Uchaguzi 2020 Lissu, kuna kila dalili wenye CHADEMA yao hawakutaki ugombee urais, kama vipi twen'zetu ACT Wazalendo

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,501
51,092
Kila dalili ndani ya Chadema zinajionyesha, brother Lissu wenye Chadema yao hawakutaki ugombee urais kupitia chama hicho. Wangekutaka wangekupa hata signal ya kuwa wako nyuma yako katika kinyang'anyiro hiki.

Kuna sauti mitandaoni Godbless Lema anasema "umeanza kujiweka katika tune ya ugombea urais", yaani umeshaanza kujiaminisha kuwa wewe ni mgombea, hii ni dalili ya kwanza kwamba brother bado hauna baraka za wenye chama chao kugombea.

Pili, kitendo cha Mwenyekiti kuchukua fomu wakati tunajua by all means hana nia ya Urais, sisi tunajua na yeye anajua, inalenga kufanya mahesabu yako ndani ya Chadema kupata hiyo nafasi kuwa ngumu, maana kiukweli mwenyekiti anaungwa mkono kuliko wewe ndani ya Chama, na there is no way unaweza kumshinda mbele ya wajumbe kwenye mkutano Mkuu.

Kitendo cha Msigwa naye kuchukua fomu wakati naye tunafahamu fika hawezi kumchallenge Magufuli head on ni dhahiri umewekwa mtu kati, chance zako za kuwa mgombea zimeminywa kutokana na move hizi tunazoziona.

Nguvu zilezie zilizoamua Dr Slaa asiwe mgombea mwaka 2015 unfortunately ndiyo hizo hizo it seems zinataka usigombee this time.

Wewe Lissu, watu wana biashara zao, wana mipango yao ya hela pembeni, wengine siasa ni mtaji, unadhani wakipewa dili wakuzuie usigombee wanaumia chochote?

Aisee utakatwa kupitia mchakato feki ndani ya chama utakaopewa jina la demokrasia na wewe utashangaa!

Sisi wananchi tunajua wewe na Membe ndiyo mlioutaka Urais mapema kabisa na tunawajua na tunaamini. mmoja kati yenu ndo angeweza kumchallenge jiwe, Yaani Membe ndani ya CCM na wewe nje ya CCM.

Karata ya Membe huko CCM imeshatolewa mchezoni kimafia, umebaki wewe nje ya CCM. na lazima uchezewe mchezo uleule lakini hukohuko ndani ya upinzani! Kuna kitu kigumu mbele ya Fedha?

Sasa jiandae, kama unautaka Urais uwe tayari kushusha Tanga na kupandisha Tanga kwa kwenda ACT.

Kuna kila dalili ya wenye Chadema yao kwenye chama chako hawajawa na msimamo kuwa wewe uwe mgombea!

Endelea kujipanga na ujiandae kisaikolojia. Wewe unaweza kuwa real, lakini kuna baadhi ya watu uchaguzi kwao ni dili.
 
Lissu alishasema chama wakinipa nafasi ya kupepeprusha bendera. Sisi sio Kama CCM hata angechukua fomu pekeake angepigiwa kura za Ndio/hapana Kama kwa Sumaye uchaguzi uliopita.Kwa hiyo wengi kuchukua fomu haimaanishi kwamba hawamtaki Lissu Wala Mwenyekiti kuchukua fomu haimaanishi Lissu hakubariki.

Hii Ndio demokrasia nanhata nafasi za ubunge wa ndani Kuna wabunge ambao huwadhanii wanaweza kupigwa chini kutokana na Sina ya watu wakakao wachallenge kwenye majimbo.

ACT wazalendo pia Wana nafasi ya kusimamisha mgombea wakitaka Ila sio Lissu.Lissu hahami kwenda popote.Lissu anaweza kugombea Tena Cha CDM miaka mitano ijayo.Usitake kuleta siasa za uchonganishi hapa
 
Kabisa Mkuu hiyo ndiyo democracy ambayo tuitakayo wacha hao majabari wa Chadema wapambane kumwaga sera zao na ikiwezekana kuwepo debates za kuuza sera zao kisha kura ipigwe ili kumchagua yule atakayekuwa na support kubwa.

Akili imemmjia kwa Lipi?Hii so ndo Demokrasia ambayo 2015 tuliteleza?Leo like kinachoitwa Demokrasia kikifanyika kwa vitendo mnaanza Tena kunung'unika.
 
Eti, "....kuna kila dalili kuwa wenye CHADEMA yao hawakutaki ugombee Urais....."

Aisee, hii ni kauli ya kuchochea hisia za wana - CHADEMA ili kuwagawanya tu....!!

Na Mimi naamini kabisa kuwa hata kama kina Msigwa, Nyalandu na huyu umsemaye japo kiukweli wala hajatia nia hiyo wasingetia nia ya kugombea na kumuacha mtu mmoja (Tundu Lissu) pekee, wala msingekosa maneno ya kusema....

Nakuhakikishia Tundu Lissu ndiye atakayepambana na mgombea wa CCM na ataungwa mkono na ACT WAZALENDO na vyama vingine kwa Urais wa JMT.....!!
 
Kale kagenge ndani ya CHADEMA kanaendelea na kazi ya kumshughulikia Lissu. Msikilize Lema.

Maneno haya ndio wanayoambiwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa Chama kwa sasa
 
Wewe huoni kuwa badala ya sasa kumpa ushirikiano mtu anayeweza kumchallenge Magufuli wao wanaanza kujifanya wanachokua fomu na kuwachelewesha wananchi kuungana nyuma ya mtu anayeweza kumchallenge Magufuli?

Angalizo kwenye post yako namba moja ni zuri, ila umeongea maneno mengi mpaka hata kama ulikuwa na nia njema unaanza kutia shaka. Mimi binafsi sikutegemea kuwa Mbowe naye atatia nia ya kugombea urais. Ni kweli Mbowe anaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa baadhi ya watu ndani ya cdm. Lakini ni ukweli usioacha shaka, kuwa Lissu ndio mwenye mvuto wa kweli kwa wapiga kura wengi kuliko mgombea yoyote ndani ya cdm.

Siamini kabisa kuwa Mbowe anaweza kuwa na mvuto alionao Lissu kwa wapiga kura wa nafasi ya urais nje ya cdm. Pia Mbowe sio mjenzi mzuri wa hoja kulinganisha na Lissu, labda kama Mbowe kachukua kwa minajili ya kupanua demokrasia, lakini sikuona ulazima wa hili. Ila tatizo la dhahiri ninaloliona ni kesi alizo nazo Lissu kwenye mahakama zetu.

Nina uhakika wa asilimia 100, kuwa Lissu atakapoingia hapa nchini ni lazima atawekwa ndani, na kesi hizo zitatumika makusudi kumzuia kugombea urais. Hakuna namna yoyote ile Magufuli au wanaccm, watakubali Lissu ashindane na Magufuli akiwa cdm au Act, kwani wanajua fika kilichomkuta JK dhidi ya Slaa uchaguzi wa 2010, na kilivyoidhoofisha ccm. Kwangu kitendo cha Lisu kuchelewa kurudi nyumbani, kisha arudi muda mfupi kabla ya uchaguzi huku akiwa na kesi, ni miscalculation kubwa.

Niwe mkweli tu, kwa mazingira ya kisiasa yalivyo mabaya, na wagombea wa cdm waliopo ukimuacha Lissu atakayepata vikwazo vya kesi, sioni mgombea yoyote wa CHADEMA mwenye mvuto wa kweli kwa wapiga kura. Labda kama wataungana na Act, wangalau Zito ni mzuri kuliko hao wagombea wote wa CHADEMA. Lakini kwangu mimi tatizo la msingi sio hao wagombea na sifa zao, bali tume ya uchaguzi isiyo huru. Hapa ndio tatizo la msingi lilipo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom