Dharra
JF-Expert Member
- Jun 23, 2017
- 1,661
- 2,973
Kushangiliwa kidogo amejiona anaweza kupambana na CCM the Giant huku nafasi ya Urais ikiwa na incumbent president.
Kama anataka kutimiza namba haina tatizo kwa sababu hata Anna Mghwira aliwahi kugombea Urais.
Hajui kuwa Watanzania ni wazuri sana kwa kushangilia na wepesi sana wa kukusahau ndio maana wanaleta misema mingi kama vile "pambana na hali yako" ikimaanisha kuwa usiwauzie fulana au matatizo yako.
Mdanganyeni akacheze hiyo kamari ili apoteze vyote. Hata ubunge utausikia kwenye TV kwa miaka mitano.
Yeye aendelee tu kuwa mwanaharakati kwa sababu mwanaharakati "anajua yote" lakini hana practical solution.
Aende akamuulize Lyatonga Mrema au Lowassa aliyekuwa anatandikiwa kanga barabarani na anadekiwa baràbara ili apite!
Juzi Lowassa aliposhuka kwenye gari lake wakati wa ufunguzi wa kampeni Kinondoni zilizikika sauti za watu kama watatu wakiimba Rais, Rais, halafu sauti nyingine ikasema mbona mmepooza na hamuimbi?
Hii ndio Tanzania
By the way, anazo pesa za kumlipa Lowassa ili amwachie nafasi yake?
Ukiachilia nguvu ya vikosi na taasisi zingine za ukandamizaji, sidhani kama CCM ni giant kama unavyodai hapa, hio ndio fact.