FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 733
Naama na hili ndilo tamko ambalo wengi mlilitegemea ndugu CMB.JK he cannot touch any serious issues ataongea kama anahutubia watoto wa secondary . Lakini JF pia inamnyima raha JK si siri maana hata Bungeni wanafunika hapa JF ni moto.
Naam it is break time na tukirudi baadaye nitakuwa na machache naenda kuongea na wajumbe kusikia kama wame elewa hotuba ya Mwenyekiti wao .
Baadaye
Asante FD naona umetupa undani zaidi. Please fanya vivyo hivyo kadri kikao kinavyoendelea, tupe updates.
Niko hapa Dodoma nangoja hilo mnalo dhani JK atasema ila nawahakikishia kwamba the guy kesha sema hana jipya . Hagusi vitu muhimu hata mara moja . Anataka kuchekesha lakini watu wao wanawaza vyeo baada ya kura .
Nothing serious is gonna be pronounced here .Anarudia madai ya kusema akina Slaa ni waongo laini sioni anakubali kwamba Tume iundwe hapana . Hakuna lolote .
Kamfanya Pope kuwa kivuli chake cha msaada na ndiyo maana anapenda sana picha na hao jamaa.Lakini mbona CCM leo makofi hayatoki ama kwa vile wajumbe wengi si waelewa sowanabaki kapa ?falsafa ya maisha bora leo inageuzwa rasmi mnaletwa wimbo mpya .
muungwana hana jipya..mambo anayoongea tumeyazoea,ila kinachouma ni kwamba ROSTAm ameshapanga timu yake,chama ni male yake-
Hapana,
Nipo kizota, ni mapumziko. JK amesisitiza kuhusu uungwana, kuhusu kejeli zenu na jinsi anavyoyachukulia. Jk amelaani Mtandao kuwapa wapiga kura orodha nzima ya NEC (wakupigiwa kura) kutoka kila kundi, amewaita wazi wazi Watoa Rushwa, na kasisitiza wapiga kura wawachague hata wale wasio na uwezo wa kwenda mikoani kutoa rushwa.
JK ameelezea maendeleo mbali mbali, ameongelea tatizo na Mbolea na namna serikali inavyolikabili, kwa kujenga kiwanda kwa ajili ya Minjingu Phosphate(sic)
JK ameongelea kuunganisha nchi kwa barabara, ya lami, ametaja ya Lindi na Singida zimeanza.
JK ameongelea kuundwa/kujengwa kwa reli ya kuunganisha TZ mpka BUrundi na Rwanda. Na kusema ya sasa (reli) njia ni ya mwaka 1910, hata mabehewa na Injini ukitaka kuagiza inabidi utengenezewe special kwa ajili yako, only TZ UG and Kenya are using this old tech.
JK ameongelea madini, ameelezea kuhusu mikataba, akasema wanaojadili hawana uwezo wa kuhujumu kwa kuwa sheria zote zimo. Amesisitiza loss carry forward ya 15% ndio tatizo na analishughulikia. Pia amesema madini inaingiza 1.9% ya pato la taifa. Ameelezea vizuri, kasoro ni moja why mikataba ni siri ndio hakusema
JK amesema kuhusu umeme Kilwa (soon kukamilika, Lindi na Mtwara kutumia umeme wa Gesi ya Mnazi mmoja.
Jk ameongelea namna falsafa yake ya maisha bora kwa kila mtz inavyofanya kazi.
JK ameongelea mafunzo kwa askari wetu na kuwajengea nyumba maafisa wake. Amesisitizia mafunzo kwa askari wakati wa amani.
JK ameongelea tatizo la Umeme kwa ujumla na kusema ni 10% tu ya watanzania wote wanapata umeme, wanaifanyia kazi hilo.
JK amesema mazungumzo ya muafaka yata resume soon, yalisimama kwa ajili ya kampeni ya CCM.
JK ameongelea mambo ya michezo na kusema wanaifanyia kazi.
JK ameongelea umasikini na jinsi alivyoifanyia kazi, jinsi alivyozungumza na CEOs katika CEO's roundtable, akaongela kuwa kama uchumi ukipanda kwa asilimia 10 kila mwaka basi pato la mtanzania inaweza kufikia kiasi fulani (nimesahahu) ikifika mwaka 2025, kiwango ambacho ni kidogo pia, amesema analifanyia kazi.
JK ameongelea UFISADI, amesema kuwa kuna tume ya maadili ipo na kuna PCCB, ameeleza wazi kwa wao hata ukituma SMS ni mali kwao Mwenyewe amesema anapokea SMS za tuhuma mbalimbali na zote zinashughulikiwa. Amesema, hata ukisemea mwembe Yanga au ulaya au hata kama ni minog'ono wao wanayafanyia kazi.
Jamani nasikia njaa ngoja nikapate msosi, foleni imepungua. Kaongea mengi sana ya maana jamani.
It was one of the best HOTUBA.
Unedited
Mzee wa Dom kwa leo
Kwa Msekwa kupita kweli mtandao unashika hatamu,
FD!Hapana,

kaka jk kwa sura na maneno ni mzuri...tatizo utekelezaji..sikatai hotuba was slightly good haishindi ile ya kuzindua bunge ..tatizo utekelezaji,..nawewe nakutakia chakula chema...sijui bia ziko wapi nipate moja...kiuuu.
Mkandara!FD,
Samahani, nawe kwa nini unatumia jina wana Chadema ikiwa hili swala la rangi ndilo tunajaribu kuliepuka?..
Huwezi kusoma hoja za watu bila kutazama kwanza ni wanachama wa chama gani? mbona yako tunayasoma na sioni mtu akisema kuwa uyasemayo ni kwa sababu wewe CCM!
Kifupi, JK anapoteza muda wa Watanzania na maswala yote ulosema ni ya maana hayana umaana wowote ikiwa reli imejengwa toka 1905 na hakuna kilichofanyika hadi leo hii 2007. Hatukuanza kuzungumzia reli leo ama jana ni gonjwa sugu ambalo kutokana na Umaskini nachelea kusema huu ni usanii mtupu! Ikiwa tumeshindwa kufanya ukarabati wa reli yetu ya zamani toka Nyerere alipoondoka madarakani leo kweli tunaweza jenga mpya?...I mean twendeni mbele tukitazama nyuma. Na kama itajengwa mpya usafiri wa reli utakuwa vipi na kwa miaka mingapi maanake ujenzi wa reli sio mchezo mdogo.
Asilimia 10 tu ya Wadanganyika wana Umeme toka tupate Uhuru tumesikia habari za kulifanyia kazi.
Nakuomba sana isome upya hotuba hiyo na utuambie kipi kipya ambacho Wadanganyika hawajawahi kukisikia toka zamani. Nadhani la muhimu hapa ni utekelezaji na sababu hasa ilofanya watu wamwite JK msanii ni hii habari ya kuzungumza mengi matamu ktk mikutano hali hizo ahadi hazisemi utekelezaji wake utaanza lini na kwisha lini, pia makadirio ya matumizi ya ujenzi huo yanatarajiwa kuwa kiasi gani na gharama zake zitalipwa vipi?..
Hizi ndizo hutuba wananchi tunataka kuzisikia yaani vitu vimekwisha wekwa mezani na Physical study imeshafanyika kinachosubiriwa ni kuanza ujenzi.
FD, Kuna habari nimezipata hapa kuwa mkutano ulitanda ukimya wa ajabu yaani kila mtu alikuwa akisubiri mazishi yake!..Hakuna furaha ndani ya Ukumbi kama ilivyo kawaida na hawa wote ni wana CCM. Ama nao tayari wamekwisha vikwa U Chadema!
FD!
Kweli nimeamini wewe ni Kada Kama walivyo makada wengine wa Chadema humu,Kuongelea ni sawa,Kwani toka amaeingia madarakani ameongea mengi sana mazuri Lakini ni Mangapi ametimiza ,Mengi yemefanywa na watendaji mabovu baada ya semina elekezi ambayo aliiandaa mahususi kwa ajili ya tahadhari na kutoa muelekeo kwa watendaji ili watende vyema na kutimiza wajibu wao Lakini ni wangapi ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao na hata kuendelea kulitia TAIFA HASARA NA YEYE KUSHINDWA KUWACHUKULIA HATUA KAMA ALIVYOAHIDI?
Nafikiri unamiss Picha kubwa hapa swala si kuongea mazuri na kuyaacha kwenye makabrasha bali swala ni kuyatekeleza na kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kubweresha maisha ya watanzania wote.Kwa kuondoa kero zinazosababishwa na adui Ujinga, Maradhi, Njaa Nk.
Hana hulka au uwezo wa kuwawajibisha wana miamvuli wake na watendaji kwa ujumla hasa ukizingatia wengi anawaonea aibu kwasababu aliwapa hizo nafasi kama fadhila na wengi ni watu wake wa karibu aliokuwa nao ktk kuvuka daraja la kuelekea Ikulu.
FD,
Samahani, nawe kwa nini unatumia jina wana Chadema ikiwa hili swala la rangi ndilo tunajaribu kuliepuka?..
Huwezi kusoma hoja za watu bila kutazama kwanza ni wanachama wa chama gani? mbona yako tunayasoma na sioni mtu akisema kuwa uyasemayo ni kwa sababu wewe CCM!
Kifupi, JK anapoteza muda wa Watanzania na maswala yote ulosema ni ya maana hayana umaana wowote ikiwa reli imejengwa toka 1905 na hakuna kilichofanyika hadi leo hii 2007. Hatukuanza kuzungumzia reli leo ama jana ni gonjwa sugu ambalo kutokana na Umaskini nachelea kusema huu ni usanii mtupu! Ikiwa tumeshindwa kufanya ukarabati wa reli yetu ya zamani toka Nyerere alipoondoka madarakani leo kweli tunaweza jenga mpya?...I mean twendeni mbele tukitazama nyuma. Na kama itajengwa mpya usafiri wa reli utakuwa vipi na kwa miaka mingapi maanake ujenzi wa reli sio mchezo mdogo.
Asilimia 10 tu ya Wadanganyika wana Umeme toka tupate Uhuru tumesikia habari za kulifanyia kazi toka hatujapata barehe.
Nakuomba sana isome upya hotuba hiyo na utuambie kipi kipya ambacho Wadanganyika hawajawahi kukisikia toka zamani. Nadhani la muhimu hapa ni utekelezaji na sababu hasa ilofanya watu wamwite JK msanii ni hii habari ya kuzungumza mengi matamu ktk mikutano hali hizo ahadi hazisemi utekelezaji wake utaanza lini na kwisha lini, pia makadirio ya matumizi ya ujenzi huo yanatarajiwa kuwa kiasi gani na gharama zake zitalipwa vipi?..
Hizi ndizo hutuba wananchi tunataka kuzisikia yaani vitu vimekwisha wekwa mezani na Physical study imeshafanyika kinachosubiriwa ni kuanza ujenzi.
FD, Kuna habari nimezipata hapa kuwa mkutano ulitanda ukimya wa ajabu yaani kila mtu alikuwa akisubiri mazishi yake!..Hakuna furaha ndani ya Ukumbi kama ilivyo kawaida na hawa wote ni wana CCM. Ama nao tayari wamekwisha vikwa U Chadema!
Mjomba tupe habari zinazoendelea haya maswala ya Chadema CUF mnayo wenyewe huko Dodoma, sisi tunachosubiri ni kuona mnakiweka kindimu kisawasawa.