unawekwa hapa kwa malengo mazuri tu kama vile;
1.Kuepusha kuharibu nyuzi nyingine!! Inatokea mara nyingi sana hapa jukwaani,
mistari inashushwa sehemu yoyote ile so kunakuwa na mwingiliano wa mada.
Kama kuna uliyempenda kutoka jukwaa lolote lile mlete hapa umwambie.
Kwa hiyo kupitia huu uzi hapa ambao ni maalumu wa kuelezana yale ya moyoni, utaeleza hisia zako na kumtaja mhusika wako na ikionekana unahitaji msaada utasaidiwa kuna wataalamu hapa Tuko jiandae kusaidia watu hapa.
2. Kutengeneza couples zaidi ndani ya jukwaa. 2014, zitawaondolea wengi stress!!
3. Kumaliza malalamiko kwa wageni na wale wote walioko single,
mara nyingi kumekuwako na malalamiko kutoka kwa jinsia zote juu ya kuwa single
Na hii hujitokeza sana pale ambapo unakuta kuna wapendanao kama Lady doctor na Arushaone wakishow malove yao, utasikia oh heri yenu mnaopendana au kutoa kauli nyingine kama hizo, ambazo ni za malalamiko.
Hakuna haja ya kulalamika tena kwani na wewe unaweza kuwa na Mpenzi na ukaonyesha malove ya nguvu.
Hii itakuwa habari njema kwa madomo zege pia, kwani kama huwezi utasaidiwa..
Kama kuna mtu umemwona kutoka jukwaa lolote lile hata la Sports, Siasa, Ujasiriamali, Kazi na Tenda n.k
Ukampenda na ukaona anakufaa wewe, mlete hapa couple itengenezwe!!!
Hakuna haja ya kushinda tena PM na ukaishia kula za uso...
Hapa vocal zinashushwa live live.... Baba V, Arushaone tuundieni kamati ya kufanikisha hili zoezi.
mwaka 2014 ni mwaka wa malove love.
Nawasilisha.
NB; hata walioko kwenye ndoa na hawazidumishi au hawaridhiki nazo!! u can create another one.
Couples ambazo zipo na zina exist
Ni hizi hapa na ni vyema zikaheshimiwa.... kiwatengu & shansarie Tuko & jawilat (hii bado ni mpya sana) na ndoa itatangazwa muda wowote...