Live on Star TV, Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe azungumzia changamoto za Corona Sekta ya Habari

Ngoja nisubiri kusikia vituko vya wasomi wa Tanzania pale wanapopewa madaraka!

Najua moja ya mambo atakayoongea kwa tambo na majivuno ni jinsi hotuba ya Magufuli ilivyo-trend duniani huku akijaribu kuaminisha watu kwamba ili-trend in a positive way.

Atataka kuaminisha ili-trend in a positive huku akisahau ili-trend kama tulivyowahi ku-trend hapo kabla kwa kuonekana ni taifa la majuha kwa kuidai Acacia Sh 425 Trillion, bajeti ya nchi kwa zaidi ya miaka 10 huku Market Cap ya hao Acacia wenyewe ilikuwa haifiki hata Sh 5 trillion!
 
Mayalla naona umetumia nafasi vyema kutema nyongo zako kwa Waziri...Naona hujagusia swala la amri toka juu au unamsubiri Ngosha mwenyewe ndio uje umuulize.?

Halafu Waziri anasema maswala ya kawaida huwa mnaongea vizuri tu ila maswala mazito ya kazi humwambii...Bila shaka amekufungulia mlango wa chumbani kazi kwako nategemea baada ya Muda mfupi vipindi vyako vitakuwa hewani.

Usisite kutupa update kwa utatuzi wa Changamoto zako kwa Mh. Waziri.

Yote kwa yote Nimependa utulivu wako na ujenzi wako wa hoja, Natamani siku moja kipindi Cha Kitimoto kirudi hewani bila vitisho vya amri toka juu.
 
Mwambie Mwakyembe asituharibie soka la bongo, akitaka atengeneze ligi ya wachezaji wa ndani siyo kuzipangia timu kusajili wachezaji wa 5 kama hela anatoa yeye



"Not everything is for everybody"
 
Leo mayala amejitahidi kumuuliza maswali lakini makiembe anaonekana kudhoofika mno kashindwa kujibu maswali kabisaa
 
Hata bulendu wamempiga maswali kuhusu kuporomoka kwa uandishi wa Habari lakini ameshindwa kujibu analalamikia kuwa wameporomoka kutokana na kukataa ushogaaa
 
Waziri wa habari mh Mwakyembe amesema bunge la Uingereza juzi limeanza vikao kwa kuiga ubunifu wa Spika Ndugai.

Mwakyembe amesema sasa wabunge wa UK wanakaa katika chambers wakiwa wachache wachache wakiendelea na vikao vya bunge ukiwa ni ubunifu ulioasisiwa na Spika Ndugai.

Tanzania kwa sasa tumekuwa nchi ya mfano hata Rais Trump amefuata nyayo za Rais Magufuli kwa kutangaza siku maalumu ya Maombi ya kuliombea taifa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom