Mahakama ya Rufaa yatupilia Mbali Maombi ya DPP ya Kuongeza Ushahidi Katika Kesi ya Tundu Lissu

Mahakama ya Rufaa yatupilia Mbali Maombi ya DPP ya Kuongeza Ushahidi Katika Kesi ya Tundu Lissu

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
304
Reaction score
1,379
Leo, tarehe 30 Julai 2026, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetoa uamuzi muhimu katika shauri lililomhusisha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Tundu Antiphas Lissu. DPP alikuwa amewasilisha maombi ya kupitia upya uamuzi wa Mahakama Kuu uliokataa jaribio la upande wa mashtaka la kuwasilisha ushahidi mpya.

IMG_6303.jpeg

Kiini cha Mzozo
  • Upande wa mashtaka ulitaka kuwasilisha ushahidi wa ziada kupitia shahidi wao, ACP Amini Mahamba, ambaye alikuwa kiongozi wa timu ya uchunguzi wa matukio yaliyohusiana na Uchaguzi Mkuu wa 2025.
  • Lissu, ambaye alijitetea mwenyewe, alipinga vikali hatua hiyo.
  • Alieleza kuwa Kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kinaruhusu tu upande wa mashtaka kumwita shahidi mpya ambaye ushahidi wake haukusomwa wakati wa taratibu za awali, na sio kuongeza ushahidi mpya kutoka kwa shahidi ambaye tayari alikuwa ametoa ushahidi.
  • Awali, Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja za Lissu na kufutilia mbali notisi ya upande wa mashtaka kwa kuwa na mapungufu kisheria.
Uamuzi wa Mahakama
  • Mahakama ya Rufaa imeunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu, ikieleza kuwa Kifungu cha 308 cha CPA kimewekwa maalum kwa ajili ya kumleta shahidi ambaye ushahidi wake haukuwahi kusomwa kwa mshtakiwa.
  • Majaji wamefafanua kuwa sheria haiweki masharti ya kutoa kibali cha kumwita tena shahidi aliyepo ili kutoa ushahidi mpya au wa ziada.
  • Kutokana na hilo, Mahakama imeamua kuwa notisi ya upande wa mashtaka ilikuwa na makosa na hivyo kutupilia mbali maombi yote ya DPP kwa kukosa mashiko.
Ombi la Fidia lakataliwa
  • Wakati wa shauri hilo, Lissu aliomba kulipwa fidia kwa kutumia siku 139 akiwa rumande wakati kesi ya msingi ikiwa imesimama kupisha maombi haya, akidai yalifunguliwa kwa usumbufu ili kuchelewesha kesi.
  • Mahakama imelikataa ombi hilo.
  • Majaji wameeleza kuwa hawana mamlaka ya kutoa amri hiyo kwa sababu wao si mahakama ya mwanzo, na sheria inaelekeza kuwa fidia inaweza kuamriwa tu baada ya mshtakiwa kuachiwa huru moja kwa moja endapo itabainika kuwa mashtaka yalikuwa ya usumbufu.
Soma Pia: Tundu Lissu: DPP anilipe fidia kwa taabu aliyonisababishia kwa siku 139
 
Attachments

Leo, tarehe 30 Julai 2026, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetoa uamuzi muhimu katika shauri lililomhusisha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Tundu Antiphas Lissu. DPP alikuwa amewasilisha maombi ya kupitia upya uamuzi wa Mahakama Kuu uliokataa jaribio la upande wa mashtaka la kuwasilisha ushahidi mpya.

View attachment 3640052
In fact,
katika uchunguzi zaidi unaondelea dhidi ya mtuhumiwa huyo wa uhaini, ushahidi mpya umepatikana na ni wa wazi kabisa ili kuthibitisha makosa ya mtuhumiwa huyo.

nazisihi mahakama huru za Tanzania, kuukubali na kuupokea ushahidi huo muhimu sana, usio na shaka dhidi ya makosa ya uhaini yanayomkabili huyo kibaraka mropokaji wa mabwenyenye ya magharibi 🐒
 
Bakora za mabeberu zinafanya kazi , kusikia kwa kenge hadi damu itoke masikioni.

Huku EU, huku US Senate, huku commonwealth, huku ICC muuaji wa Kizimkazi hawezi kuchomoka pote.

Soon watamwachia Lissu bila masharti sababu hakuna uhaini wowote hapo kwa nchi yenye mahakama zinaozojitambua.

Cc : Vidampa wa Samuya muuaji Lucas Mwashambwa ChoiceVariable
 
In fact,
katika uchunguzi zaidi unaondelea dhidi ya mtuhumiwa huyo wa uhaini, ushahidi mpya umepatikana na ni wa wazi kabisa ili kuthibitisha makosa ya mtuhumiwa huyo.

nazisihi mahakama huru za Tanzania, kuukubali na kuupokea ushahidi huo muhimu sana, usio na shaka dhidi ya makosa ya uhaini yanayomkabili huyo kibaraka mropokaji wa mabwenyenye ya magharibi 🐒

Gentleman! Unaleta usia kwenye sheria? Huwa sipendi unavyotukanwa, lakini kuna muda huwa unaalika matusi kwa makusudi kwa kutojua kwako. 😊
 
Back
Top Bottom