Mfahamu Jokate Mwegelo (Kidoti); Kuzaliwa Marekani, Urembo, kipanga darasani, Mapenzi, Siasa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
286949336_133064609338953_3767749297366868456_n.jpg


Kabla hajaukwaa Ukuu wa Wilaya, moja ya habari kubwa zaidi kumuhusu Jokate Mwengelo ambayo iliwahi kutikisa bara zima la Afrika, ni pale ambapo jarida bora zaidi ulimwenguni la Forbes lilipomtaja kuwa ni miongoni mwa vijana 30 bora kwa bara la Afrika ambao wana potential kubwa kuleta mapinduzi ya ujasiriamali na kuisaidia jamii kwenye bara la Afrika. Kuna vitu vingi mno kumuhusu binti huyu mrembo, aliewahi kujaribu ujasiriamali na sasa ni kiongozi. Viko vizuri vya kutia moyo, vibaya vya kumuonea huruma, na vya ujasiri kutufunza.

Jokate Mwegelo amezaliwa March 20 mwaka 1987 akiwa mtoto wa tatu katika familia ya Mzee Urban Costa Ndunguru. Baba yake ni mmoja ya wanadiplomasia bora kabisa kuwahi kuwapata katika nchi yetu. Kwenye miaka ya themanini baba yake alipelekwa nchini Marekani kwenda kufanya kazi kwenye ubalozi wa Tanzania kwenye mji wa Washington D.C. Mzee Ndunguru akachukua familia yake, yaani mkewe anayeitwa Bernadertha pamoja na watoto wao wawili ambao walikuwa nao kipindi hicho na wakaondoka Tanzania na kuhamia nchini Marekani. Na wakiwa huko Marekani ndipo wakapata mtoto wao wa tatu ambaye ni Jokate. Kwa hiyo Jokate alizaliwa Marekani na hata shule za chekechea madarasa ya kwanza ya shule ya msingi alianza kusoma huko huko Marekani.

Baada ya utumishi wa miaka nane kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, baba yake akarejeshwa nchini na kupangiwa majukumu mengine ya kiserikali hapa kwetu Tanzania. Kwa hiyo watoto wake akiwemo na Jokate, nao wakarejea nchini. Jokate akaendelea na elimu ya shule ya msingi katika shule ya Olimpio iliyoko Upanga na baadae mwaka 2000 akaenda kusoma kidato cha kwanza mpaka cha nne katika shule ya sekondari ya St. Anthony. Akiwa hapa St. Anthony ndipo hasa vitu vingi ambavyo baadae vilikuja kumsaidia Jokate kwenye maisha vilianza kuonekana.

Kwanza kabisa talanta yake ya uongozi hasa ilianza kuonekana akiwa hapa St. Anthony. Akiwa kidato cha tatu, Jokate alichaguliwa kuwa kiranja mkuu msaidizi. Na pia mwaka huo huo ilitokea fursa ya kufanyika kwa kongamano la mfano la Umoja wa Mataifa la Wanafunzi (Model United Nations) na Jokate alichaguliwa kuwa kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye hilo kongamano. Unaweza kusema kwamba ile damu ya diplomasia na mahusiano ya kimataifa ya baba yake Mzee Ndunguru ilikuwa inajidhihirisha pia kwa Jokate.

akiwa hapa hapa St. Anthony alikuwa ni kipanga darasani lakini ndipo ambapo jina la ‘kidoti’ lilianzia ni kwasababu ya ile sehemu ambayo ipo pembeni ya pua yake ambayo kaipata ukubwani maana hakuzaliwa nayo, ukitazama picha zake za utoto haipo. Inaonekana kwamba kilianza kidogo sana na kikawa kinakua taratibu mno kadiri ambavyo naye mwili ulikuwa unakua. Na kipindi yuko sekondari akiwa msichana mkubwa ndipo ile sehemu ilikuwa kubwa kiasi ikaanza kuonekana kwa uwazi na wanafunzi wenzake wa St. Anthony wakanza kumtania kwa kumuita ‘kidoti’. Na kwa vile alikuwa maarufu sana shuleni kwa hiyo jina hili la utani nalo likawa kubwa sana pale shuleni kwao.

Alifanya mitihani yake ya kidato cha nne mwaka 2003 na “akapasua” division 1 ya 11 huku akinyoosha somo la lugha ya kiingereza kwa alama ya A na lugha ya kifaransa kwa alama B. baada ya hapo aliendelea kidato cha tano mwaka 2004 katika shule ya Loyola High School, aliendelea kuonyesha uwezo wake wa talanta ya uongozi kwa kuchaguliwa kuwa Dada Mkuu wa shule na pia alipata nafasi ya kuiwakilisha shule anayosomea katika shindano la kuandika Essay kwa nchi 30 za jumuiya ya madola na akaibuka mshindi wa pili, mitihani ya mwisho ya taifa ya kidato cha sita Jokate alipata division 2 ya kwanza (2.10).

Baada ya kumaliza kidato cha sita, Jokate ndipo hasa akaanza kujihusisha na masula ya urembo na mitindo na wengi tukamfahamu baada ya kushiriki shindano la Miss Tanzania ambalo aliibuka mshindi wa pili. Kushiriki kwake kwenye shindano la Miss Tanzania ndio ilikuwa kama chanzo cha Jokate kuingia kwenye kundi la watu maarufu hapa nchini. Japokuwa umaarufu ulimfungulia Jokate milango mingi, lakini pia umaarufu ulimletea shida nyingi sana na kufikia kipindi kutaka kupotea kabisa kimaisha.

Lakini kabla ya masahibu hayo ambayo yaliletwa na umaarufu hayajamkuta, kwanza Jokate umaarufu ulimpa faida kubwa.. kwa mfano, Jokate ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuwa mtangazaji katika mashindano ya Bongo Star Search kipindi yanaanza. Na baada ya kuonyesha uwezo mkubwa sana katika kuyatangaza mashindano ya Bongo Star Search, Jokate alipata dili nyingi sana za kuwa MC hasa kwenye events za makampuni / mashirika. Lakini pia Jokate akapata fursa ya kuigiza filamu na alishinda mpaka tuzo za filamu za ZIFF kama mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2011. milango ikamfungukia zaidi Jokate hata kuingia kwenye muziki wa kizazi kipya na kutangaza vipindi vya televisheni.

Licha ya umaarufu mkubwa sana ambao alikuwa ameupata kipindi hicho, lakini Jokate alifanya jambo la muhimu sana ambalo limemfaa sana mpaka leo hii. Jokate hakuachana na masomo kama wasichana wenzake wengi ambao walijikuta wanapata umaarufu mkubwa kipindi hicho hasa kutoka kwenye tasnia ya urembo na mitindo. Jokate alienedelea na shughuli zake na umaarufu lakini pia aliendelea na elimu. Alijiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam ambacho kwa hapa kwetu ni kama chuo cha taifa kisicho na mpinzani, ni chuo pekee kilichofilia level za kupokea wageni wa nchi nyingine hasa zilizotuzunguka kuja nchini hapa kusoma (Rais wa Uganda, Rwanda na viongozi wengi wan chi zilizotuzunguka wamesoma hapa na wengine wanaendelea kuleta watoto wao), Jokate alisomea shahada ya Sayansi ya Siasa na Falsafa na akahitimu kwa kufaulu vizuri kabisa kwa kupata GPA matata sana ya 4.0.

Lakini licha ya kwamba umaarufu ulikuwa unamfungulia Jokate milango mingi lakini pia umaarufu huo ukaanza kumletea shida. Na shida kubwa alianza kuipata alipoanza kuingia kwenye mahusiano na watu maarufu wenzake. Mwaka 2008 mwezi April, Jokate alihudhuria fashion show ambayo ilikuwa inafanyika maeneo ya Water Front. Kupitia kwenye hii event, ndio kwa mara ya kwanza Jokate alikutana na mcheza kikapu Hashim Thabiti, kapanda hewani si mchezo aisee. Kipindi hicho Hashim Thabiti alikuwa ni wa moto kweli kweli. Kijana wa kwanza wa Kitanzania kucheza kikapu ligi maarufu ya NBA nchini Marekani. Baada ya kukutana kwenye hii event walibadilishana mawasiliano na kisha wakaanza kuwa marafiki na baadae wakawa wapenzi. Jokate mwenyewe anakiri kwamba Hashim Thabiti ndiye alikuwa mwanaume wa kwanza yeye kumpenda kikwelikweli kwenye maisha yake.. her first love. Jokate alimpenda Hashim yaani alikufa akaoza na mwenyewe aliamini kwamba wao ni soul mates, muda ule aliona watakuwa wote pamoja daima mpaka kuzikana.

Lakini kama ambavyo uhusiano huu waliufanya siri kubwa, ndivyo hivyo hivyo mpaka leo hii wamefanya siri kubwa sababu hasa ambayo iliwafanya waachane. Hii break up ilimuumiza mno Jokate kiasi alitaka kuchanganyikiwa. Jokate aliumia mno kumpoteza ‘first love’ na mwanaume ambaye alikuwa anaamini ni soulmate wake na atakufa naye. Alijikuta anatapatapa kutafuta faraja ya kuponya majeraha na maumivu ya mapenzi ambayo alikuwa nayo. Na kwenye huku kutapatapa akajikuta amedondokea mikononi mwa mtoto wa Tandale, Diamond Platnumz.

Uhusiano wa kimapenzi wa ghafla kati ya Diamond na Jokate ulikuwa wa ajabu sana. Huyu Diamond wa siku hizi japo watu wanamsema lakini kwa sasa ni kijana ambaye amestaarabika sana ukilinganisha na Diamond wa miaka ile. Diamond wa kipindi kile alikuwa ni mtoto wa Kiswahili machachari ambaye kila siku ya Mungu huwezi kukosa skendo yake fulani kwenye magazeti ya udaku ya Shigongo. Tofauti na Jokate alikuwa anaonekana msichana mpole, msomi, ‘mzungu’ na mtu wa dini. Couple yao ilikuwa ya ajabu sababu walikuwa wanaonekana kama watu wawili tofauti sana. Bahati nzuri kama namna ambavyo uhusiano wao ulianza kiajabu ajabu na ghafla, ndivyo hivyo hivyo pia haukudumua muda mrefu, na ghafla tu wakaachana.

Baada ya kutoka kwenye uhusiano na Diamond, ndipo Jokate akaelekeza nguvu zake nyingi sana kwenye ujasiriamali. Akazindua brand yake ya ‘Kidoti Loving’ ambayo ilijihusisha na kuuza nywele, ndala na mabegi ya mgongoni vyote vikiwa na chapa nembo yenye brand ya ‘Kidoti’. Hii brand ya Kidoti pengine ndio kampuni ya celebrity wa Kitanzania ambayo imewahi kufanikiwa zaidi sana. Brand yake hii ilikuwa kubwa kiasi kwamba mpaka kampuni toka China inayoitwa Rainbow Shell Craft walimfuata na kuingia naye mkataba. Kama mkataba ule ungeenda vile ambavyo ilitakiwa, hawa wachina walitaka waje wajenge kiwanda hapa hapa Tanzania cha kuzalisha bidhaa za hizo za chapa ya Kidoti, yaani nywele, viatu na mabegi na kisha bidhaa hizi ziuzwe kila kona ya Afrika.

Lakini si hivyo tu, Jokate pia akaanzisha kampeni iliyoitwa ‘Be Kidotified’ ambayo ililenga kusaidia shule za vijijini na kuboresha mazingira ya wanafunzi kujifunzia. Lakini pia kampeni hii ililenga kutoa exposure ya kidunia hasa kwa watoto wa kike walioko vijijini.

Kazi zote nzuri hizi za ujasiriamali na harakati za kusaidia jamii ndizo ambazo zilichangia sana Jokate kuja kutangazwa na jarida maarufu ulimwenguni la Forbes katika orodha yao maalumu ya vijana 30 ndani ya Afrika ambao wana potential kubwa kuleta mapinduzi ya ujasiriamali na kuisaidia jamii kwenye bara la Afrika na dunia. Hii ilikuwa heshima kubwa sana ambayo ilimpandisha Jokate na kumuweka kwenye viwango vipya kabisa.

Lakini pia heshima ambayo Jokate alikuwa anapewa haikuishia tu hapo. Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM wakamteua kuwa Katibu wa Hamasa na Chipukizi ngazi ya Taifa. Jina la Jokate likang’ara kweli kweli lakini kama ilivyo kawaida ya hapa bongo, mafanikio ya mtu hugeuka kuwa kisu kinachogonga mifupa kwa watu wengine tena wale wa karibu wa kwenye nyumba moja, kuna vijana ndani ya uvccm hawakufurahia kabisa mafanikio ya Jokate, mitandaoni kulizuka hoja za vijana hao wa uvccm kupinga kitendo cha Jokate kuteuliwa kuwa Katibu wa Hamasa Taifa kwa madai ya kwamba kuna rafiki zao walikuwa ndio ilibidi wapate hio nafasi kuliko yeye.. Lengo lilikuwa kwamba hao rafiki zao wangekuwa na hicho cheo basi nao wangeteuliwa na rafiki yao vyeo vya chini, kwa hio hawakufurahia Jokate kupewa nafasi hio.

Vijana hawakupoa wakalikoleza kweli kweli, Mjadala huu ulianza kama masihara lakini baadae ukawa mkubwa kweli kweli kiasi kwamba ikabidi Mwezi March 2018 kamati ya Utekelezaji ya UVCCM ikalazimika kumvua Jokate wadhifa wake huo wa Katibu wa Hamasa na Chipukizi. Hii ilikuwa moja ya habari kubwa sana mwaka ule 2018. Vyombo vya habari viliandika heading za maneno makali kweli kweli.. “Jokate atumbuliwa UVCCM”, Mitandaoni huko kama kawaida viiana wale walimshambulia Jokate na kumcheka.

Masahibu haya yalikuwa yamemtokea mwezi March, Kama hiyo haitosha mwezi uliofuata yakamkumba masahibu mazito zaidi. Kwa kipindi kirefu Jokate alikuwa anatajwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Ali Kiba. Couple yao ilikuwa inawavutia watu wengi sana, pia Jokate alikuwa amesaidia sana kwenye kum-brand Ali Kiba pindi ambapo Kiba aliamua kurejea kwenye muziki baada ya kupigwa pin na clouds fm pindi wanapompandisha Diamond Platnumz kwa karibia miaka mitatu au minne. Watu wengi walikuwa wanaona kwamba kuna kila dalili kwamba wawili hawa wangeweza kufunga pingu za maisha.

Lakini mwanzoni mwa mwaka 2018 zikaenea tetesi kwamba wawili hawa walikuwa na mgogoro mkubwa. ghafla tu, ilipofika mwezi April 2018 Ali Kiba akatangaza kuoa msichana kutoka Mombasa. Na kama masihara Ali Kiba akaoa kweli na harusi ilikuwa na mbwembwe za hali ya juu mno kwa harusi kurushwa mubashara na vituo vya televisheni. Na kama ilivyo kawaida, watu mitandaoni wakaacha kufurahia harusi badala yake wakaanza kumcheka tena Jokate. Jokate alichekwa, alitukanwa, na akasemwa kila aina ya maneno mabaya. Hiki kilikuwa pengine ndio kipindi kibaya zaidi katika maisha ya Jokate. Yaani mwezi March ametoka ‘kutumbuliwa’ wadhifa wake ndani ya UVCCM. Mwezi uliofuata Kiba akaoa na watu mitandaoni wakaanza kumshambulia yeye wa kejeli.

Jokate alikuwa kwenye hali mbaya kisaikolojia kiasi kwamba akaacha kutumia mitandao ya kijamii kwa kipindi cha takribani miezi minne. Na hiki kipindi cha miezi minne kilikuwa muhimu sana kwenye maisha yake. Jokate akajitafakari sana kuhusu mustakabali wa maisha yake. Kwenye kujitafakari huku akayaona masuala kadhaa ambayo alikuwa anapaswa kuyarekebisha kwenye maisha yake. Kwanza aligundua kwamba mfumo wa maisha ambao alikuwa anaishi haukuwa sahihi. Alikuwa ametoka kwenye uhalisia wake kama ‘Jokate’ na alikuwa anaishi maisha mengine kabisa ambayo si yeye anayejifahamu. Alikuwa ameukumbatia mno umaarufu na mambo ya mjini na kutoka kwenye misingi yake kama msichana mcha Mungu, msomi na anayejithamini. Pia aligundua kwamba alikuwa anajichanganya kwenye makundi na aina ya marafiki ambao hawakuwa sahihi kwake. Alikuwa amezungukwa na watu ambao walikuwa wanamtumia bila wao kufanya lolote kumuinua yeye. Na hayakuwa aina ya makundi ya marafiki ambao wanaakisi aina ya maisha ya heshima ambayo alipendelea kuishi.

Jokate akakata shauri kubadili yote haya, kwanza kabisa Jokate akaacha kutumia mitandao ya kijamii kwa muda wa karibia miezi minne. Pili, Jokate akakata mawasiliano na watu wote isipokuwa familia yake tu na marafiki zake wa zamani ambao sio maarufu ambao hawakuzidi wanne. Jokate akawa haonani na mtu yeyote au kuwasilaiana na mtu yeyote yule isipokuwa familia yake na hao marafiki wachache. Jokate akapotea kabisa mjini. watu wakabaki wanajiuliza huyu binti kaenda wapi. Wakati watu wanajiuliza Jokate ameenda wapi, mwenyewe Jokate na wale marafiki zake wanne wakaunda kikundi chao cha maombi. Karibia kila siku walikuwa wanakutana kufanya maombi ya nguvu kumuomba Mungu awaongoze na kuwaweka kwenye kusudi lake la maisha. Kwa miezi kadhaa walikuwa wamezama kwenye maombi makubwa namna hiyo karibia kila siku.

Wanasema kwamba ogopa sana mwanamke akijifunga kanga tumboni akapiga magoti chini kumlilia Mungu katika maombi. Mwenyezi Mungu huwa anajibu kwa nguvu kubwa. na ndivyo ambavyo ilikuwa kwa Jokate, Siku hiyo ilikuwa ni July 28 mwaka 2018. Siku hii jumuiya ilikuwa inafanyika nyumbani kwao Jokate. Jokate akatoka kuwasalimu wana jumuiya kisha akaingia kwenye gari na kuondoka kuelekea kwenye maombi yale anayofanya na rafiki zake kila siku. Akiwa njiani kuelekea kwenye maombi Jokate akapigiwa simu. Alikuwa ni moja ya wale rafiki zake wanao omba pamoja. Alipopokea akamsikia rafiki yake akiwa analia. Alipomuuliza analia nini, rafiki yake akamueleza kwamba, imetangazwa taarifa toka Ikulu kwamba Jokate ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya.

Mshtuko ambao Jokate aliupata, ilibidi apaki geri pembenzoni mwa barabara na kufanya maombi mafupi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa namna hii ya kipekee ambayo alikuwa amejibu maombi na kumfuta machozi. Na tangia hapo historia ya Jokate imebadilika. Leo hii ameibuka kuwa moja ya viongozi mahiri vijana kwenye nchi yetu. Ameibuka kuwa role model ya wasichana wengi wenye ndoto za kufanya makubwa kwenye siasa na uongozi. Na amegeuka kuwa mfano wa kuigwa wa watu wengi kwa namna gani unapaswa kupigania ndoto zako na kamwe kutokukata tamaa hata kama dunia nzima ikiwa kimyume chako.

Bila kusahau kuwa kuliwahi kuwa na rumours maneno maneno mitandaoni juu ya ukaribu na aliewahi kuwa kiongozi mkubwa, mitandaoni huko kulizuka tetesi kwamba baada ya Jokate kuwa mkuu wa wilaya ule uhusiano wa kikazi baina yake na kiongozi ukazidi, sasa hapa siwezi kuzungumzia sana maana hizi zilikuwa ni rumours .

Tunamtakia heri Mhe. Jokate Mwegelo katika safari yake ya uongozi na mwenyezi Mungu amuinue juu zaidi na zaidi. Na si safari ya uongozi pekee, bali pia hata kwenye maisha yake binafsi,

huyu kijana mjasiriamali anayetajwa tajwa sana mtaani kwamba mdie anahusika kumjaza uja uzito Jokate unaoonekana wazi wazi na ndie anatarajiwa kuwa baba watoto, basi ikawe kheri, ‘best friend’ huyo Mungu amguse afike Ruvuma kutoa posa ili Wamatengo wapate kupiga vigelegele kwa kukuza binti yao.
 
Kaka umetisha sana,umechambua vizuri.Inaonekana wewe ni role model wa Jokate maana umemfuatilia vizuri sana.

Ila kwamba first lover wake alikuwa Hasheem Thabiti,kweli alikuwa ana stamina za kustahimili.
Maana Hasheem size ya kiatu ni 65.

Ila nimependa kwamba aliamua kumrudia Mungu tena kwa kishindo na Mungu akajifunua kwake.

Tuendelee kumuamini Mungu,kila mtu atambariki kwa wakati wake.

Never ever give up.
 
Lakini hujasema aliupataje UDC ukaribu wake na bwana yule ulianzaje anzaje baada ya kutimuliwa hamasa, pia hujasema kuwa dogo yule aliyekua kibopa UVkunani alikuwa anataka apite kimasikhara kwa doti baada ya kuchomolewa doti akaundiwa zengwe akasepeshwa hamasa , alafu vile vile hujasema kwa nin yule msanii anayetoa ngoma moja kwa mwaka alimuacha J hujasema msanii yule alivyopigwa biti kama asipoachana na mali yenyewe kitamkuta kitu akaona cha kufia nn? Bora akaoe kwa bwana Jo na msanii ameyasema yote kwenye wimbo wake aliouimba kwa kumix lugha ya bwana Macron na kimatumbi chetu.Ila bwana yule alikua hataki masikhara kabisa na doti kuna mwamba mmoja alikuwa anamzengea kibarua kilimuota nyasi bwana yule alipofanya ziara wilayani hapo, huyu ndo atakuja amrithi katibu yule aliyewahi kuwa RC sijui DC daresalama
 
Lakini hujasema aliupataje UDC ukaribu wake na bwana yule ulianzaje anzaje baada ya kutimuliwa hamasa, pia hujasema kuwa dogo yule aliyekua kibopa UVkunani alikuwa anataka apite kimasikhara kwa doti baada ya kuchomolewa doti akaundiwa zengwe akasepeshwa hamasa , alafu vile vile hujasema kwa nin yule msanii anayetoa ngoma moja kwa mwaka alimuacha J hujasema msanii yule alivyopigwa biti kama asipoachana na mali yenyewe kitamkuta kitu akaona cha kufia nn? Bora akaoe kwa bwana Jo na msanii ameyasema yote kwenye wimbo wake aliouimba kwa kumix lugha ya bwana Macron na kimatumbi chetu.Ila bwana yule alikua hataki masikhara kabisa na doti kuna mwamba mmoja alikuwa anamzengea kibarua kilimuota nyasi bwana yule alipofanya ziara wilayani hapo...
Kumbuka Jokate alikuwa na GPA ya 4.0 chuo kikuu UDSM, hii GPA sio kusema ni kwapa kila mtu analo :rolleyes: ni Gpa ambayo inakuweka automatically kwenye spotlight kuonekana kirahisi tena hasa ukiwa na umaarufu, Naweza kusma ni kama ilivyo kwa Niki wa pili, alikuwa na elimu na umaarufu hivyo ikawa rahisi kuonekana.

Kuhusu mapenzi kuna rumours zilisambaa mitandaoni kwamba ishu ilianza baada ya Jokate kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya, kuna ule ukaribu wa kikazi huwa unakuwepo kati ya Mkuu na wakuu wa wilaya, kilichoendelea ni tetesi zilizoacha viulizo vingi
 
Kidoti.....mimi nakuombea kila lililo jema. Mungu wa mbinguni akutimizie haja za moyo wako. Umekutana na mengi kwa mujibu wa mtoa mada lakini mara zote unajipa muda wa kujitafakari na kumlillia Mungu kisha kujikung'uta vumbi na kusonga mbele. Mungu mwingi wa rehema azidi kukuinua kwa viwango vya juu...
 
una fahamu kwanini aliitwa Jojo?
Kumbuka Jokate alikuwa na GPA ya 4.0 chuo kikuu UDSM, hii GPA sio kusema ni kwapa kila mtu analo :rolleyes: ni Gpa ambayo inakuweka automatically kwenye spotlight kuonekana kirahisi tena hasa ukiwa na umaarufu, Naweza kusma ni kama ilivyo kwa Niki wa pili, alikuwa na elimu na umaarufu hivyo ikawa rahisi kuonekana.

Kuhusu mapenzi kuna rumours zilisambaa mitandaoni kwamba ishu ilianza baada ya Jokate kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya, kuna ule ukaribu wa kikazi huwa unakuwepo kati ya Mkuu na wakuu wa wilaya, kilichoendelea ni tetesi zilizoacha viulizo vingi
 
una fahamu kwanini aliitwa Jojo?
Yawezekana yaliyotokea yana ukweli lakini hayo mengine kila mtu anamzigo wake, lakini kiuhalisia kwa hizi sifa alizokiwa nazo Jokate unapinga kipi asiwe kiongozi.

1. Kwenye elimu alikuwa vizuri kuanzia Divisioni 1 ya form 4, Division 2 ya form 6, Kushika nafasi ya pili kwenye Essay za kimataifa, kupata GPA 4.0 chuoni.

2. Talanta ya uongozi alikuwa nayo tangu shuleni

3. Kusomea kitu chenye uhusiano na teuzi: hapa kasomea shahada ya Sayansi ya Siasa na Falsafa, kwenye falsafa huku kuna maarifa muhimu sana ya wanafalsafa kama kina Plato, Aristotle na Socrates ambayo ni muhimu sana katika uongozi.

4. Kuwa mtu anaehusika katika uamsho positive kwenye jamii

5. Kuwa role model wa mabinti wengi positively and ethically

6. Kuzijua lugha za kimataifa kiingereza na kifaransa, hizi lugha ni muhimu kuzijua hasa unapo interact na watu wa mataifa ya nje wanaofanya shughuli zao kwenye jamii,,
 
Mitandao inabtiza majina lakini haiondoi uhalisia wa efficiency ya jokate kuwa candidate sahihi kipindi kile analamba teuzi (Hta kama yalitokea bado alikuwa ni candidate sahihi zaidi)

Mtu ana hizi sifa unapinga kipi asiwe kiongozi.

1. Kwenye elimu alikuwa vizuri kuanzia Divisioni 1 ya form 4, Division 2 ya form 6, Kushika nafasi ya pili kwenye Essay za kimataifa, kupata GPA 4.0 chuoni.

2. Talanta ya uongozi alikuwa nayo tangu shuleni

3. Kusomea kitu chenye uhusiano na cheo: hapa kasomea Political science ni kozi inaendana vizuri kabbisa na cheo chake

4. Kuwa mtu wa jamii

5. Kuwa role model wa mabinti wengi positively and ethically

6. Kuzijua lugha za kimataifa kiingereza na kifaransa.
Jojo? unazani jina limetoka mtandaoni kama kidoti?
 
Joketi.ana nyota ya kun'gaa kila alichogusa kinafanikiwa kuanzia umiss, uigizaji,,utangazaji, ujasiriamali hadi siasa tofauti yake na Sepenga ni kuwa Sepenga hayuko serious skendo zinamwangusha Sepenga utulivu 0 la sivyo naye angekuwa kashalamba nafasi nyeti kwa Hangaya
 
Joketi.ana nyota ya kun'gaa kila alichogusa kinafanikiwa kuanzia umiss, uigizaji,,utangazaji, ujasiriamali hadi siasa tofauti yake na Sepenga ni kuwa Sepenga hayuko serious skendo zinamwangusha Sepenga utulivu 0 la sivyo naye angekuwa kashalamba nafasi nyeti kwa Hangaya
Wema Sepetu tatizo ni skendo nyingi sana ambazo zishamuharibia image ya kulamba teuzi serikalini. Laiti angekuwa katulia kwa miaka hata miwili hivi angelamba hata teuzi za idara za vitengo vya ukalimani, maana lile yai analolitema kiukweli hatuwezi kulibeza, anakichapa kiingereza si mchezo.
 
Lakini hujasema aliupataje UDC ukaribu wake na bwana yule ulianzaje anzaje baada ya kutimuliwa hamasa, pia hujasema kuwa dogo yule aliyekua kibopa UVkunani alikuwa anataka apite kimasikhara kwa doti baada ya kuchomolewa doti akaundiwa zengwe akasepeshwa hamasa , alafu vile vile hujasema kwa nin yule msanii anayetoa ngoma moja kwa mwaka alimuacha J hujasema msanii yule alivyopigwa biti kama asipoachana na mali yenyewe kitamkuta kitu akaona cha kufia nn? Bora akaoe kwa bwana Jo na msanii ameyasema yote kwenye wimbo wake aliouimba kwa kumix lugha ya bwana Macron na kimatumbi chetu.Ila bwana yule alikua hataki masikhara kabisa na doti kuna mwamba mmoja alikuwa anamzengea kibarua kilimuota nyasi bwana yule alipofanya ziara wilayani hapo...
nimecheka mnooo lol.
 
Aliongoza chama cha wanafunzi wakaenda US akiwa UD, alidate na Domo pia Kiba100 ,alikuwa na brand yake kama KP ikamfia.Baadae akaenda kutangaza Channel O na kutoa single zake hadi na wanigeria.

Alipendwa na mkulu Marehemu na hatimaye kaona ndoa inagoma kaamua kuzaa na Vunjabei. mwanakwaya wetu ana bahati kasoro ndoa
 
Back
Top Bottom