Jeshi la Polisi Kutozingatia Sheria ni kwa Sababu ya Kukosa Weledi au ni Kiburi?

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,055
Kati ya mambo ambayo hufanya jeshi la polisi na polisi wa wetu wa Tanzania kudharaulika na kuonekana limejaza watu wasio na weledi au weledi mdogo, ni pale linapofanya mambo kinyume cha sheria, au kujipa mamlaka ambayo halina.

Jeshi la polisi linapotenda mambo kinyume cha sheria labda kwa sababu tu lina bunduki na mabomu, linakuwa halina tofauti na kikundi cha uhalifu.

Ni muhimu sana jeshi la polisi kujitenga kabisa na matendo yasiyo halali kisheria dhidi ya raia au kujipa mamlaka isiyokuwa nayo dhidi ya raia, eti tu kwa sababu ni chombo cha dola.

Jeshi la polisi linasimamia sheria. Lenyewe linatakiwa kuwa mfano wa kutii sheria. Na huwezi kusimamia sheria vizuri kama huzijui sheria vizuri.

Ni muda mrefu, watu wakiliandikia barua jeshi la polisi kulitaarifu kuwa wanakusudia kufanya maandamano, utasikia eti jeshi la polisi limezuia maandamano au eti limetoa kibali cha maandamano! Loh! Huu ni ujinga wa hali ya juu. Yaani ndani ya jeshi zima la Polisi, hakuna anayeweza kuisoma vizuri sheria inayoongoza maandamano na akatoka na tafsiri sahihi ya sheria ili Jeshi la Polisi lisimamie vizuri sheria?

Hakuna mahali ndani ya sheria inayohusu maandamano ambapo jeshi la polisi limepewa mamlaka ya kutoa kibali cha maandamano au kuzuia maandamano, palewaandaaji wa maandamano wanapolitaarifu jeshi la polisi.

Polisi wanapewa tu taarifa, hawaombwi au kuulizwa. Jeshi la polisi wajibu wake ni kusimamia tu hayo maandamano na kuhakikisha hakuna anayevunja sheria za nchi wakati huo wa maandamano.

Utetezi pekee ambao jeshi la polisi lina uwezo wa kutoa kwa waandaaji wa maandamano, ni kukosekana kwa askari wa kutosha kusimamia usalama wa maandamano, kama kuna shughuli nyingine zinazohitaji pia idadi kubwa ya askari. Ikiwa hivyo, ni juu ya waandaaji wa maandamano kuamua kuendelea na maandamano yao bila ya ukinzi wa polisi au kusubiria muda sahihi ambao polisi watakuwa na askari wa kulinda usalama wa waandamanaji na watu wengine wakati wa maandamano.

Lakini polisi hawana mamlaka kabisa ya kisheria au kikatiba ya kusema wamezuia maandamano au wameruhusu. Wananchi wameruhusiwa na katiba, hawahitaji ruhusa ya polisi. Kwa sababu maandamano ni namna nyingine ya kikatiba ya wananchi kuwasilisha malalamiko yako pale uwakilishi unapokuwa umeshindwa kufikia matarajio ya wananchi, au pale anayelalamikiwa anapokuwa amepuuza matakwa ya umma kupitia wawakilishi au maelekezo ya sheria na katiba.

Vitu hivi ambavyo ni very basic inapoonekana polisi hawafahamu, unajiuliza kule kwenye chuo chao huwa wanafundishwa nini?

Nchi hii tuna safari ndefu sana kuyafikia maendeleo ya kweli na ustaarabu kwa sababu vyombo vya dola na viongozi wa Serikali ndio watu wanaoongoza katika kukiuka na kutotii sheria. Mfano mdogo, endesha gari, uone magari ya vyombo vya ulinzi na usalama, magari ya viongozi wa Serikali na chama tawala yasivyozingatia sheria za usalama barabarani. Yaani watu waliotakiwa kuifundisha jamii kwa matendo mema, ndio wamekuwa mfano mzuri wa uovu.

Tuanzie wapi kulibadilisha hili Taifa? Maana kila mahali ni uozo mtupu!!
 
Kigezo cha kujiunga na jeshi la police ni kuwa na division 0 kwenye matokeo ya kielimu, binafsi nitalivunja hili jeshi na all above 40yrs ninawastaafisha,young graduates watachukua nafasi zao, traffic officer's kama 1000 training ndani ya GABS kwenye zero corruption
 
1. Tii Shuruti bila Sheria.

2. Kigogo mmoja mstaafu wa Jeshi la Polisi aliwahi kuniambia kwamba "wakati wa kuajiriwa wao Mapolisi huwa wanapimwa Urefu tu, na kamwe huwa hawapimwi Akili" kwa hiyo wasilaumiwe kwa jambo lolote ambalo linahusisha matumizi ya akili.
 
CCM ndio sheria kwa jeshi la polisi!!! Kikubwa ni kutii maagizo ya wanasiasa wa CCM!! Over
 
Kati ya mambo ambayo hufanya jeshi la polisi na polisi wa wetu wa Tanzania kudharaulika na kuonekana limejaza watu
Kwahiyo wanakuwa wazuriiii pale wanapolinda chadema kwenye mikutano ya siasa au pale tundulisuu anapolindwa hapa ndioo polisi mnawafagilia. Ila wakilinda amanii na kufukuza magenge yawavunja amani, hapo polisi Huwa ni hovyo huko kwenuuu
 
1. Tii Shuruti bila Sheria.

2. Kigogo mmoja mstaafu wa Jeshi la Polisi aliwahi kuniambia kwamba "wakati wa kuajiriwa wao Mapolisi huwa wanapimwa Urefu tu, na kamwe huwa hawapimwi Akili" kwa hiyo wasilaumiwe kwa jambo lolote ambalo linahusisha matumizi ya akili.
Sasa titaendelea na jeshi la namna hii mpaka lini? Unapokuwa na msimamizi wa sheria ambaye ni zero brain, atawezaje kusimamia sheria?

Ndiyo sababu tuna polisi ambao hawajui chochote zaidi ya kusema, kaa chini, au nitakupeleka kituo cha polisi.
 
Kigezo cha kujiunga na jeshi la police ni kuwa na division 0 kwenye matokeo ya kielimu, binafsi nitalivunja hili jeshi na all above 40yrs ninawastaafisha,young graduates watachukua nafasi zao, traffic officer's kama 1000 training ndani ya GABS kwenye zero corruption
PIa ni kazi ya laana
 
Sasa titaendelea na jeshi la namna hii mpaka lini? Unapokuwa na msimamizi wa sheria ambaye ni zero brain, atawezaje kusimamia sheria?

Ndiyo sababu tuna polisi ambao hawajui chochote zaidi ya kusema, kaa chini, au nitakupeleka kituo cha polisi.
Wanachofundishwa ni kupiga pekee
 
Kwahiyo wanakuwa wazuriiii pale wanapolinda chadema kwenye mikutano ya siasa au pale tundulisuu anapolindwa hapa ndioo polisi mnawafagilia. Ila wakilinda amanii na kufukuza magenge yawavunja amani, hapo polisi Huwa ni hovyo huko kwenuuu
Wewe ni polisi? Nasikia huko wanaangalia tu urefu, na siyo.akili au uwezo wa kufundishika.

Loh, huelewi hata kinachojadiliwa!
 
Kama maandamano ni haki ya kikatiba iweje polisi waingilie maandamano ambayo hayajaleta uvunjifu wowote wa amani, nchi zote ambazo mnaiga ustaarabu watu huwa wanaandamana hadi kwa maelfu na polisi kazi yao ni kuhakikisha usalama wa hayo maandamano, siyo kukamata na kupiga watu.​
 
Wewe ni polisi? Nasikia huko wanaangalia tu urefu, na siyo.akili au uwezo wa kufundishika.

Loh, huelewi hata kinachojadiliwa!
Polisi wanakidhi vigezo pale wanapolinda kwenye ilemikutano yenu ya +255 tuuu. Ila wakitimua vibaka wanaoleta fujo kwenye jamiii hapo Huwa vigezo vyao mnavishushaa. Hovyo kabisaa
 
Kama maandamano ni haki ya kikatiba iweje polisi waingilie maandamano ambayo hayajaleta uvunjifu wowote wa amani, nchi zote ambazo mnaiga ustaarabu watu huwa wanaandamana hadi kwa maelfu na polisi kazi yao ni kuhakikisha usalama wa hayo maandamano, siyo kukamata na kupiga watu.​
Kwahiyo polisi waruhusu watu KUTENGENEZA vigenge vigenge barabarani eti nimaandamanoo?
 
Hua wanapoenda kule kwanza wanakaririshwa kwamba wao sio raia tena....😝
Sasa wanapo rudi mtaani wanakua wmekariri kwamba wao sio raia, na shida ndipo huanzia hapo....😎
 
Back
Top Bottom